Walioanza na Kikwete wataondoka naye mwakani

ligera

JF-Expert Member
May 17, 2014
2,646
1,167
Hii ni falsafa inayoonekana kumea kila siku miongoni mwa vijana wa kitanzania.

Falsafa kama hiyo ndiyo iliyo wagharimu wabunge wengi mwaka 2005 ,wakati mkapa anaondoka madarakani aliondoka na wabunge wengi walioingia mwaka 1995 wakati mkapa anaingia.

Baadhi ya wabunge walioondoka na mkapa k.v gama, dr. thadeus luoga, pr.mbilinyi, nk.

Mwaka 2005 ndipo watu waliposhuhudia sura mpya nyingi zikiingia bungeni.

Tutegemee mwaka 2015 sura mpya nyingi kuingia bungeni hasa kutokana na kuongezeka kwa uelewa miongoni mwa wananchi kwamba kila mtu anaouwezo wa kuwa mbunge, mbunge hachangii chochote katika kuendesha maisha binafsi ya mtu na bidii yako ndiyo itakayo kuwezesha kupata mkate wa siku, na wengine wanaamini kwamba maisha yanaweza kwenda tu bila hata mbunge , kwani wabunge wengi ni wasanii tu, hivyo wakikupa miaka kumi kama hujashiba basi wanampa na mwingine akale

Kuna wabunge walio ulizwa maswali majimboni mwao mwaka 2005, tumekupa miaka 10 bado hujatosheka na huna shukrani je umesahau nini bungeni
 
sijajua akina Mpoligomi, Wilson masilingi, Mwampesya, Selelii, Sarungi, Mungai, Makweta, kama walikumbwa na falsafa ya fagio hilo mwaka 2005.
 
Pinda,membe,masele,mwigulu,Riz1,akina nape,makonda watapotea kabisa katika ulingo Wa siasa hasa mzee mamvi akishinda

Mzee wa manvi hatapitishwa, nakutompitisha huyu mzee wa Richmond itakuwa Gaza ya ccm maana mpaka sasa

wanayumba hawaelewi wanafanyaje, enzi za mwalimu teyari mambo yangekuwa hadharani, tulimfaham Mzee wa maakaa

ya mawe kiwira long akiwa waziri wa mambo ya nje, tukamfaham fast jet au dhaifu long akiwa waziri wa mambo ya nje.

Je ukiulizwa leo, au nikiulizwa ni nani atapeperusha bendera ya ccm 2015 sina ninachoelewa.
 
wakuondoka na jk ni wengi mno. muhongo, umi mwalim, maghembe, nyalandu, nkamia nk. bila kusahau zaidi ya nusu ya waliozawadiwa u-rc, dc na ubalozi. Wangelijua hili, leo wangeanza kutenda kazi vizuri kujaribu kumvutia rais ajaye. Maana jk ndo anaondoka hivyo.
 
wote walioingia na jk wataondoka naye , serikali ya UKAWA haitakuwa na nafasi yoyote kwa wanaccm .
 
Walioingia na Kikwete mbona wengi wamekwishaondoka, ni nani yuko kwenye Baraza lake la Mawaziri mpaka sasa?

au umewasahau akina Masha,Rostamu,Karamagi,lowasa,Sitta n.k, aliyebaki ni yeye tu dhaifu na ni kwa msaada mkubwa sana wa NEC,Usalama wa Taifa,Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa gharama kubwa sana ya kodi zetu na matumizi yakupita kiasi ya pesa chafu.

Ama sivyo yeye mwenyewe anajua, 2010 aliondoka, ndo maana sasa anafanya mambo yake, na ana hasira sana na wananchi.

Japo ki ukweli atayelia sana ni Kawambwa.
 
nIMECHEKA SANA HAPO KWA KAWAMBWA ! HUYU JAMAA NI GUNIA LA MISUMARI .
 
Kawambwa atarudi tu ! Nenda Bagamoyo kaulize na ufuatilie yanayofanyika pale mjini ! Lami mitaa yote , fitna ipo pale wengi wa ccm wataogopa kuchuana na Mjomba wao Kawambwa! Aliandaliwa Riz1 sasa kapata Chalinze njia nyeupe kwa Dr Shukuru K
 
tutahakikisha anang'oka.
 
Back
Top Bottom