Waliochaguliwa kuandaa mpango wa maendeleo 2050 wote wanaishi Mbezi Beach au Masaki, wanalishwa kwa kodi za umma miaka yote, wana umri zaidi ya 50 yrs

Kuna mtu juzi kaniambia, huenda 2050,Mikoa iliyo vizuri kiuchumi ikarudi nyuma kama Singida. Nilimwuliza ni kwa nini, akanjibu anayepanga [ Waziri wa Mipango] anatoka Singida. Na anayetoa fedhs za Mipango hiyo[ Waziri wa Fedha] naye anatoka Singida. Tena wote ni Wanyira. Niliishia kucheka.
 
Mhe. Waziri Kitila Mkumbo ametoa majina ya watu alioteua kutengeneza mpango wa 2050. Wote walioteuliwa wana miaka 50 kwenda mbele, ni wake au watoto wa viongozi wa CCM, ni wanazuoni waliofundisha na kusoma naye chuo...........hizi siyo zama za giza ni zama za technology. Hakuna namna hawa wazee wanaweza kuweka projection za nchi kuendana na technology badala yake watakwenda kutuletea nadharia kwenye vitabu

Tulitegemea kuona wafanyabiashara, wataalam wa TEHAMa na watu wenye mafanikio kwenye jamii wakiwa Sehemu ya timu . Academia wangebaki kwenye technical team ya waandishi siyo wachakata hoja.

Tunaanza kufeli kupanga kama Ishara ya kufeli kufanikiwa...........nchi haiwezi ikapangiwa kila kitu na wakaazi wa mbezi beach inahitaji watu wa namtumbo, Kaperamsenga na Kipandaule washiriki pia.

Hawa watu wa masaki na Mbezi Beach wanawekwa kwenye mipango ya nchi ndio wanaotengeneza propaganda za utajiri kwenye umaskini. Mtu kazaliwa hadi anazeeka yupo analishwa na serikali kwa kodi za wananchi anawezaje kujua matatizo ya wananchi? Ndio hawa badala ya kuripoti uhalisia wao wanaripoti uongo na uzandiki walioandika kwenye vitabu vyao.
I second this ...😐
 
Mbona jana nilisikia watu wanaweza kutoa maoni yao hata kwa simu?imekuwaje tena?
 
Kwa "unazi wa CCM" ndio maana hatukuwahi kutekeleza hata mpango mmoja kwa 30% kwa miaka yote 62 ya uhuru (tangu ccm iwe madarakani)
Ni ngumu kutekelezeka kwa sababu zifuatazo:
1. Wanaotengeneza hii dira nao hawana dira kamili (hawajui Taifa linataka lini)
2 Wengi hawana exposure na huteuliwa kwa kujuana zaidi na porojo juu!
3. Kutoshirikisha makundi mengine ie wafanyabiashara, wakulima na fani nyingine.
 
Mhe. Waziri Kitila Mkumbo ametoa majina ya watu alioteua kutengeneza mpango wa 2050. Wote walioteuliwa wana miaka 50 kwenda mbele, ni wake au watoto wa viongozi wa CCM, ni wanazuoni waliofundisha na kusoma naye chuo...........hizi siyo zama za giza ni zama za technology. Hakuna namna hawa wazee wanaweza kuweka projection za nchi kuendana na technology badala yake watakwenda kutuletea nadharia kwenye vitabu

Tulitegemea kuona wafanyabiashara, wataalam wa TEHAMa na watu wenye mafanikio kwenye jamii wakiwa Sehemu ya timu . Academia wangebaki kwenye technical team ya waandishi siyo wachakata hoja.

Tunaanza kufeli kupanga kama Ishara ya kufeli kufanikiwa...........nchi haiwezi ikapangiwa kila kitu na wakaazi wa mbezi beach inahitaji watu wa namtumbo, Kaperamsenga na Kipandaule washiriki pia.

Hawa watu wa masaki na Mbezi Beach wanawekwa kwenye mipango ya nchi ndio wanaotengeneza propaganda za utajiri kwenye umaskini. Mtu kazaliwa hadi anazeeka yupo analishwa na serikali kwa kodi za wananchi anawezaje kujua matatizo ya wananchi? Ndio hawa badala ya kuripoti uhalisia wao wanaripoti uongo na uzandiki walioandika kwenye vitabu vyao.
Duh! Hakuna hata moja lenye ukweli. Twende hatua kwa hatua na hoja kwa hoja:
  1. Hoja: Wote walioteuliwa wana miaka 50 kwenda meble. Ukweli: Mgawanyo wa umri wa timu ni kama ifuatavyo: 80, 72, 67, 63, 62, 58, 56, 55, 54, 53, 50, 48, 47, 47, 46, 46, 42, 40, 34, 34, 29. Kati ya wajumbe 21, wenye umri wa miaka 50 na/au zaidi ni 11. Kwa hii hoja haina ukweli. Kwa neno moja ni UWONGO!
  2. Hoja: Wote ni wake au watoto wa viongozi wa CCM: Ukweli: Ninaambatisha orodha ya wajumbe ili wasomaji wachambue wenyewe ili kubiani wangapi ni wake au watoto wa viongozi wa CCM. Kimsingi hakuna hata moja katika kundi hili. Huo nao ni UWONGO.
  3. Hoja: wajumbe wa Timu ni wanazuoni waliofundisha na kusoma naye chuo.. Ukweli: Mie nimesoma na kufundisha Chuo Kikuu cha DSM (UDSM). Katika wajumbe 21, walimu au waliowahi kuwa walimu wa UDSM ni saba (7), ambao ni Prof. Msambichaka, Prof. Semboja, Dr Asha Rose Migiro, Dr Richard Kimwaga, Dr Richard Shukia, Dr Amina Msengwa, na Dr Gladness Salema. Kwa hiyo huu nao ni UWONGO.
  4. Hoja: Tulitegemea kuona wafanyabiashara, wataalam wa TEHAMA na watu wenye mafanikio kwenye jamii wakiwa sehemu ya timu: Jibu: Sema ulitegemea, badala ya tulitegemea. Sasa sio kila kitu unachokitegemea kaika maista hutokea kama kilivyo. Vigezo vyako sio lazima viwe vigezo vyetu. Ni maoni yako na tunayaheshimu lakini tunayakataa. Aidha, wafanyabishara katika timu wapo. Wajuzi wa TEHAMA wapo tele-actually angalau wajumbe wawili ni wabobezi katika kutengeneza mifumo ya TEHAMA. Kwamba walioteuliwa hawana mafanikio katika jamii ni maoni yako lakini sikubaliani nayo kwa kuwa hata sijui unatumia vigezo gani kupima mafanikio ya mtu katika jamii!
  5. Hoja: Kwamba wote wanakaa Masaki na Mbezi Beach. Jibu: Mosi, kukaa Masaki na Mbezi Beach sio dhambi na hakukufanyi kuwa mtanzania nusu au robo. Pili, sio kweli kwamba wajumbe wa timu wote wanakaa Masaki na Mbezi Beach. Kwa mfano, Dr Neema Mduma anakara Arusha. Dr Yahaya Hamad Sheikh na Dr Maryam Vuai wanakaa Zanzibar. Ms Emmy Kalomba, Dr Ntuli Kapologwe, wanakaa Dodoma. Dr Turuka anakaa Morogoro. Dr Richard Shukia anakaa Kijitonyama. Dr Richard Kamwaga anakaa Msewe. Huu nao ni UWONGO.

HITIMISHO: wewe ni MWONGO sana.
 
Attachments

  • BRIEF PROFILES OF MEMBERS OF NVCTT.pdf
    434.9 KB · Views: 3

Kupeana ULAJI ndio kawaida yao, kupewa vyeo kwenye bodi, sijuwi ni Nini na nini..
Kifupi viongozi wetu HAWAJALI RAIA. Wanajali matumbo yao na KULINDANA..
TUTAOKOLEWA NA NANI SISI WADANGANYIKA?!☹️😞😟😢😥😦😭
 
Unastahili kujibiwa. Twende hoja kwa hoja:
  1. Kwamba wajumbe wate wa Timu wana miaka 50 kwenda mbele. Mgawanyo wa umri wa wajumbe ni kama ifuatavyo: 80, 72, 67, 63, 62, 58, 56, 55, 54, 53, 50,48,47, 47, 46, 46, 42, 40, 34,34,29. Mpaka hapo utaona kuwa wenye umri wa miaka 50 ni 11. Kwa hiyo kwamba wajumbe wote ni wana miaka 50 na kwenda mbele ni UWONGO. Muhimu zaidi, tuache ubaguzi wa umri. Tusimnyime mtu nafasi ya kutoa mchango wake kwa sababu ni mzee. Uzee sio dhambi, wala sio ugonjwa. Tumeteua timu ya wataalam, sio wawakilishi wetu katika michezo ya masumbwi!
  2. Kwamba wajumbe wote wa timu ni wake au watoto wa viongozi wa CCM. Hii nayo sio kweli. Hata kama ingetokea yupo mke au kiongozi wa CCM mwenye kukidhi vigezo tulivyoweka tusingeacha kumteua kwa sababu ni mke au mtoto wa kiongozi wa CCM. Kuwa mke au mtoto wa kiongozi wa CCM au chama kingine chochote hakukuondolei sifa ya kutumikia taifa hili wala hakukufanyi uwe mtanzania nusu au robo.
  3. Kwamba wajumbe wote wa timu ni wanazuoni waliofundisha nami. Mie nimesoma na kufundishia Chuo Kikuu cha DSM (UDSM). Walimu au waliowahi kuwa walimu katika UDSM ni saba (7), ambao ni Prof. Msambichaka, Prof Semboja, Dr Asha Rose Migiro, Dr Richard Kimwaga, Dr Richard Shukia, Dr Amina Msengwa, na Dr Gladness Salema. Kwamba wote wametoka UDSM ni UWONGO. Wapo pia wanataaluma kutoka UDOM, SUA, NM-AIST, etc. Nirudie tena ubini wako (demographic variable) wowote ule hauwezi kukuondolea sifa ya kutumikia. Nisingeacha kumteua mtu kwa kuwa tu amesoma au kufundisha chuo ambacho mie nilifundisha. Kwa ukongwe wake hapa nchini UDSM bado ina wataalam wengi na haikwepeki linapokuja shughuli na kazi zinazohitaji utaaluma na utalaam.
  4. Kwamba ‘tulitegemea’ kuona wafanyabiashara, wataalam wa TEHAMA na watu wenye mafanikio katika jamii wakiwa sehemu ya timu. Kwanza sema ‘ulitegemea’ badala ya ‘tulitegemea’. Pili, sio kila unachotegemea hapa duniani unakipata. Bahati mbaya vigezo vyako havikuwa vigezo vyetu. Pole kwa mategemeo yako kutokukidhiwa. Hata hivyo, kutokukidhiwa kwa mategemeo yako haifanyi timu isiwe na sifa. Tatu, katika timu wabobezi wa TEHAMA wapo na wafanyabiashara wapo. Kwamba hawana mafanikio katika jamii ni maoni yako ambayo ninayaheshimu lakini ninayakataa!
  5. Kwamba wajumbe wa Timu wanakaa Masaki na Mbezi Beach. Mosi, kukaa Masaki au Mbezi Beach sio dhambi wala kosa na hakumuondolei mtu sifa. Pili, sio kweli wajumbe wote hao wanakaa maeneo hayo. Wajumbe wametoka katika maeneo mbalimbali nchini, Tanzania Bara na Zanzibar.
  6. HITIMISHO: umesema uwongo. Hivyo wewe ndugu ni MWONGO.
 
Asante kwa kujitokeza , kuna kijiswali kidogo cha nyongeza , kwenye hoja namba 2 , Pamoja na kwamba si dhambi , lakini ni kweli kwamba waliochaguliwa wote ni familia za wanaccm , kwa maana ya watoto , wake ama wanaccm wenyewe kama ulivyo wewe ? na unadhani ni kwanini kwenye jambo la kitaifa kama hili umeweka wanaccm tupu ? na Je hii dira ya nchi ni kwa ccm tu au na wengine wanahusika ?

Asante kwa kunisikiliza .
 
Unastahili kujibiwa. Twende hoja kwa hoja:
  1. Kwamba wajumbe wate wa Timu wana miaka 50 kwenda mbele. Mgawanyo wa umri wa wajumbe ni kama ifuatavyo: 80, 72, 67, 63, 62, 58, 56, 55, 54, 53, 50,48,47, 47, 46, 46, 42, 40, 34,34,29. Mpaka hapo utaona kuwa wenye umri wa miaka 50 ni 11. Kwa hiyo kwamba wajumbe wote ni wana miaka 50 na kwenda mbele ni UWONGO. Muhimu zaidi, tuache ubaguzi wa umri. Tusimnyime mtu nafasi ya kutoa mchango wake kwa sababu ni mzee. Uzee sio dhambi, wala sio ugonjwa. Tumeteua timu ya wataalam, sio wawakilishi wetu katika michezo ya masumbwi!
  2. Kwamba wajumbe wote wa timu ni wake au watoto wa viongozi wa CCM. Hii nayo sio kweli. Hata kama ingetokea yupo mke au kiongozi wa CCM mwenye kukidhi vigezo tulivyoweka tusingeacha kumteua kwa sababu ni mke au mtoto wa kiongozi wa CCM. Kuwa mke au mtoto wa kiongozi wa CCM au chama kingine chochote hakukuondolei sifa ya kutumikia taifa hili wala hakukufanyi uwe mtanzania nusu au robo.
  3. Kwamba wajumbe wote wa timu ni wanazuoni waliofundisha nami. Mie nimesoma na kufundishia Chuo Kikuu cha DSM (UDSM). Walimu au waliowahi kuwa walimu katika UDSM ni saba (7), ambao ni Prof. Msambichaka, Prof Semboja, Dr Asha Rose Migiro, Dr Richard Kimwaga, Dr Richard Shukia, Dr Amina Msengwa, na Dr Gladness Salema. Kwamba wote wametoka UDSM ni UWONGO. Wapo pia wanataaluma kutoka UDOM, SUA, NM-AIST, etc. Nirudie tena ubini wako (demographic variable) wowote ule hauwezi kukuondolea sifa ya kutumikia. Nisingeacha kumteua mtu kwa kuwa tu amesoma au kufundisha chuo ambacho mie nilifundisha. Kwa ukongwe wake hapa nchini UDSM bado ina wataalam wengi na haikwepeki linapokuja shughuli na kazi zinazohitaji utaaluma na utalaam.
  4. Kwamba ‘tulitegemea’ kuona wafanyabiashara, wataalam wa TEHAMA na watu wenye mafanikio katika jamii wakiwa sehemu ya timu. Kwanza sema ‘ulitegemea’ badala ya ‘tulitegemea’. Pili, sio kila unachotegemea hapa duniani unakipata. Bahati mbaya vigezo vyako havikuwa vigezo vyetu. Pole kwa mategemeo yako kutokukidhiwa. Hata hivyo, kutokukidhiwa kwa mategemeo yako haifanyi timu isiwe na sifa. Tatu, katika timu wabobezi wa TEHAMA wapo na wafanyabiashara wapo. Kwamba hawana mafanikio katika jamii ni maoni yako ambayo ninayaheshimu lakini ninayakataa!
  5. Kwamba wajumbe wa Timu wanakaa Masaki na Mbezi Beach. Mosi, kukaa Masaki au Mbezi Beach sio dhambi wala kosa na hakumuondolei mtu sifa. Pili, sio kweli wajumbe wote hao wanakaa maeneo hayo. Wajumbe wametoka katika maeneo mbalimbali nchini, Tanzania Bara na Zanzibar.
  6. HITIMISHO: umesema uwongo. Hivyo wewe ndugu ni MWONGO.
Profesa asante kwa ufafanuzi, wakati napitia neno kwa neno uliyoandika, na wewe tukuambie ukweli huu..kuwa Profesa au Dkt. katika jambo fulani si kwamba unajua vyote vinavyokuja mbele yako, pili, kipimo kizuri cha mafanikio ya jambo lolote vema kiambatane na matendo, hao walimu wenzako na makatibu wakuu wastaafu wana mafanikio gani nje ya utumishi wao serikalini ambayo wanaonekana mfano kwa jamii, nikupe mfano Profesa Shivji nje ya ajira yake na utumishi serikalini ni Mwandishi wa vitabu na makala, mshiriki kwenye midahalo na kazi nyingine za jamii tena kwa kujitolea nk..mfano mwingine Mzee Uttoh baada ya ajira serikalini anasimamia Taasisi ya WAJIBU kuleta majibu ya changamoto kwenye maeneo ya utawala bora, uwajibikaji nk hao mliowachukua nini kimewafanya muwachague kwa kazi hii..vyeti vyao au uzoefu? Nini hasa..mfano uko na watoto 2 nyumbani wote wana umri wa kuanza shule, mmoja kila ukirudi unamkuta anacheza mpira, yule mwingine unamkuta anachora na kuandika herufi kwa kuigiza chini, kwa muono wako yupi anafaa kuanza shule mapema suppose umepewa nafasi moja na mwenye shule?
Kuna hitilafu kubwa kwenye selection yenu, haraka unaweza kuona kupeana ulaji, upendeleo, ubinafsi na kulindana..niishie hapa kwanza.
 
Duh! Hakuna hata moja lenye ukweli. Twende hatua kwa hatua na hoja kwa hoja:
  1. Hoja: Wote walioteuliwa wana miaka 50 kwenda meble. Ukweli: Mgawanyo wa umri wa timu ni kama ifuatavyo: 80, 72, 67, 63, 62, 58, 56, 55, 54, 53, 50, 48, 47, 47, 46, 46, 42, 40, 34, 34, 29. Kati ya wajumbe 21, wenye umri wa miaka 50 na/au zaidi ni 11. Kwa hii hoja haina ukweli. Kwa neno moja ni UWONGO!
  2. Hoja: Wote ni wake au watoto wa viongozi wa CCM: Ukweli: Ninaambatisha orodha ya wajumbe ili wasomaji wachambue wenyewe ili kubiani wangapi ni wake au watoto wa viongozi wa CCM. Kimsingi hakuna hata moja katika kundi hili. Huo nao ni UWONGO.
  3. Hoja: wajumbe wa Timu ni wanazuoni waliofundisha na kusoma naye chuo.. Ukweli: Mie nimesoma na kufundisha Chuo Kikuu cha DSM (UDSM). Katika wajumbe 21, walimu au waliowahi kuwa walimu wa UDSM ni saba (7), ambao ni Prof. Msambichaka, Prof. Semboja, Dr Asha Rose Migiro, Dr Richard Kimwaga, Dr Richard Shukia, Dr Amina Msengwa, na Dr Gladness Salema. Kwa hiyo huu nao ni UWONGO.
  4. Hoja: Tulitegemea kuona wafanyabiashara, wataalam wa TEHAMA na watu wenye mafanikio kwenye jamii wakiwa sehemu ya timu: Jibu: Sema ulitegemea, badala ya tulitegemea. Sasa sio kila kitu unachokitegemea kaika maista hutokea kama kilivyo. Vigezo vyako sio lazima viwe vigezo vyetu. Ni maoni yako na tunayaheshimu lakini tunayakataa. Aidha, wafanyabishara katika timu wapo. Wajuzi wa TEHAMA wapo tele-actually angalau wajumbe wawili ni wabobezi katika kutengeneza mifumo ya TEHAMA. Kwamba walioteuliwa hawana mafanikio katika jamii ni maoni yako lakini sikubaliani nayo kwa kuwa hata sijui unatumia vigezo gani kupima mafanikio ya mtu katika jamii!
  5. Hoja: Kwamba wote wanakaa Masaki na Mbezi Beach. Jibu: Mosi, kukaa Masaki na Mbezi Beach sio dhambi na hakukufanyi kuwa mtanzania nusu au robo. Pili, sio kweli kwamba wajumbe wa timu wote wanakaa Masaki na Mbezi Beach. Kwa mfano, Dr Neema Mduma anakara Arusha. Dr Yahaya Hamad Sheikh na Dr Maryam Vuai wanakaa Zanzibar. Ms Emmy Kalomba, Dr Ntuli Kapologwe, wanakaa Dodoma. Dr Turuka anakaa Morogoro. Dr Richard Shukia anakaa Kijitonyama. Dr Richard Kamwaga anakaa Msewe. Huu nao ni UWONGO.

HITIMISHO: wewe ni MWONGO sana.
Pamoja na ufafanuzi huo nina maswali;Kuna scheme nyingi zimepita lakini zimefeli japo nazo tuliambiwa zimeandaliwa na wataalam mahiri,mosi je Mmechukua hatua gani kuhakikisha scheme hii inaenda kufanikiwa?Pili kwanini scheme zilizopita hazikufanikiwa?tatu Sababu zipi zilipelekea scheme zilizopita kutofanikiwa?
 
Unastahili kujibiwa. Twende hoja kwa hoja:
  1. Kwamba wajumbe wate wa Timu wana miaka 50 kwenda mbele. Mgawanyo wa umri wa wajumbe ni kama ifuatavyo: 80, 72, 67, 63, 62, 58, 56, 55, 54, 53, 50,48,47, 47, 46, 46, 42, 40, 34,34,29. Mpaka hapo utaona kuwa wenye umri wa miaka 50 ni 11. Kwa hiyo kwamba wajumbe wote ni wana miaka 50 na kwenda mbele ni UWONGO. Muhimu zaidi, tuache ubaguzi wa umri. Tusimnyime mtu nafasi ya kutoa mchango wake kwa sababu ni mzee. Uzee sio dhambi, wala sio ugonjwa. Tumeteua timu ya wataalam, sio wawakilishi wetu katika michezo ya masumbwi!
  2. Kwamba wajumbe wote wa timu ni wake au watoto wa viongozi wa CCM. Hii nayo sio kweli. Hata kama ingetokea yupo mke au kiongozi wa CCM mwenye kukidhi vigezo tulivyoweka tusingeacha kumteua kwa sababu ni mke au mtoto wa kiongozi wa CCM. Kuwa mke au mtoto wa kiongozi wa CCM au chama kingine chochote hakukuondolei sifa ya kutumikia taifa hili wala hakukufanyi uwe mtanzania nusu au robo.
  3. Kwamba wajumbe wote wa timu ni wanazuoni waliofundisha nami. Mie nimesoma na kufundishia Chuo Kikuu cha DSM (UDSM). Walimu au waliowahi kuwa walimu katika UDSM ni saba (7), ambao ni Prof. Msambichaka, Prof Semboja, Dr Asha Rose Migiro, Dr Richard Kimwaga, Dr Richard Shukia, Dr Amina Msengwa, na Dr Gladness Salema. Kwamba wote wametoka UDSM ni UWONGO. Wapo pia wanataaluma kutoka UDOM, SUA, NM-AIST, etc. Nirudie tena ubini wako (demographic variable) wowote ule hauwezi kukuondolea sifa ya kutumikia. Nisingeacha kumteua mtu kwa kuwa tu amesoma au kufundisha chuo ambacho mie nilifundisha. Kwa ukongwe wake hapa nchini UDSM bado ina wataalam wengi na haikwepeki linapokuja shughuli na kazi zinazohitaji utaaluma na utalaam.
  4. Kwamba ‘tulitegemea’ kuona wafanyabiashara, wataalam wa TEHAMA na watu wenye mafanikio katika jamii wakiwa sehemu ya timu. Kwanza sema ‘ulitegemea’ badala ya ‘tulitegemea’. Pili, sio kila unachotegemea hapa duniani unakipata. Bahati mbaya vigezo vyako havikuwa vigezo vyetu. Pole kwa mategemeo yako kutokukidhiwa. Hata hivyo, kutokukidhiwa kwa mategemeo yako haifanyi timu isiwe na sifa. Tatu, katika timu wabobezi wa TEHAMA wapo na wafanyabiashara wapo. Kwamba hawana mafanikio katika jamii ni maoni yako ambayo ninayaheshimu lakini ninayakataa!
  5. Kwamba wajumbe wa Timu wanakaa Masaki na Mbezi Beach. Mosi, kukaa Masaki au Mbezi Beach sio dhambi wala kosa na hakumuondolei mtu sifa. Pili, sio kweli wajumbe wote hao wanakaa maeneo hayo. Wajumbe wametoka katika maeneo mbalimbali nchini, Tanzania Bara na Zanzibar.
  6. HITIMISHO: umesema uwongo. Hivyo wewe ndugu ni MWONGO.
Profesa Kitila, niruhusu nikuambie yafuatayo:
1. Kama na wewe umeamua kuungana na kundi la kutetea tumbo badala ya ustawi wa nchi, elimu yako uliyoipata kwa taabu na kujitolea sana kwa msaada mkubwa wa Mwenyezi Mungu itakuwa ni usaliti mkubwa kwa aliyekupa fursa ya kuelimika ili utende vile inatakiwa..usitetee mambo yanayofanyika huku yakiwa na kasoro za wazi, process zinazotumika kuteua watu kwa jukumu fulani HAZIFAI zina upendeleo, ghiliba na hila na hivyo hazina jema lolote kwa nchi.
2. Naomba uelewe CCM ya sasa haina uwezo na hata tu utashi wa kutenda kwa wema kwa masilahi ya nchi, kubwa linalowaunganisha ni KULA na kushibisha matumbo yao, vile ulivyo wewe toka ujana wako ni vigumu kubeba kasoro hii, vinginevyo hutakaa kwa amani muda wote utakaokuwa huko..
3. Wasaidie hao waliokupa hizo nafasi kujua zama hizi si za kuteua watu pasina na kuhoji uwezo na utayari wake kufanya jukumu mnalotaka kumpa, haya mawili ndio yanaamua matokeo ya jukumu mnalompa mtu, anaweza kuwa tayari kufanya lakini hana uwezo, au anaweza kuwa na uwezo lakini hana utayari..akiulizwa kabla ya kumteua msimamo wake utaonekana kati ya haya mawili, waambie waache hiyo animal strategy kuteua wale tu wanaoshabihiana nao, au wale wanaoona si wadadisi wenye msimamo huru usioruhusu kuingiliwa pasina na hoja!
4. Rekebisheni muundo wa hii timu mmeteua, kama kweli mna lengo la kupata dira nzuri ya 2050, mtu asiyeandika hata makala tu gazetini au pahala popote juu ya jambo lolote analolifahamu wakati ni msomi wa level ya kama Profesa Semboja, hana pia muda wa kusoma na hivyo anawezaje kuwa na kitu bora kichwani kama hasomi mawazo ya wengine..ninafahamu wewe umejiwekea utartibu wa kusoma vitabu vingi ndani ya mwaka, hii ndio njia pekee kurutubisha uwezo kifikra na kimtazamo! Asante
 
Mambo ya "wale samaki waliokufa,,vifo vilisababishwa na wingi wa kinyesi cha Mifugo katika maji ya mto ----!!"
 
Kuna mambo mengi yanotokea duniani kwa sasa khasa vita vya kijiografia, ukuaji Artificial Intelligence, kuibuka kwa silaha mpya, mabadiliko ya sayansi na teknolojia, mabadiliko ya tabia nchi, viashiria hatarishi vya hali ya usalama duniani, usalama wa chakula (food security), usalama na afya za wananchi, kuangalia sera ya elimu Kama yakidhi hali ya sasa ya kidunia na mambo mengine lukuki.
HAKIKA

'Usalama wa Chakula' ni jambo ufunguo kwa msingi thabiti wa maendeleo ya watu na vitu.

'Usalama wa Jamii' ni suala mtambuka.

Akili Bandia inaweza kusaidia katika mapinduzi ya kweli ya maisha ya watu duniani -- na tutaenda kutoboa kupitia ujuzi na ufundi wa kuratibu maendeleo kupitia mapinduzi ya nyenzo hii -- Ni 'mpango wa kando' kwa hata wataalam hawa walioteuliwa kwa dhamira hii ya kusanifu dira ya maendeleo.

Sasa suala la 'Akili Bandia' na 'Usalama wa Jamii' lina 'mafundi wake'; hawawezi kuwa watu wa kutokea kwenye akademia pekee yake ama wazoefu wa tawala na mipango; japo humo wanaweza kuwepo wawili watatu wenye kufanania na ujuzi wa haya kutoka kwenye hizo kada -- kada za akademia ama nchi-dola.

Haya ni mambo ya Elimu 2.0 na Elimu 3.0; lau kwenye nchi nyingi sehemu ya haya yanahodhiwa na 'kanisa' ama/na 'washirika wa himaya'.

Kuna mengi yanakwenda yanafanania kutokea, na 'yanayozuiwa kutokea' na hali yako 'nje ya uwezo wa wasomi mashudu' -- lau si matusi; ila ni ukweli mchungu unaohitaji baadhi ya wadau 'wawe wapole' ili wapatie maoteo sahihi ya watu na maendeleo duniani.

Kuna mawezekano ya 'magomvi ya michongo', 'vita kuu ya dunia', 'Maradhi ya kutengeneza kama yale yaliyoshindwa; na tena hapa Tanzania tulikuwa sehemu ya 'ushindi'; 'Uongo wa Kiufundi sana wa Siasa za Mabadiliko ya Tabia Nchi' na mengine mengi.

Sehemu ya haya ndiyo yamesabisha na yanaendelea kusababisha hata dira ya taifa inayokatikia kuwa 'ndoto nusu nusu' ya 'Watanzania'.

Kuna mambo mawili matatu yanaweza kuzungumzwa kwa kutangulia -- hata kama yatashangaza: Sura ya nchi na tawala inayonasibu ya kubadilika sana ikiwa dira yoyote inayokwenda kutengenezwa itapatia 'ukweli wa mambo' -- kufika 2050.

- Namna ya leo ya siasa za uwakilishi, inakwenda kubadilika sana kutokana na maendeleo ya matumizi ya Akili Bandia.

- Mifumo ya watu na serikali inakwenda kubadilika sana

- Mambo ya 'watawala wanaoabudiwa' labda kwa upambe na uchawa yanakwenda kuthibitisha 'mkosi kamili wa kimifumo', kokote kule hapa duniani -- japo hili linataka sana umma 'ujitambue' kabla kujifunza kupitia na migogoro mikubwa ya kijamii, siasa na maendeleo hapa duniani.

Kuna mambo yamefika ukomo wa matumizi yake lakini kikundi/vikundi vya 'watawala wa dunia' wana vuta nikuvute ya wao kwa wao -- hili ndilo linalochochea uwezekano wa 'vita ya dunia' ili 'kumwaga ugali'; hili tayari linaendelea...

Hili tukilifahamu vizuri tunaweza 'kujipanga' kulingana na ile mithali ya 'Mafahali Wawili Wapambanapo'...

Uchumi wa kifedha, mikopo na masoko globali umefika 'mwisho'; tunahitaji kubuni namna mpya ya uchumi unaweza kuwa himilifu na wakujitegemea kiukweli; labda itashangaza kulisema hili : 'ujamaa na kujitegemea' ilikuwa ni mapelekeo ya maendeleo ya watu na nchi, ambavyo kwa sehemu, 'mafundi wa uono' na 'washirika' walikuwa wakishawishi mawezekano ya 'njia ya tatu'...

SASA, dhamira iliyopelekea ushawishi wa dhamira ya kuanzishwa kwa Chama cha Mapinduzi ndiyo inaufunguo; ikiwa wanamipango wanataka 'kupatia' majukumu yao, ni vema wakatumia 'fremukazi ya uono na ufikirifu mifumo'...

Chama cha Mapinduzi ni 'mtoto' wa 'watu washirika' waliokuwa na 'maono' ya kiroho, maadili na miiko... Haya yote 'yamesahaulika'; lakini ili tutoboe kiza kinachofanania kutukumba, tunalazimika 'kujisahihisha sasa' ama 'hapo mbele'. Tukianza mapema basi tunapunguza mawezekano ya kero na mateso -- kero na mateso ya kujichanganya na kudanganyana...

Hapa Tanzania, 2023, bado hatuna 'Chama Mbadala' hasa; hatima ya nchi bado iko mikononi mwa 'washirika'...

Ufunguo wa 'kumalizana na siasa za nchi', kutengeneza serikali ya watu huru kweli inayonafasi kupitia wadau wa Chama cha Mapinduzi wenye upeo, uwezo na ufundi wa kurejea katika misingi--HILI LINAWEZEKANA; linahitaji tu wadau kujiongeza kwa Elimu 2.0 na Elimu 3.0....
 
Unastahili kujibiwa. Twende hoja kwa hoja:
  1. Kwamba wajumbe wate wa Timu wana miaka 50 kwenda mbele. Mgawanyo wa umri wa wajumbe ni kama ifuatavyo: 80, 72, 67, 63, 62, 58, 56, 55, 54, 53, 50,48,47, 47, 46, 46, 42, 40, 34,34,29. Mpaka hapo utaona kuwa wenye umri wa miaka 50 ni 11. Kwa hiyo kwamba wajumbe wote ni wana miaka 50 na kwenda mbele ni UWONGO. Muhimu zaidi, tuache ubaguzi wa umri. Tusimnyime mtu nafasi ya kutoa mchango wake kwa sababu ni mzee. Uzee sio dhambi, wala sio ugonjwa. Tumeteua timu ya wataalam, sio wawakilishi wetu katika michezo ya masumbwi!
  2. Kwamba wajumbe wote wa timu ni wake au watoto wa viongozi wa CCM. Hii nayo sio kweli. Hata kama ingetokea yupo mke au kiongozi wa CCM mwenye kukidhi vigezo tulivyoweka tusingeacha kumteua kwa sababu ni mke au mtoto wa kiongozi wa CCM. Kuwa mke au mtoto wa kiongozi wa CCM au chama kingine chochote hakukuondolei sifa ya kutumikia taifa hili wala hakukufanyi uwe mtanzania nusu au robo.
  3. Kwamba wajumbe wote wa timu ni wanazuoni waliofundisha nami. Mie nimesoma na kufundishia Chuo Kikuu cha DSM (UDSM). Walimu au waliowahi kuwa walimu katika UDSM ni saba (7), ambao ni Prof. Msambichaka, Prof Semboja, Dr Asha Rose Migiro, Dr Richard Kimwaga, Dr Richard Shukia, Dr Amina Msengwa, na Dr Gladness Salema. Kwamba wote wametoka UDSM ni UWONGO. Wapo pia wanataaluma kutoka UDOM, SUA, NM-AIST, etc. Nirudie tena ubini wako (demographic variable) wowote ule hauwezi kukuondolea sifa ya kutumikia. Nisingeacha kumteua mtu kwa kuwa tu amesoma au kufundisha chuo ambacho mie nilifundisha. Kwa ukongwe wake hapa nchini UDSM bado ina wataalam wengi na haikwepeki linapokuja shughuli na kazi zinazohitaji utaaluma na utalaam.
  4. Kwamba ‘tulitegemea’ kuona wafanyabiashara, wataalam wa TEHAMA na watu wenye mafanikio katika jamii wakiwa sehemu ya timu. Kwanza sema ‘ulitegemea’ badala ya ‘tulitegemea’. Pili, sio kila unachotegemea hapa duniani unakipata. Bahati mbaya vigezo vyako havikuwa vigezo vyetu. Pole kwa mategemeo yako kutokukidhiwa. Hata hivyo, kutokukidhiwa kwa mategemeo yako haifanyi timu isiwe na sifa. Tatu, katika timu wabobezi wa TEHAMA wapo na wafanyabiashara wapo. Kwamba hawana mafanikio katika jamii ni maoni yako ambayo ninayaheshimu lakini ninayakataa!
  5. Kwamba wajumbe wa Timu wanakaa Masaki na Mbezi Beach. Mosi, kukaa Masaki au Mbezi Beach sio dhambi wala kosa na hakumuondolei mtu sifa. Pili, sio kweli wajumbe wote hao wanakaa maeneo hayo. Wajumbe wametoka katika maeneo mbalimbali nchini, Tanzania Bara na Zanzibar.
  6. HITIMISHO: umesema uwongo. Hivyo wewe ndugu ni MWONGO.
Kuna document yoyote majina inayoonesha washiriki wote.

Ingependeza ingewekwa wazi kwa ajili ya uwekaji kumbukumbu sawa.
 
Back
Top Bottom