Wana JF karibuni....

Jeho

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
5,053
5,504
Kwa kuanza napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kuniruhusu niendelee kula licha ya uovu mwingi ninaotenda kila siku hapa duniani. Pia kwa wale ambao ndugu, marafiki na jamaa zao walikatishwa na mwenyezi Mungu kuendelea kula, nachukua muda huu kuwapa pole.
Waliotangulia kuona jua kabla yetu walisema "kila lenye mwanzo halikosi mwisho", ndugu na rafiki zangu wana JF, hatimae zile siku 60 ili niapishwe kuwa WAZIRI WA UPUUZI NA MIPANGO YA GHAFLA GHAFLA zinahitimishwa kesho. Napenda kuchukua muda huu kuwakaribisha katika sherehe hizo zitakazofanyika mnamo saa 10:30 jioni. Baadhi ya mambo ambayo wizara yangu itayashugulikia ni haya yafuatayo.
1. Kuhamasisha wananchi kuacha upuuzi wa kuchagua viongozi njaa na wasiokuwa na uwezo wa kupigania maslahi ya wapigakura wao.
2. Kuelimisha wananchi waache upuuzi wa kuiga kila wanachoona katika vioo vyao vinavyofanywa na wazungu, badala yake waige yale mazuri tu.
3. Kuelimisha wananchi waache kusikila maada za kipuuzi kama ile ya udini, maana hakuna mwenye uhakika wa dini yake kama inakubalika mbele za mwenyezi Mungu, maana haya ni mapokeo tu na zaidi kila mtu anaabudu dini aliyopo kutokana na dini hiyo kuwa ya kwanza kuingizwa eneo lake.
Mambo ya upuuzi ni mengi sana, lakini hayo hapo juu ni kwa uchache tu.
WanaJF wote mnakaribishwa sana.
Ndimi WAZIRI MTEULE WA UPUUZI NA MAMBO YA GHAFLA GHAFLA.
 
siku moja nitakuja na mada ya historia ya dini zetu.
Nadhani tukijaribu kuelewa hilo litatusaidia kuchukuliana na kuishi kwa amani zaidi.
 
siku moja nitakuja na mada ya historia ya dini zetu.
Nadhani tukijaribu kuelewa hilo litatusaidia kuchukuliana na kuishi kwa amani zaidi.

Inatakiwa uilete mapema sana maana huu upuuzi wa udini hata hapa JF wapo baadhi walioshindwa kabisa kuachana nao.
WAZIRI WA UPUUZI NA MIPANGO YA GHAFLA GHAFLA.
 
Oooh! Kumbe kuna mambo mengine ambayo yalitakiwa niwe nimekamilisha ndani ya siku sitini. Mambo hayo ni.
1. Kufunua faili jipya- kwa huzuni kubwa napenda niseme hili halikufanikiwa maana mafaili yote yameshafunguliwa.
2. Kesho baada ya kuapishwa nitaanzisha slogan ya " study BIBLE as you live forever, and PRAY to your GOD as you die at the moment you are PRAYING".
WAZIRI WA UPUUZI NA MIPANGO YA GHAFLA GHAFLA.
 
WAZIRI WA UPUUZI NA MIPANGO YA GHAFLA GHAFLA anapenda kuwajulisha wanaJF wote kuwa jana aliapishwa rasmi na toka jana amezindua slogan ya STUDY BIBLE AS YOU LIVE FOREVER AND PRAY TO YOUR GOD AS IF YOU WILL DIE AT THE MOMENT YOU ARE PRAYING. Na slogan hii ndiyo inatumika pia kama signature. Naomba ushirikiano wenu.
 
pamoja sana... waziri wa upuuzi.
 
Back
Top Bottom