Wamarekani lile jiji la New York waliamua aisee!

Kuna jambo nimeamua kushea kidogo humu.

Kwa kazi yangu nashukuru Mungu nimetembea tembea kidogo katika majiji mengi makubwa duniani.

Nilipofika New York Marekani, aisee lile jiji ni zuri sana. Wiki mbili nilizokaa niliziona chache sana. Wenyeji wangu walinitembeza sana, nilienjoy mno, nilikuwa na wakati mzuri sana. (Naamini kuna siku nitaruri tena).

Nilimelitaja jiji la New York kuwa zuri sana nikilinganisha na majiji niliyowahi kufika ingawa yote sikuwahi kukaa zaidi ya mwezi. (Unaweza kupingana na mimi kwa majiji ambayo umewahi kufika mimi sijawahi)

Majiji yenyewe ni haya:

Afrika.
Bujumbura(Burundi), Nairobi, Kisii na Kisumu(Kenya), Blantyre, Karonga, Mzuzu, Zomba na Lilongwe(Malawi), Maputo, Cabo Delgado, Tete na Chimoio (Msumbiji), Luanda na Calulo (Angola), Kinshasa na Lubumbashi (DR Congo), Johannesburg((Afrika Kusini)

Ulaya
Frankfurt na Berlin (Ujerumani), London (England), Helsinki(Finland), Paris (Ufaransa)

Midlle East
Beirut (Lebanon)

Asia
Hon Kong na Beijing (China), Seoul (Korea Kusini), New Delhi na Mumbai (India)

Latin America
Huku sikufika katika nchi tano tu (Argentina, Paraguay, Uruguay, Chile na Venezuela) zingine zote nimefika

North Amerika
Marekani(New York)

Hitimisho langu, katika majiji yote hayo niliyofika mimi, kwakweli nakiri kabisa, New York ni JIJI haswa.

Halafu kwa jiji la Kinshasa kule DR Congo kwangu mimi binafsi Dar es Saalam bado tuko nyuma sana. Kabla hujafika ukisia mambo ya vita ya Congo unaweza kudhani Kinshansa ni kajiji tu kahovyo, lakini aisee, nalo ni jiji kweli kweli.
Kinshasa....👍👍
 
Eti New York!...... Eti New York!.... New York ya Nyooko!...!!!

Hivi hiyo new York unadhani ni kama ushirombo eh!!? ..... Unaichukulia kirahisi rahisi hivyo eeh!?......

Vimiji vya kusini mwa jangwa la sahara umevitaja vizuri vyoote....kwa msaada wa google maps....

Ila kulee .....New York yenyewe sasa! Og!......teh!....! Mtihani!
Umasikini wa mali na akili! #kataaUmasikini
Dream Queen
 
Ukitembelea majiji kama hayo kazi sio kujifotoa picha tu bali kuchukua picha za mitaa mbalimbali iliyokuvutia majengo open spaces hotel rooms madhari ya mje ya hoteli n.k sasa ulifeli wapi?
Ungejua tunavyokuwaga basi tu. Mara nyingi tunapenda self kwenye sehemu nzuri nzuri. Ukipiga sehemu peke yake ukirudi bongo hakuna cha kuwatambia wana ofisini watasema umegoogle
 
Hongera sana kiongozi kwa ku explore the world
Binafsi sioni New York likiwa jiji zuri la kukaa, kwanza ni very populated, wanakaribia 9mil. Pamoja na kuwa na majengo mengi yaliyopangika ila mengi ni ya zamani miaka 1980 kurudi nyuma hadi 1950 hivi.
Kwa Marekani majiji ninayo yapenda sana ni kama Los Angeles au Chicago; yamejengeka vizuri sana na pupulation ndogo (karibia Nusu ya Dar).
Kwa mtu anayependa miji mizuri na kuenjoy mazingira yasiyo na Purkushani; hiyo ndio miji ya kutembelea.
Kwa hapa Africa Capetown is the best kwa wanaopenda miji mizuri na iliyotulia
Ushahidi upo wazi; Angalia hata kile kiwanja chao cha ndege maarufu sana hapo New York kijulikanacho kama John F Kennedy (JFK)ni cha kizamani ilijengwa miaka ya 1960 na huwezi kukilinganisha na viwanja vya kisasa kama vilivyopo Nchi za Kiarabu na Asia kwa ujumla. Hata hivyo wanampango wa kujenga termina III hapo JFK ambayo naamini itakuwa ya kisasa sana
Ukweli sijafika huko Ila naijua vizuri miji ya dunia kupitia World Tourisim Geography niliyosoma miaka hiyo....
 
Back
Top Bottom