Waliovuma Kwaya ya Ulyankulu barabara ya 13 Tabora

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,192
Kwaya ya Ulyankulu barabara ya 13 Tabora ilikuwa kwaya ilivuma na kushika chati za nyimbo za injili na ninakumbuka wazazi wangu walikuwa wapenzi wakubwa na tuangalie video yao kali ingawa walitokea kitongoji kidogo huko Tabora miaka nadhani ya 1970/80

 
Last edited by a moderator:
Mkuu ubarikiwe sana!! Enzi hizo nyimbo zilikuwa na alot of feelings kwani watu walikuwa wanaimba kwa hiari zao bila kusukumwa na mauzo zaidi ya album.
 
Lazima utabarikiwa ukisikiliza nyimbo zao. Mmbarikiwe sana.
 
ebwana mada imenigusa sana. Nimekumbuka mbali back in the days 1988 up2 mid 1990s wakati choir hii ilipokuwa imeteka muziki wa injili hapa nchini na afrika mashariki kwa ujumla. Nakumbuka wakati huo nilikua bado kijana mdogo naishi kwa wazazi. Kila toleo lao yani vol. Halikuwahi kukosekana pale nyumbani. Nakumbuka baba yangu alipokuwa akija na cassete tape ya choir hii alituita wote wanafamilia tuje kusikiliza. Wakati huo hakukuwa na cd wala dvd mwendo radio cassete tena zile zenye disko light pembezoni mwa spika. Ah i wish i cud bring back those good days. Nakumbuka tulikua tunabarikiwa sana kwa tungo na beats na mirindimo ya magitaa ya choir hii. Nakumbuka nyimbo zao km. Kwa viumbe, mateso ya ayubu,samson n.k kwakweli ya kale dhahabu. Yani kweli choir za zamani zilikua kihuduma zaidi na siyo kibiashara kama sasa muziki wa injili umevamiwa na kilamtu hakuna ujumbe wa kibiblia kama zamani. Nakumbuka kwaya nyingi zilitoa jumbe kutoka mistari ya biblia. Ilinifanya nitamani kuisoma nipate undani wa yale yalokuwa yakiimbwa. Jamani kwaya zote za kuanzia miaka ya 70 mpaka 90 zilikuwa nzuri sana. Nafkiri kuna haja ya waimbaji wa sasa wajifunze mengi kutoka ya kale. Tena ikibidi warudie nyimbo hizo au wafanye sample ya vyombo vilivyotumika zamani ktk beats.
 
ebwana mada imenigusa sana.
Nimekumbuka mbali..................
Nakumbuka wakati............
Halikuwahi kukosekana.........
Nakumbuka baba yangu..........
Wakati huo............
Nakumbuka tulikua...........
Nakumbuka nyimbo...........
Yani kweli.................
Nakumbuka kwaya..........
Jamani kwaya...........
Nafkiri kuna.........
Tena ikibidi.............

Hakika Mpendwa Imekugusa. Ubarikiwe sana!
 
Back
Top Bottom