Waliochaguliwa vyuo vya ualimu 2014/2015

Kaplizer

JF-Expert Member
Apr 27, 2014
710
569

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA YA JUU (MIAKA 3) MWAKA WA MASOMO 2014/2015


MAELEKEZO:

Waombaji waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa masomo 2014/2015 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa tarehe 06/10/2014. Fomu za maelekezo (Joining Instructions) zitatolewa na chuo husika na zitatumwa kwa waliochaguliwa tu. Waliochaguliwa wanatakiwa kufika vyuoni wakiwa na mahitaji yaliyoainishwa kwenye fomu ya kujiunga na Chuo. Aidha, fomu hizi zinapatikana pia kwenye Tovuti ya Wizara:www.moe.go.tz; NACTE:www.nacte.go.tz; na TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz

Muhimu:

1. Waombaji waliochaguliwa ni wale wenye ufaulu wa Daraja la I hadi III

2. Waliochaguliwa wanatakiwa kuwasilisha Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani la Tanzania Kidato cha NNE na SITA (CSEE na ACSEE) na vyeti vya kuhitimu Elimu ya Sekondari na Mafunzo ya Ualimu.

3. Ada ya mafunzo Stashahada ya Juu ni 600,000/= kwa mwaka (Muhula wa kwanza 300,000/= na muhula wa pili 300,000/=)

4. Wanafunzi watakaosajiliwa Chuoni ni wale waliopo kwenye orodha hii tu na SIYO vinginevyo, waweza pata orodha hyo kwa kufungua kiunganishi kimoja wapo hapo chini.

Stashahada_ya_juu_elimu_maalum.pdf

Stashahada_ya_juu_lugha.pdf

Stashahada_ya_juu_sayansi_na_hisabati.pdf


Stashahada_ya_kawaida_elimu_ya_awali.pdf


Stashahada_ya_kawaida_elimu_ya_michezo.pdf

Stashahada_ya_kawaida_elimu_ya_msingi.pdf
 

Attachments

  • stashahada_ya_juu_elimu_maalum.pdf
    390.7 KB · Views: 364
  • stashahada_ya_juu_lugha.pdf
    254.1 KB · Views: 213
  • stashahada_ya_juu_sayansi_na_hisabati.pdf
    531.7 KB · Views: 490
  • Stashahada_ya_kawaida_elimu_ya_awali.pdf
    4.9 MB · Views: 1,088
  • stashahada_ya_kawaida_elimu_ya_michezo.pdf
    341.6 KB · Views: 305
  • stashahada_ya_kawaida_elimu_ya_msingi.pdf
    830.9 KB · Views: 756
NB. Majina yaliotoka ni wale wenye ufaulu kuanzia division 3
 
INYASI ROMAN ngazi cheti

sijaona bt title yao inasema waliochaguliwa kujiunga na STASHAHADA ya kawaida elimu ya msingi (miaka miwili). sasa sielewi ngazi ya cheti si inaitwa ASTASHAHADA? Lakini apa sion majina ya ASTASHAHADA
 
cheti kk.

sijaona bt title yao inasema waliochaguliwa
kujiunga na STASHAHADA ya kawaida elimu ya
msingi (miaka miwili). sasa sielewi ngazi ya cheti
si inaitwa ASTASHAHADA? Lakini apa sion majina
ya ASTASHAHADA
 
sijaona bt title yao inasema waliochaguliwa kujiunga na STASHAHADA ya kawaida elimu ya msingi (miaka miwili). sasa sielewi ngazi ya cheti si inaitwa ASTASHAHADA? Lakini apa sion majina ya ASTASHAHADA

niangalizie elimu ya kawaida miaka 2 au namba hi s1880/0193
 
Back
Top Bottom