Wamarekani lile jiji la New York waliamua aisee!

Bro hiyo miji mi nimekwenda sana miaka ya 2012 huko Sasa natembea na picha kwenye cm mpaka leo za nini. Ila ukitaka picha mbona zipo hewan unagoogle tu simpo Mzee.
Uzi unao endana na picha humoga sana. Unadhani sijawahi pota youtube kuangalia walking through newyork?
 
Kuna jambo nimeamua kushea kidogo humu.

Kwa kazi yangu nashukuru Mungu nimetembea tembea kidogo katika majiji mengi makubwa duniani.

Nilipofika New York Marekani, aisee lile jiji ni zuri sana. Wiki mbili nilizokaa niliziona chache sana. Wenyeji wangu walinitembeza sana, nilienjoy mno, nilikuwa na wakati mzuri sana. (Naamini kuna siku nitarudi tena).

Nilimelitaja jiji la New York kuwa zuri sana nikilinganisha na majiji niliyowahi kufika ingawa yote sikuwahi kukaa zaidi ya mwezi. (Unaweza kupingana na mimi kwa majiji ambayo umewahi kufika mimi sijawahi)

Majiji yenyewe ni haya:

Afrika.
Bujumbura(Burundi), Nairobi, Kisii na Kisumu(Kenya), Blantyre, Karonga, Mzuzu, Zomba na Lilongwe(Malawi), Maputo, Cabo Delgado, Tete na Chimoio (Msumbiji), Luanda na Calulo (Angola), Kinshasa na Lubumbashi (DR Congo), Johannesburg((Afrika Kusini)

Ulaya
Frankfurt na Berlin (Ujerumani), London (England), Helsinki(Finland), Paris (Ufaransa)

Midlle East
Beirut (Lebanon)

Asia
Hon Kong na Beijing (China), Seoul (Korea Kusini), New Delhi na Mumbai (India)

Latin America
Huku sikufika katika nchi tano tu (Argentina, Paraguay, Uruguay, Chile na Venezuela) zingine zote nimefika

North Amerika
Marekani(New York)

Hitimisho langu, katika majiji yote hayo niliyofika mimi, kwakweli nakiri kabisa, New York ni JIJI haswa.

Halafu kwa jiji la Kinshasa kule DR Congo kwangu mimi binafsi Dar es Saalam bado tuko nyuma sana. Kabla hujafika ukisikia mambo ya vita ya Congo unaweza kudhani Kinshansa ni kajiji tu kahovyo, lakini aisee, nalo ni jiji kweli kweli.
Mkuu mbona unatupanga hv.....Hata Kinshasha na Nairobi na Bujumbura??????
 
Back
Top Bottom