Walimu watoboa siri mahusiano mwenzao, RPC Barlow

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
kamanda%20polisi%20mwanza%20barlow.jpg


Baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Nyamagana wamevunja ukimya na kueleza kile kinachodaiwa ni mahusiano kati ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Leberatus Barlow, na mwalimu mwenzao, Dororth Moses.

Wakizungumza na NIPASHE shuleni hapo jana, pia walielezea kusikitishwa kwao na jinsi tukio hilo la mauaji ya RPC lilivyotokea mbele ya mwalimu mwenzao, Doroth Moses aliyeuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia Jumamosi eneo la Kitangiri, jijini Mwanza.

Mwalimu Doroth ndiye aliyekuwa na RPC Barlow ndani ya gari wakati watu wanaosadikiwa kuwa majambazi walipowavamia na kumuua kwa kumpiga risasi Kamanda huyo.

Katika mahojiano hayo Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo, Mary Ngalula, alisema wanamuonea huruma mwalimu mwenzao kutokana na kushuhudia tukio hilo la kutisha.

Alisema wanamsikitikia kwa sababu jamii imeanza kumfikiria vibaya kwa kudhani anahusika kwa namna moja ama nyingine katika mauaji hayo.

“Tunamuonea huruma mwalimu mwenzetu kutokana na maneno tunayoyasikia, lakini sisi tuko pamoja naye kwa sababu tunamfahamu ni mtu safi, na hivi tunajiandaa kwenda kumuona na kumtia moyo ili amudu kuilea familia yake kwani ni mjane,” alisema.

Mwalimu Baraka Magafu alisema tofauti na hisia za baadhi ya watu kuhusu uhusiano wa Mwalimu Doroth na Kamanda Barlow, wao (walimu) wanafahamu kuwa ni watu wa kabila moja wanaotoka kijiji kimoja huko Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Alibainisha kuwa Mwalimu Doroth amekuwa ni mtu anayejihusisha sana na shughuli mbalimbali za watu wa kabila lake (Wachaga), hivyo hakuna sababu ya kumfikiria vibaya kwa sababu tu mtu aliyekuwa amemsindikiza nyumbani wakitokea kwenye kikao cha maandalizi ya harusi aliuawa kwa kupigwa risasi.

“Ukifuatilia mwenendo wa tukio lote, utaona kwamba kilichotokea ni bahati mbaya na kingeweza kumtokea yeyote, kwani Barlow alikuwa akimsindikiza Mwalimu Doroth nyumbani kwake, na hata baada ya tukio, alipowapigia simu wenzao waliokuwa nao kwenye kikao walikuwa ndipo na wao wanafika majumbani mwao,” alisema.

Aliongeza kwamba katika mazingira kama hayo ni makosa kuwa na mtazamo hasi dhidi ya Mwalimu Doroth kama ambavyo baadhi ya watu wameanza kuvumisha kuwa walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Wakati huo huo, majonzi, simanzi na kauli za kulipa kisasi ni miongoni mwa mambo yaliyogubika shughuli ya kuuaga mwili wa Barlow.

Mwili wa Barlow uliagwa na wakazi wa Jiji la Mwanza wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, katika shughuli iliyofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana jana.

Baada ya shughuli ya kuagwa mwili wa Barlow, ulisafirishwa baadaye jana jioni kwa ndege kuelekea jijini Dar es Salaam kabla ya leo kusafirishwa kwenda kijijini kwake Vunjo, mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.
 
Unataka sasa kusema nini katika hii sired yako, ina maana marehemu RPC Barlow katika jiji zima la Mwanza walietoka nae kijiji kimoja ni mwalimu Doroth peke yake ama wote waliokuwa kwenye hicho kikao walikua na magari ispokuwa mwalimu Doroth ndo maana marehemu RPC alimuonea huruma akampa lift. Sijasomea intelijensia lakini naona kuna jambo la zaidi ya kutoka kijiji kimoja hapo.Cha msingi wahusika wa mauaji wasakwe na wawekwe ndani kujibu mashtaka lakini chokochoko mchokonoe pweza binadamu hautamuweza hata kidogo
 
candid hii biashara iishakwisha na faida yake tayari imeshatusaidia kufanya mambo mengine makubwa
 
mwisho wa siku ukweli utabainika tu...
so far hakuna mtu atajifanya kiherere kuropoka na kuthibitisha kuwa Dorothy na Barlow walikuwa na mahusiano...
mwalimu mkuu na wengineo wametumia busara ili kuepukana na mkono wa sheria au kadhia nyinginezo...
mimi bado nina hili swali, kama kweli watu hao walikuwa ni majambazi, kwa nini hawakumdhuru huyo mama?(aliachwa hai ili awe shuhuda?) kumbuka inasemekana Barlow alipigwa risasi tokea upande wa bega la kushoto ambapo huenda mama Dorothy alikuwa amekaa...
 
ngoja na mimi nitafute mademu tuliotoka wote manyovu nijipigie kwani nikifumaniwa nasema tumetoka kijiji kimoja na huyu dada anijitolea sana kwa waliotoka kijiji kimoja.
nitajinomaje kwa fix kama hizi.
 
HEKAYA ZA ABUNUAS ZISHAANZA WANATENGENEZA MAZINGIRA YA KUMSAFISHA rpc UKWELI UTABAKI KAMA TUNAVYOUJUA MSITUZUGEE
 
mwisho wa siku ukweli utabainika tu...
so far hakuna mtu atajifanya kiherere kuropoka na kuthibitisha kuwa Dorothy na Barlow walikuwa na mahusiano...
mwalimu mkuu na wengineo wametumia busara ili kuepukana na mkono wa sheria au kadhia nyinginezo...
mimi bado nina hili swali, kama kweli watu hao walikuwa ni majambazi, kwa nini hawakumdhuru huyo mama?(aliachwa hai ili awe shuhuda?) kumbuka inasemekana Barlow alipigwa risasi tokea upande wa bega la kushoto ambapo huenda mama Dorothy almbona kuna habari kua huyo mama ni hawarayake na barlow na hilo halina ubishi,na huyo mama inasemekana amehusika moja kwa moja kupanga njama za kuuwawa kwa mpendwa wawatu wa mwanza barlow huyo mama alitumiwa kufanikisha njama yote,hizi ni tetesi zilizozagaa huko mwanza.
 
Nilitaka kunua gazeti la Nipashe kwa kudanganywa na kichwa cha habari, nikajua kuna siri kubwa.Nashukuru sijapoteza 800 yangu
 
Kichwa cha habari kizito, habari yenyewe nyepesi, sijaona siri waliyotoboa zaidi ya kusaidia kutupa maswali zaidi. Haya mauaji ya kamanda wetu yana kisa chake haiwezekani ukaniambia eti kamanda aliuawa na majambazi mbele ya huyo mwalimu, kwa jinsi ninavyowafahamu majamba wasingemuacha huyo mama kwa kuhofia kuwatambua ni lazima wangemuulia mbali na yeye
 
Back
Top Bottom