Walimu Zanzibar Wapigwa Marufuku Kuvaa Baibui!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Na Salim Said
WIZARA ya Elimu ya Zanzibar, imewataka walimu wa shule za serikali wanaovaa baibui kujieleza kwa maandishi sababu za kuvaa nguo hizo wawapo kazini.

Waziri wa Elimu wa Zanzibar, Haroun Ally Suleiman aliliambia gazeti hili jana kuwa wizara ina mwongozo wa mavazi kwa walimu na wanafunzi wanapokuwa shuleni hivyo hawaruhusiwi kuvaa baibui.

Alisema mwongozo huo wa mwaka 1988, ndio unaowaelekeza walimu na wanafunzi aina ya mavazi wanayopaswa kuvaa wawapo shuleni.

"Zanzibar tuna mwongozo wa mavazi kwa walimu na hata wanafunzi, ulitungwa tangu mwaka 1988," alisema Haroun. Alisema kwa mujibu wa mwongozo huo, walimu wanazuiwa kuvaa baadhi ya baibui hasa zile ambazo zinazovaliwa nyakati za jioni visiwani.


Kwa habari zaidi soma Mwananchi.
 
Hapa ni kuingilia uhuru wa kuabudu/mtu binafsi, au tuseme hakuna uhuru usio na mipaka?
 

Mimi nimesema kuwa Ufaransa (sio Zanzibar) ndio waliokatazwa kuvaa hijabu na alama nyinginezo za kidini!
Mi sijazungumzia Ufaransa, nazungumzia katazo la ZNZ, ni kuwa walimu wa kike wamekatazwa kuvaa Mabaibui na si HIjab.
 
hapo hapo mkubwa naona ni yale yale kwamba bado zenj kuwa kama bongo ktk mabo fulani wanatuchokoza naenda jeshini kujifunza mabo nije kumwaga njugu maana tz sasa bila hivo hatuelewi na huyo aliesema maneno hayo sijui kama akiwa mkewe mwalimu atamrusuhu kuvaa mbali na buibui .
zenji yavamiwa trtibu
haya wazenj mwabesabesa au mwabesekewa mdogomdogo
Conquest.
 
Back
Top Bottom