Walioruhusu picha hii itumike hawakuwa wajinga

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,697
106,862
I hope y'all are doing just fine, It has been long time since I was here[JF Inteligence]
1678527001054.png

Kuna mtu alileta mada humu akiuliza kwamba picha inayotumiwa na wakristo hasa wakatoliki ya mtu mmoja mzungu kua “ndie” yesu, je hiyo picha ni ya Yesu kweli? Akaongeza kwa kusema kwamba wakati yesu akiwepo kulikua hakuna teknolojia ya Photography wala Motion Picture…So wao waliitoa wapi picha hiyo na wana ushashidi upi kwamba yule ndio Yesu mwenyewe??

I’m glad you asked coz I would like to use this moment to Splendid Explain these stuffs to you!


Toka dunia kuumbwa, dunia imeshuhudia kuzaliwa kwa watu wawili wenye akili zaidi.watu hao walikua wenye uwezo wa kujifunza mambo wao wenyewe yaani Autodidacts na walikua wana uelewa na uwezo wa kufanya mambo meengi kwa wakati mmoja yaani Polymaths…watu hao si wengine bali ni Imhotep kutoka Misri ya zamani (Ancient Egypt) na Leonardo Da’Vinci kutoka Sicily Rome.

Imhotep alikuwepo duniani Zaidi ya miaka 5000 kabla ya kuzaliwa kwa Da’Vinci, Da’Vinci kazaliwa miaka 600 iliyopita yaani 1400s.Imhotep alikua kuhani mkuu wa mungu mkuu wa wamisri aitwaye mungu jua Ra, mbali na hayo jamaa alikua mbobevu katika hesabu,fizikia na biology hivyo alijikita sana katika usanifu wa majengo na tiba mbalimbali. Ukiziona Pyramids zilizopo misri wala usidanganyike kua alien ndio wamejenga bali ni huyu Inhotep ndio alizisanifu.

Wagiriki walimuabudu huyu mtu kama mungu wao wa tiba kutokana na mchango wake mkubwa katika tafiti zake zi kitabibu.

Kwa waliosoma mada zangu kadhaa zilizopita nilielezea jinsi utawala wa Ugiriki ulivyotokea na kuanguka na matokeo yaliyotokea baada ya ugiriki kuanguka. Kwa ambao hawajasoma nitaelezea kwa ufupi sana nini kilitokea.
Miaka ya nyuma ugiriki ya zamani ilikua imeundwa na miji ipatayo 100 na kila mji na ulikua na utawala wake japo walikua wakiungana na kusaidiana pindi uvamizi unapotokea, enzi hizo superpower wa dunia alikua Persia yaani Iran ya sasa. Iran ilikua inajitanua kwa kuvamia maeneo na kuyachukua hapo ndio alipoikaribia Ugiriki akitaka aanze kuchukua mji baaada ya mji, hapo ndio unakutana kisa cha mfalme Leonidas wa jiji la Sparta.

Vumbi ilitimka kweli kwa wapenzi wa muvi waliotazama muvi ya 300 na 300 Rise of Empire wanaelewa.
Baada ya vamizi kadhaa zilizokua zinafanywa na nchi kubwakubwa wagiriki wakaamua kuungana na kutengeneza nchi moja ya Greece. Mikaka ikaenda akatokea alexander the great akaikuza sana Greek, akaanzisha mji wake ulioitwa Alexandria katika nchi ya Misri. Kipindi hicho misri ilikua ndio hazina na kitovu cha Elimu dunia nzima.
1678527410227.png

[Mwigizaji Gerald Butler aliyeigiza kama mfalam Leonidas wa sparta kutoka muvi ya ]

Wanafalsafa wengi na walienda hapo kusomea, hata mwandishi wa injili Luka alisomea hapo. Miaka ikaenda baada ya Ugiriki kuanguka Superpower aliyeibuka akawa Rome, Rome ilienda kuchukua kila kitu kilichokua misri wakakihamishia kwao. Maarifa yote yaliyokua Misri kwenye Maktaba ya kwanza kuanzishwa duniani yalihamishiwa Rumi.

Wakati nchi ya Israel ikitawaliwa na Rumi anazaliwa Yesu anafanya kilichomleta duniani kisha anafariki miaka 33 baadae, wafuasi wa Yesu wanaongenzeka na kupata ushawishi mkubwa katika serikali na maeneo mengi duniani.

Kwa wanaopenda Conspiracy, inasemaekana baada ya utawala wa Rumi duniani kuanza kuanguka watu wenye kufikiria mbali (futurist) wakiongozwa na mfalme Nero walikabidhi madaraka kwa wafuasi wa Yesu Kristo wa kipindi hicho ili Rumi iendelee kutawala dunia kupitia mlango wa nyuma (indirectly) ndipo ukristo ukatambuliko rasmi duniani kama Roman Catholic na wakapafanya Rumi kama ndio makao makuu ya Ukristo badala ya Yesrusalemu. (Sina uhakika kama nadharia hii ina ukweli ndani yake ila ina make sense sana maana wote twafahamu nguvu na ushawishi iliyonayo RC katika mataifa mbalimbali)

Miaka kadhaa tawala ya Rumi inaanguka, Ukatoliki ukawa umeenea maeneo mengi na ushawishi mkubwa ulimwenguni anazaliwa Leonardo Da’Vinci 1452, kutokana na uwezo mkubwa katika mambo mbalimbali kila alichokifanya kiliweza kua Perfecto. Davinci aliweza kuifanya tasnia ya uchoraji kua kubwa na yenye thamani sana kutokana na kazi zake bora na zenye kufikirisha za uchoraji.

Ni moja kat ya wachoraji wakubwa kuwahi ktokea hapa duniani kuna vitu kachora hakuna mwingine anayeweza kuchora labda urumie Powerful software…kama utanibishia jaribu kuchora duara na pembe nne vikiwa pamoja kama alivyochora mchoro wake wa Vitruvian man… Jamaa alikua anaweza kujichora yeye mwenyewe sura yake…Baadae anazaliwa Michelangelo ambae na kwa kiasi Fulani alijitahidi sana katika uchoroja unaweza kujionea michoro yake ya Sistine Chapel iliyopo hapo Vatican, lakini pia nae alibobea katika uchonganji (sculptures)
1678528173018.png

[Sistine Chapel]
Inahusiana vipi na Picha ya Yesu…?

Kama nilivyoeleza huko juu Baada ya Ugiriki na Misri kuanguka na Rumi kuibuka kama Superpower alibeba maarifa yote yaliyokua Rumi na Ugiriki na kuyahamishia Roma, hivyo baada ya rumi kuanguka kanisa katoliki likabaki limeshikilia maarifa kutoka pande zote za dunia hasa misri,ugiriki na Israel. Leo hii hakuna taarifa au maarifa ambayo hayapo Vatican…Vatican inamiliki moja kati ya eneo lenye kulindwa Zaidi duniani ambalo hua haiingii huko mtu bila ruhusu maalumu…Hata Pope inabidi apate kibali kutoka kwa kiongozi wa Jesuists ndio anaweza kwenda huko.

Hivyo basi sidhani kwamba kanisa katopliki wanaweza kua wameshindwa kupata piacha ya yesu wakati wameweza kumiliki taaroifa za kutoka kila pande ya dunia. Kama Plato,Socrate, nk picha zao zipo na waliishi miaka mingikabla ya yesu haiwezekani yeye picha yake isiweze kupatikana.

Nimesema kipindi hicho taaluma ya uchoraji na uchongaji ilitumika Zaidi katika kuweka kumbukumbu za watu mbalimbali ndio maana leo ukiitaka picha ya Plato unaipata, kuna watu wamejaliwa uwezo mkubwa wa uchoraji unaweza kumuelezea kwamba Fulani sura yake ipo hivi na hivi na akaichora kama ilivyo. Njia hii hutumiwa sana na mashirika ya usalama hususan FBI na polisi. Tena sasa hivi kuna msaada wa softwares yaani ukimuelezea mtu anakutulea mchoro kama picha halisi…hivyo basi natumaini hata picha ya yesu watu wa zamani walitumia njia hiyo kuhifadhi taswira ya Kristo.

Ndio maana utakuta picha hiyo inayotumika sura yake ipo mahali pote sio tofauti. Hata miaka ya 1970s wakati wanaandaa filamu ya yesu walijaribu watu Zaidi ya waigizaji 200 ambao watafanana na Sura hiyohiyo ni Brian Deacon pekee ndio alifanikiwa kufit kwenye role hiyo kutokana na sura yake kufanana na sura inayotumika kuwasilisha taswira ya Kristo.
Ndio maana wasiojua wanapoona hiyo taswira ya yesu hua wanasema kwamba ni sura ya mwigizaji Brian Deacon…Si kweli, kwa maarifa waliyonayo RC hawawezi ruhusu hilo.

So kwa kuhitimisha ni kwamba Wakatoliki kukubali kuruhusu picha hiyo ya Yesu kutumika sio wajinga hata kidogo kwamba hawafahamu taswira halisi ya Kristo.
 
Wakatoliki ndo wanatumia hyo , wao ndo Wana majibu kulingana na impression ya picha , Sisi wasabato tunazo zetu pia , sio picha halisi ya Yesu Ila zinatoa elimu fulan ya picha kuhusu huyo Yesu , na ni picha za kuchora computerized
Wasabato mnaupinga utatu mtakatifu, mnapinga fumbo la imani. Kristo alikufa, Akafufuka na atarudi tena. Nyie ndio wapinga kristo
 
Kwa watakaotaka kusoma zaidi..
 
Hebu tuwekee sura ya Borgio kwanza, ndio tutaelewana.
Unapenda Conspiracy?? Nilishawahi kuandika jambo hilo. Si kweli hata kidogo
 
Unapenda Conspiracy?? Nilishawahi kuandika jambo hilo. Si kweli hata kidogo
Porojo dot com.
 
Mkuu kwa heshima kabisa sikubaliani na fikra yako kwasababu zifuatazo;

Yesu wakati wa uhai wake hakuwa mtu maarufu bali umaarufu wake umekuja miaka mingi baada ya yeye kufariki na habari zake kutangazwa. Sasa kama hakuwa maarufu ni wazi watu walimpuuzia ndio maana hata wakamuua kama waalifu wengine.

Ilihitajika awe mtu maarufu ndipo kumbukumbu zake ziwepo kwa watawala hasa picha sababu alitakiwa kulipia achorwe, kumbukumbu za Yesu zilizopo ni stori za mambo aliyofanya. Ni sawa na stori za babu wa machifu kabla ya kuja mkoloni kamwe hutaona picha zao bali stori tu.

Angalau kwa Mtume Mohammed yeye alieneza dini ya uislamu, ingekuwa rahisi sana kwa picha za Mtume kuwepo sababu yeye ndio mtu aliyekuwa nyuma ya uislamu tofauti na Yesu ambaye hata Ukristo wenyewe hakuuhubiri sababu yeye alikuwa myahudi na alitumwa kwao wayahudi.

Hii picha ni dhana tu au ndoto za wanadamu wa kipindi cha utambuko wakaamua kuileta tuitumie.

Jambo lingine ni uvaaji, huo uvaaji sio wa miaka hiyo watu wa zamani naweza kusema walikuwa rafu sana kuanzia nywele kichwani, ndevu zao hadi mavazi sasa yeye ilikuwaje akawa smart hivyo?, wakati alikuwa ni mtoto wa seremala tu? Mfano mzuri ni vikkings angalia walivyokuwa rafu na miaka waliyoishi ndio sembuse Yesu aliyeishi 2000 nyuma?.

Tubaki tu na imani ila hakuna uhalisia hapo.
 
Maelezo yako umerelate na uko sahihi kabisa hapo zamani palikuwa na watu wengi hata Africa wenye uwezo wa kutengeneza picha hata kuchonga vinyago kwa imagination ya kupewa maelezo mtu fulani alikuwa hivi na hivi basi moja kwa moja wanaunda picture halisi au kinyago..

Ila kwa yesu wengi wanadai sura ilitokana na kile kitamba alichofutiwa damu na majasho na kipo makumbusho mpake Leo sijajua ni Vatican au Israel
 
Mkuu kwa heshima kabisa sikubaliani na fikra yako kwasababu zifuatazo;

Yesu wakati wa uhai wake hakuwa mtu maarufu bali umaarufu wake umekuja miaka mingi baada ya yeye kufariki na habari zake kutangazwa. Sasa kama hakuwa maarufu ni wazi watu walimpuuzia ndio maana hata wakamuua kama waalifu wengine.
Inawezekana walimpuuzia ila wale waliomfuata hawakumpuuzia. Ndio maana utaona miaka kadhaa kabla ya 100 baada ya kifo chake Wanazuoni kadhaa walifanya tafiti juu ya maisha yake na matendo yake. Kupitia wao tukapata vitabu mbalimbali vya injili vilivyo kwenye Bible na Marejea mbalimbali
Ilihitajika awe mtu maarufu ndipo kumbukumbu zake ziwepo kwa watawala hasa picha sababu alitakiwa kulipia achorwe, kumbukumbu za Yesu zilizopo ni stori za mambo aliyofanya. Ni sawa na stori za babu wa machifu kabla ya kuja mkoloni kamwe hutaona picha zao bali stori tu.
Kuchorwa kwake inawezekana ilikua organised na wafuasi wake sitaki kuamini kama walikosa pesa za kulipa wafuasi. I concur kipindi hiko taifa lake lilikua halimtambui kabisa
Angalau kwa Mtume Mohammed yeye alieneza dini ya uislamu, ingekuwa rahisi sana kwa picha za Mtume kuwepo sababu yeye ndio mtu aliyekuwa nyuma ya uislamu tofauti na Yesu ambaye hata Ukristo wenyewe hakuuhubiri sababu yeye alikuwa myahudi na alitumwa kwao wayahudi.
Unamaanisha nini kusema Yesu hakuuhubiri Ukristo? Au kwa kumaanisha Mwenyewe ndio alikua Kristo??
Hii picha ni dhana tu au ndoto za wanadamu wa kipindi cha utambuko wakaamua kuileta tuitumie.

Jambo lingine ni uvaaji, huo uvaaji sio wa miaka hiyo watu wa zamani naweza kusema walikuwa rafu sana kuanzia nywele kichwani, ndevu zao hadi mavazi sasa yeye ilikuwaje akawa smart hivyo?, wakati alikuwa ni mtoto wa seremala tu? Mfano mzuri ni vikkings angalia walivyokuwa rafu na miaka waliyoishi ndio sembuse Yesu aliyeishi 2000 nyuma?.

Tubaki tu na imani ila hakuna uhalisia hapo.
Viking walikua Savages, huwezi kufananisha vikings na watu wa mataifa mengine ndio maana walikua rafurafu.
Mwenyewe Kristo alisema kwa wafuasi wake kwamba Wakiondoka wachukue nguo mojamoja maana huko waendako watavishwa na kulishwa. So inawezekana hata yeue alivishwa kumbuka walikua na mfuko wao maalumu wa kuhifadhi pesa za mahitaji ambazo zilitoka kwa waamini
 
Maelezo yako umerelate na uko sahihi kabisa hapo zamani palikuwa na watu wengi hata Africa wenye uwezo wa kutengeneza picha hata kuchonga vinyago kwa imagination ya kupewa maelezo mtu fulani alikuwa hivi na hivi basi moja kwa moja wanaunda picture halisi au kinyago..
Teknolojia hii ipo miaka na miaka ndio maana utakuta michoro ya mafarao yenye miaka zaid ya 10000.
Ila kwa yesu wengi wanadai sura ilitokana na kile kitamba alichofutiwa damu na majasho na kipo makumbusho mpake Leo sijajua ni Vatican au Israel
Hili inaaminima hivyo ila sikutaka kuligusia maana lipo zaidi kiimani kuliko kiFact
 
Kwa maarifa na taarifa wanazomiliki Kanisa katoliki pale Vatican city Kwa mantiki ya maelezo yako basi hata picha au taswira ya Mtume Muhamad(Saw) Kwa wenzetu ndugu zetu sana Waislamu,wakatoliki wanayo.
Muhammad alikuwepo miaka 600 baada ya kristo sitaki kuamini warabu hawakutunza kumbukumbu yake maana nao walikua vizuri kiteknolojia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom