kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
Wadau nimeshitushwa na kutahayari baada ya kupokea ujumbe wa whatsapp unaosambazwa kwa kasi katika magroup ya wana ukawa na chadema, wakihamasishana kupiga kura kwa wingi ili Rais John Pombe Magufuli ambaye amechaguliwa kuwa ni miongoni mwa wanaoshindania tuzo ya FOBES ya watu mashuhuri kwa mwaka 2016 Afrika.
Ujumbe huo unawataka wana ukawa na Chadema kumpigia kura mtu wa Rwanda ili Rais Magufuli asishinde tuzo hiyo, sehemu ya ujumbe huo inasema hivi “Tupige kura THE PEOPLE OF RWANDWA ili asishinde na tusigawe kura kuonesha kuwa kuminya DEMOKRASIA HAKUMPI MTU UMASHUHURI."
Katika ujumbe huo ambao wameambatanisha na link ya fobes ambayo ndio wanapoingia wapiga kura na kumchagua mshindi wa tuzo hiyo ya FOBES, wameweka maneno haya, ingia apo usimpigie kura Magufuli pigia peole of Rwandwa makamanda tujitahidi sana.
Maoni yangu
Kwanza nasikitika sana kwa chadema kufanya mambo ya hovyo hovyo kabisa kwa kuendekeza siasa na kuacha uzalendo, inaonekana hata ikitokea nchi tukaingia vitani na maadui wa Tanzania hawa jamaa watawaunga mkono maadui kwa kuendekeza siasa, ifikie hatua tusifanye siasa kama usimba na yanga yanapojitokeza mambo ya kitaifa kama hili hatuna budi kuungana jambo linapomalizika tuendelee na ushabiki wetu kisiasa. Binafsi hata kama simkubali Mbowe na Lowassa lakini kama wangekuwa nao washiriki katika Tuzo hiyo ningewachagua kwa kuwa tu ni Watanzania wenzangu na heshima kwa taifa pia.
Pili Hata kama hawataki lakini wanapaswa kujua kuwa Rais Magufuli ni maarufu hata kama asingeshindwanishwa katika tuzo hiyo, nafasi yake ya urais na harakati zake za kuondoa kero na zinazowakabiri watanzania vimemfanya awe maarufu kulikoi hiyo tuzo anayoshindanishwa, wanajisumbua tu kwa kuendesha kampeni ambazo haziwasaidii lolote katika siasa zao zaidi watanzania tutazidi kuwapuuza kwa ujinga na uhovyo wao.