Wanafunzi 1000 Hawana Sifa IFM

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
WANAFUNZI zaidi ya 1000 wapo hatarini kufukuzwa katika Chuo cha Usimamaizi wa Fedha [IFM] baada ya kubainika kukosa sifa za kujiunga katika vyuo vya elimu ya juu nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa chuo hicho na kubandikwa kwenye mbao za matangazo wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza ambao majina yao yaliorodheshwa walitakiwa kuwasiliana na uongozi huo.

Taarifa hiyo ilikwenda sambamba na kutajwa kwa wanafunzi hao ambao hawakuwa na sifa kwenda kwa msajili wa chuo kuhakiki majina yao na kuwasilisha vyeti vyao vya kumaliza elimu ya sekondari.
 
Kwa hiyo chuo kinakubali makosa ya/udhaifu wa kudahili wanafunzi wasio na sifa ? Makosa hayo yametokea bahati mbaya au yalikuwepo katika miaka ya nyuma pia ?
 
Mama,

Nimesoma hiyo taarifa nikafikiria the same thing, same exact thing! Inabidi chuo kilipotoa hiyo revelation, yeyote waliyemwambia, ilibidi waulizwe, ilikuwaje sasa wakawa admitted? Yani hii siyo skandali la wanafunzi kufanya usanii, ni skandali la chuo!
 
Kwa hiyo chuo kinakubali makosa ya/udhaifu wa kudahili wanafunzi wasio na sifa ? Makosa hayo yametokea bahati mbaya au yalikuwepo katika miaka ya nyuma pia ?

Hiyo inawezekana mzee
 
Kama wana udhahifu si waanzishe masomo ya pre-college? Elimu mnaifanya kuwa complicated, na kitu anachofanya mwanafunzi akimaliza shule ni kuwa Muhasibu tu.
 
Hiyo inawezekana


Kwa hiyo kama hiyo inawezekana basi Tanzania ni kaput education-wise. Tunashangilia kuwa na magraduate wengi ambao hawana sifa za kuwa graduates. Wakishindwa kudeliver makazini tunalalamika...au waajiri wakiajiri magraduate wageni tunalalamika.

Tanzania yangu maskini, imeoza kila pahala. Na huu upungufu kwenye education system utatucost generations and generations; kama hatua mahsusi na madhubuti zisipochukuliwa haraka iwezekanavyo kurekebisha haya mapungufu.
 
Wawachunguze pia na malecturer wao hasa waliosoma hapo hapo, nadhani wengi tu wataumbuka. Haka kamchezo kalianza zamani sana pale IFM.
 
Kwa hiyo chuo kinakubali makosa ya/udhaifu wa kudahili wanafunzi wasio na sifa ? Makosa hayo yametokea bahati mbaya au yalikuwepo katika miaka ya nyuma pia ?

Hongo zilitembezwa wakati wa admission!
 
They need to be serious tumechoka na vihiyo makazini unaweza kuta ndo hao hao wa Richmond,EPA,IPTL etc
 
Wana JF hebu tupeni habari za jikoni zaid inawezekanaje watu 1000 wafoji vyeti na wakafanikiwa kupata admission. That's technical blunder to the University Management!. Watu 1000 ni wengi sana kwa scope ya IFM is like wote wamefoji, nadhani hii ni weakness kubwa kwa uongozi wa IFM ni vema ukachunguzwa. Hii inaashiria swala hili limekuwa likifanyika toka siku za nyuma kwani ni ngumu just once to incounter 1000 forgery cases.

Anyway tunashukuru kwa kuliweka wazi hili nadhani next time tuangalie na quality ya vyuo vyetu visiwe too commercial bila kuangalia standard.
 
kwamba kuna rushwa ktk kusajili wanafunz wapya sio sual la kuulizwa. vyuoni kuna rushwa kama zilivyo sehemu zingine pia. hii inasababisha waombaji wenye sifa wazikose hizo nafasi
lakin pia kusajili wanafunz wengi inaweza kuwa njia ya kuongeza income
taratibu zao za kutoa 'result slips' zina mushkeli pia. hii inawezafanya mhitimu aliyepata alama c, b+, c, c, b, c kwa mfano aandikiwe kapata b, b+, b, b, a, b katika mfuatano huo.
cheti kitaonekana kinapendeza tofaut na ilivyostahili.
lakin hili si la pale tu. vyuo vingine vingi hapa tz hali ni hiyohiyo na wala wahusika hawaonekani kulitilia maanani.
nimewahi kushuhudia kwenye chuo fulani mhitimu analalamika kakosa zawadi ya kufaulu vizuri kuliko wote somo fulani. hiyo zawadi aliipata mwingine ambaye hakustahili. hii inamaana kuwa kumbukumbu za matokeo ya mitihani zinaweza kuchezewa
 
inaweza kuwa njia ya kuongeza income
taratibu zao za kutoa 'result slips' zina mushkeli pia. hii inawezafanya mhitimu aliyepata alama c, b+, c, c, b, c kwa mfano aandikiwe kapata b, b+, b, b, a, b katika mfuatano huo.
cheti kitaonekana kinapendeza tofaut na ilivyostahili. hii inamaana kuwa kumbukumbu za matokeo ya mitihani zinaweza kuchezewa

kama hali imefikia hivyo basi tunaenda pabaya
 
Itabidi waanzie walio mwaka wa 3 maana kumejaa vimeo pale IFM Ndio wengi wanatoka hapo kwenda Taasisi zetu nyeti za Fedha.
 
Back
Top Bottom