Walimu watoboa siri mahusiano mwenzao, RPC Barlow

Habari hii kuanzia kichwa cha habari imechukuliwa kutoka Gazeti la Nipashe, kichwa cha habari sijakitunga mimi.

Jambo moja la msingi ninavyofahamu RPC hulindwa wakati wote na jeshi la polisi. Nyumba anayoishi hulindwa pamoja na familia yake. Awepo asiwepo utakuta askari wanazamu ya kupokezana kulinda makazi ya RPC usiku na mchana.

Po pote aendako RPC anaendeshwa na dereva ambaye kwa namna nyingine ndiye mlinzi wake.

Mazingira ya kukutwa RPC akiwa peke yake akiendesha gari usiku akiwa na mwanamke ndani ya gari yake na hivyo kuuawa katika mazingira tatanishi bila uwepo wa dereva wake na bila ulinzi wa askari polisi kwa mujibu wa sheria kwa sasa ni jambo linalofunikwafunikwa, lakini ni kasoro kubwa ambayo sasa polisi wanategemea source moja tu ya yule mama aliyekuwa naye ambaye hakuguswa katika mauaji yale.

Kiongoze wa ngazi ya RPC hutakiwa muda wote alipo radio yake iwe on ili kubaini cho chote kinachoweza kumdhuru au mazunguzo yake yawe yanafuatiliwa na mfumo wa mawasiliano wa ofisi yake na ni njia ya usalama wa viongozi wa vyombo vya usalama.

Wenzetu polisi muda wote akiwa kazini hata wa kawaida radio na video viko on na kurekodi kila kitu na kuwa ofisini wanaona kila kitu kinavyoendelea polisi akiwapo kazini, hii husaidia utandawazi katika shughuli zao za kila siku bila kificho.

Nini kilichomwogopesha RPC kuwa na dereva wake wakati mauaji yakimkuta wakiwa wawili peke yao na mwanamke? Kwani hata mlinzi wake kama angekuwepo si Tanzania tumezoea wafanyayo wakubwa tunalinda heshima zao wakisha kunywa soda zao wakati tunajua wako wapi na tunawalinda kisha tutamfikisha salama kwake. Hata kama alitumia gari binafsi kwa nafasi yake na kwa taratibu za jeshi anapaswa kuwa na ulinzi.

Tusipokuwa waangalifu katika hili tutakuja kushangaa Rais wa nchi anaendesha collola ya Ridhiwan akiwa mazingira tatanishi yenye kuhatarisha usalama wake bila uwepo wa walinzi wake, bado tutajenga hoja za utetezi kumlinda.

Nemeshuhudia viongozi wengi wa ngazi yake hata wa chini ya ngazi yake wawapo katika vikao kama hivyo hufuatana walao na mtu au watu wenzake tena hao hawahitaji ulinzi wa pekee, sembuse RPC?
 
mimi naona cha msingi hapa sio kujua kwamba RPC na mwalimu walikuwa wanatonibana au la, sisi hiyo haituhusu. Maswali ya kujiuliza,
Huyu RPC majeshi yake yalimkosakosa kumuua afisa fulani, na RPC akatoa statement nyepesi tu. Siku chache zilizofuata na yeye akauawa kwa risasi, hakukoswakoswa.
Kama suala ni mwanamke, huyo mwalimu alikua mjane(yaani mme wake keshafariki).
Kuna mtu humu JF alisema huyu RPC alimgomea PM Pinda, kupeleka FFU sehemu ambayo PM alikua anahutubia, kwa kujibu kwamba hawezi kupeleka FFU wakati hakuna fujo.
Je reaction ya mapapa wakuu wa nchi ilikuaje baada ya hili tukio?
Hii issue inaweza ikawa ni tofauti na tunavyodhani.
 
Waandishi wa Kitanzania sijui shule zao za uandishi wanasomea wapi? sasa hiyo siri waliyotoboa iko wapi? maana kwa utata uliozingira kifo cha RPC unaposema SIRI hadhira inavutika kusoma kujua labda utata huo umetanzuliwa au baadhi ya maswali magumu yamejibiwa! poor journalists!!
 
mimi naona cha msingi hapa sio kujua kwamba RPC na mwalimu walikuwa wanatonibana au la, sisi hiyo haituhusu. Maswali ya kujiuliza,
Huyu RPC majeshi yake yalimkosakosa kumuua afisa fulani, na RPC akatoa statement nyepesi tu. Siku chache zilizofuata na yeye akauawa kwa risasi, hakukoswakoswa.
Kama suala ni mwanamke, huyo mwalimu alikua mjane(yaani mme wake keshafariki).
Kuna mtu humu JF alisema huyu RPC alimgomea PM Pinda, kupeleka FFU sehemu ambayo PM alikua anahutubia, kwa kujibu kwamba hawezi kupeleka FFU wakati hakuna fujo.
Je reaction ya mapapa wakuu wa nchi ilikuaje baada ya hili tukio?

Hii issue inaweza ikawa ni tofauti na tunavyodhani.
hili eneo linahitaji upepelezi wa kina ukizingatia kauli aliyowahi kutoa Pinda kuwa madaktari acha wagome liwalo na liwe na kilichomtokea Ulimboka najumlisha moja na moja napata mbili!
 
Mbona sioni siri iliyotobolewa hapo?
Kusikitishwa na kumuonea huruma ndiyo kutoboa siri?
 
nosense,hatuwezi kuelezwa dhamani ya uhai wa mtu na ukabila,na hao walimu wahojiwe kuna kitu wanakificha.

Funguka tukuelewe la kama ukiona kuna kitu kinafichwa songa front kafache uchunguzi
amekwenda kama walivyo kweda wengine na sisi tutafuata tuu kama sio leo kesho
 
Zitatengenezwa hadithi hapa hadi basi! Ilimradi magazeti yauzwe sana na wajuaji wa bandia waadithie jinsi walivyowafahamu Barlow na mwl. Dorothy, imradi tu kila mtu na lake. Lakini mwisho wa yote ni mapito tutasahau punde tu ikizinduliwa sinema nyengine...
 
Zitatengenezwa hadithi hapa hadi basi! Ilimradi magazeti yauzwe sana na wajuaji wa bandia waadithie jinsi walivyowafahamu Barlow na mwl. Dorothy, imradi tu kila mtu na lake. Lakini mwisho wa yote ni mapito tutasahau punde tu ikizinduliwa sinema nyengine...

Lile move la Mwangosi ndio linaishia ajabu ya hii move iko na ile ya waislamu kupiga moto makanisa lakini usisahau dogo aliekojolea Qur an,,,achana na hizo zote tisa kumi tusubiri Limove litakalo kuja mda si mrefu
styiii innn tunneeess ...Malizia na hiii ni Tanzania
 
Ndio yale yale ya viongozi wetu kuhamasisha watu kupima ngoma na kujitangaza pindi wanapokutwa na virusi huku wao hakuna hata mmoja anayefanya hivyo, au hamna kiongozi wa serikali mwenye ngoma?

Tunakazania Mwalimu ni dada ya Marehemu, Vipi majina yao ya ubini hayafanani? Marehemu aliwezaje kutoka usiku wote ule bila walinzi, au sheria ya jeshi hairuhusu kulindwa na walinzi wa jeshi akiwa na dada yake? Majambazi walipenda uhai wa wa marehemu zaidi ya gari na mali nyingine alizokuwa nazo?

Mimi nashangaa sana kwani hatakama walikuwa wapenzi sioni shida maana wote ni 18+ yrs. Ila sababu imezoeleka TZ kuwa wanaokufa na ukimwi au kufumaniwa na wake/waume za watu ni wananchi wa kawaida na si watu wenye nyadhifa za juu serikalini, basi Doro na marehemu ni mtu na dada yake
 
mimi naona cha msingi hapa sio kujua kwamba RPC na mwalimu walikuwa wanatonibana au la, sisi hiyo haituhusu. Maswali ya kujiuliza,
Huyu RPC majeshi yake yalimkosakosa kumuua afisa fulani, na RPC akatoa statement nyepesi tu. Siku chache zilizofuata na yeye akauawa kwa risasi, hakukoswakoswa.
Kama suala ni mwanamke, huyo mwalimu alikua mjane(yaani mme wake keshafariki).
Kuna mtu humu JF alisema huyu RPC alimgomea PM Pinda, kupeleka FFU sehemu ambayo PM alikua anahutubia, kwa kujibu kwamba hawezi kupeleka FFU wakati hakuna fujo.
Je reaction ya mapapa wakuu wa nchi ilikuaje baada ya hili tukio?
Hii issue inaweza ikawa ni tofauti na tunavyodhani.

Mkuu umenikumbusha hii story.

JUMAPILI iliyopita niliahidi kuelezea jinsi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alivyozomewa katika jimbo la Nyamagana, jijini Mwanza. Ilikuwa Septemba 17, mwaka huu majira ya jioni, Pinda alipowasili kwa msafara mrefu katika Uwanja wa Shule ya Msingi, Sahara katikati ya jiji la Mwanza.

Kabla ya kuwasili Sahara, jana yake, yaani Septemba 16, akiwa viwanja vya Magomeni, kata ya Kirumba, jimbo la Ilemela, jijini Mwanza, Pinda alikumbana pia na upinzani mkali wa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Wananchi wengi walimuonyesha alama ya V pamoja na bendera za CHADEMA mkutanoni hapo.

Ingawa alihutubia mwanzo hadi mwisho bila kuzomewa pale Magomeni, lakini alionekana kupatwa na hofu dakika za mwisho za hotuba yake, baada ya umati wa watu mkutanoni hapo kumtaka mbunge wao, Highness Samson Kiwia, apande jukwaani amwage sera. Pinda alikataa kwa madai kwamba huo ni mkutano wake, wala siyo wa mbunge. Baada ya Waziri Mkuu kusema hivyo, wananchi wengi walisikika wakisema: "Tunamtaka mbunge wetu azungumze, mbunge wetu, mbunge wetu msimzuie kuongea na sisi, tunamtaka mbunge wetu Highness!" Pinda akanyamaza kwa muda mfupi.

Licha ya kelele hizo, Pinda akasema kwa upole: "Aaah, mbunge wenu atakuja siku nyingine kuongea nanyi. Mkutano huu ulikuwa wangu, kisha akashuka haraka haraka jukwaani na kumfuata Mbunge Highness Kiwia akamwambia: "Naomba nisindikize wasije wakatupiga hawa watu." Kiwia akakubali, akamsindikiza hadi Pinda alipopanda gari lake.

Kesho yake akatinga pale Sahara kuhutubia mkutano wa hadhara. Watu walikuwa wengi sana. Kiprotokali Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Welle Ndikilo, ndiye aliyekuwa mwenyeji wa msafara wa Waziri Mkuu. Na kwa upande wa chama chake Pinda, mwenyeji wake alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Clement Gregory Mabina.

Baada ya muda mfupi tangu kuwasili kwa Pinda katika viwanja hivyo vya Sahara, mkuu wa mkoa alipanda jukwaani kutoa utambulisho na kuwakaribisha walengwa ili wazungumze kwenye mhadhara huo. Alianza kwa kumtambulisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Mabina, kisha kumkaribisha jukwaani japo awasalimie wananchi.

Bila ajizi, Mabina alipokaribishwa jukwaani kusalimia wananchi, hakupoteza muda. Alitoka meza kuu kisha kupanda jukwaani na kutoa salamu kwa kusema: "CCM oyeeee!" Wananchi wengi wakazomea huku wakimuonyesha alama ya V na bendera za CHADEMA. Baadaye ikabidi ashuke na kwenda kukaa.

Baada ya Mabina, mkuu wa mkoa akashika kipaza sauti, kisha akamkaribisha Waziri Mkuu kwa kusema: "Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, karibu uje uzungumze na wananchi wa Nyamagana. Wafuasi wa CCM waliokuwa wamekaa katikati ya mkutano huo wakiwa wamevalia sare za CCM wakashangilia.

Waziri Mkuu akapanda jukwaani. Akasema: "Nyamagana oyeeeee!"
Baadhi ya watu wakaitikia: "Oyeeee."
Wengine wakasema: "Hoiii!" Pinda akatabasamu, kisha akaanza kuzungumza.

Baada ya Pinda kuanza kumwaga sera za serikali na mambo mengine, wananchi wengi hasa waliokuwa wamekaa na kusimama upande wa mashariki mlimani walisikika wakianza kuzomea kupinga kile alichokuwa akikisema mkutanoni hapo.
Chanzo cha Pinda na viongozi hao kuzomewa mkutanoni hapo, ilitokana na kile kilichoonekana kuwepo kwa kero nyingi zilizodaiwa kushindwa kutatuliwa na serikali ya CCM, iliyo chini ya Rais Jakaya Kikwete.

Hali hiyo ilimlazimisha Pinda kushindwa kuhutubia kwa muda, huku akionekana kujawa jazba na kuzomewa kwake huko.
Kutokana na kelele za kuzomewa kwake kuonekana kushika kasi, Waziri Mkuu akasema: "Nyamazeni basi mnisikilize." Watu wakazomea tena. Hali hiyo ilionekana kuwashtua sana maofisa usalama wa taifa waliokuwepo uwanjani hapo. Vivyo hivyo askari polisi nao wakakumbwa na mshangao. Wakaanza kujipanga.

Wakati Pinda akiendelea kujaribu kuzungumza na halaiki hiyo ya wananchi wa Nyamagana, pia walikuwepo wananchi wengi wa wilaya jirani ya Ilemela, utulivu ulionekana kuwa sifuri, maana zomeazomea ilizidi. Lakini wakati Pinda akiwa bado yuko jukwaani huku hotuba yake ikikatizwa kwa kuzomewa, Pinda alimwita kwa jina moja mbunge wa Nyamagana kwa kusema: "Wenje..."

Wananchi wakashangilia kwa nguvu kubwa.
Kisha Pinda akasema tena: "Hii ndiyo serikali ya siku zijazo."
Akashangiliwa. Akapaza sauti kwa kusema pia: "Lakini naona hamuwezi, maana itakuwa ni serikali ya vurugu tupu kuanzia asubuhi hadi jioni."
Akazomewa.

Kufuatia hali hiyo mbaya, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliokuwepo mkutanoni hapo na silaha nzito za kivita aina ya SMG, mabomu na rungu, walionekana kwenda upande wa watu kule mashariki ilikokuwa ikisikika miluzi na zomeazomea kwa lengo la kuwatisha kuwapiga.

Baada ya kuona hivyo baadhi ya wananchi walikimbia. Wengine walibaki kusubiri liwalo na liwe. Wakati polisi wakiwa huko, Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Mwanza, Liberatus Barlow, alionekana akiwasihi wananchi hao watulie ili wamsikilize Waziri Mkuu. Lakini wapi. RPC Barlow akatumia busara na hekima kuzuia askari wake wasifanye lolote. Watu wakarudi tena maeneo yao na zomeazomea ikashika kasi zaidi.


Baada ya kuzidi zomeazomea hiyo, Pinda alilazimika kumuita Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), aliyekuwa meza kuu, na kusema: "Nyamazeni basi!. Wenje...hii ndiyo serikali ya siku chache zijazo. Lakini naona hamuwezi, maana itakuwa ni serikali ya vurugu asubuhi hadi jioni." Akazomewa, kisha wananchi hao wakaanza kuimba: "Hatuitaki CCM, hatuitaki CCM, hatuitaki CCM. Peoples power, peoples power, peoples power…"

Kutokana na hali hiyo, Pinda akiwa jukwaani huku amesogeza kipaza sauti karibu na mdomo wake, akacheka na kusema: "Hahahahaaaaaaa, huo ni wimbo tu. Hata mkiimba ‘Peoples power' hadi asubuhi, maana CCM ndiyo iko madarakani." Akazomewa. Kisha Pinda akashindwa kuendelea kuzungumza jukwaani kwa dakika kadhaa hivi. Polisi wakaonekana tena kujipanga kutuliza mambo.

Baada ya zomeazomea hiyo kuonekana kumwelemea Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa, Ndikilo, alilazimika kuingilia kati kisha kushika kipaza sauti na kusema: "Wanaozomea tunawafahamu. Na tunawafahamu waliowaleta hapa ili mje kufanya nini!" Akazomewa na yeye pia.

Hali ikatulia kidogo. Pinda akaanza kuhutubia, ambapo aliwataka wananchi hao waache ushabiki wa kisiasa na kwamba Halmashauri ya Jiji la Mwanza inayoongozwa na CHADEMA ndiyo inayopaswa kulaumiwa iwapo itashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wake.

"Hapa jiji la Mwanza linaongozwa na CHADEMA. Meya wa CHADEMA, mwenyekiti wa Mipango Miji wa CHADEMA, Naibu Meya ni wa CHADEMA. Lakini kama wameshindwa kuweka mipango mikakati ya kuwasaidia tutasema hawafai," akasema kisha akazomewa. Hata hivyo, baada ya hali kutulia kidogo, Pinda alichokoza nyuki tena baada ya kuwaambia wananchi wa jiji la Mwanza hasa vijana waondoke mjini kisha waende vijijini wakalime.

"Vijana acheni ushabiki. Ondokeni mjini nendeni vijijini mkalime."
Wananchi wengi wakamzomea tena. Safari hii alizomewa sana.

Ingawa Pinda alilazimika kutumia muda mfupi kutoa hotuba yake, aliwaomba wana Mwanza washirikiane kuleta maendeleo yao na kwamba iwapo tatizo ni mkurugenzi wa jiji suala hilo litaangaliwa. Aliwaomba wadumishe amani iliyopo hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na serikali kupambana na vitendo vya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria, ili kuweza kuzua samaki wadogo wasivuliwe kisha kuharibu mazalia ya rasilimali hiyo.

"Jambo jingine ninalotaka kuwaeleza hapa leo ni hili la uvuvi haramu. Samaki ndani ya Ziwa Victoria wameisha (akazomewa). Kisha akasema tena: "Aaah hata hili nalo mnazomea? Nawaombeni sana tupambane na uvuvi usiozingatia sheria. Tushirikianeni kupambana na vitendo hivi." Baada ya kusema hayo, akazomewa tena.

Baadaye Waziri Mkuu alifikia tamati ya hotuba yake katika mkutano huo wa Sahara. Na wakati akiondoka uwanjani hapo, baadhi ya wananchi walionekana wakirusha mawe kupiga magari yaliyokuwa kwenye msafara wake. Hali ikawa tete tena.
Muda mfupi baada ya msafara wa Pinda kuondoka uwanjani hapo, gari moja la polisi lililokuwa limejaa askari kanzu lilirudi Sahara kwa lengo la kupima upepo. Lakini nalo lilinusurika kupondwa mawe huku makachero hao wakizomewa. Liliondoka kwa kasi sana ili kukwepa hatari iliyoonekana eneo hilo.


Lakini Waziri Mkuu Pinda kesho yake akiwa kwenye majumuisho ya ziara yake hiyo, iliyoanzia Kahama Shjinyanga, Geita na kisha mkoani Mwanza, alivunja ukimya kwa kusema: "Kama mimi nimezomewa, ni kiongozi yupi atakayeenda uwanjani hapo asizomewe? Wakati hali hiyo ikiendelea uwanjani hapo, Wenje aliniambia tangu umalizike uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza hawajafanya mkutano wa hadhara kuwaeleza wananchi utatuzi wa kero zao."

Mizengo Pinda alizomewa hivi Mwanza
 
kamanda%20polisi%20mwanza%20barlow.jpg


Baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Nyamagana wamevunja ukimya na kueleza kile kinachodaiwa ni mahusiano kati ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Leberatus Barlow, na mwalimu mwenzao, Dororth Moses.

Wakizungumza na NIPASHE shuleni hapo jana, pia walielezea kusikitishwa kwao na jinsi tukio hilo la mauaji ya RPC lilivyotokea mbele ya mwalimu mwenzao, Doroth Moses aliyeuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia Jumamosi eneo la Kitangiri, jijini Mwanza.

Mwalimu Doroth ndiye aliyekuwa na RPC Barlow ndani ya gari wakati watu wanaosadikiwa kuwa majambazi walipowavamia na kumuua kwa kumpiga risasi Kamanda huyo.

Katika mahojiano hayo Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo, Mary Ngalula, alisema wanamuonea huruma mwalimu mwenzao kutokana na kushuhudia tukio hilo la kutisha.

Alisema wanamsikitikia kwa sababu jamii imeanza kumfikiria vibaya kwa kudhani anahusika kwa namna moja ama nyingine katika mauaji hayo.

“Tunamuonea huruma mwalimu mwenzetu kutokana na maneno tunayoyasikia, lakini sisi tuko pamoja naye kwa sababu tunamfahamu ni mtu safi, na hivi tunajiandaa kwenda kumuona na kumtia moyo ili amudu kuilea familia yake kwani ni mjane,” alisema.

Mwalimu Baraka Magafu alisema tofauti na hisia za baadhi ya watu kuhusu uhusiano wa Mwalimu Doroth na Kamanda Barlow, wao (walimu) wanafahamu kuwa ni watu wa kabila moja wanaotoka kijiji kimoja huko Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Alibainisha kuwa Mwalimu Doroth amekuwa ni mtu anayejihusisha sana na shughuli mbalimbali za watu wa kabila lake (Wachaga), hivyo hakuna sababu ya kumfikiria vibaya kwa sababu tu mtu aliyekuwa amemsindikiza nyumbani wakitokea kwenye kikao cha maandalizi ya harusi aliuawa kwa kupigwa risasi.

“Ukifuatilia mwenendo wa tukio lote, utaona kwamba kilichotokea ni bahati mbaya na kingeweza kumtokea yeyote, kwani Barlow alikuwa akimsindikiza Mwalimu Doroth nyumbani kwake, na hata baada ya tukio, alipowapigia simu wenzao waliokuwa nao kwenye kikao walikuwa ndipo na wao wanafika majumbani mwao,” alisema.

Aliongeza kwamba katika mazingira kama hayo ni makosa kuwa na mtazamo hasi dhidi ya Mwalimu Doroth kama ambavyo baadhi ya watu wameanza kuvumisha kuwa walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Wakati huo huo, majonzi, simanzi na kauli za kulipa kisasi ni miongoni mwa mambo yaliyogubika shughuli ya kuuaga mwili wa Barlow.

Mwili wa Barlow uliagwa na wakazi wa Jiji la Mwanza wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, katika shughuli iliyofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana jana.

Baada ya shughuli ya kuagwa mwili wa Barlow, ulisafirishwa baadaye jana jioni kwa ndege kuelekea jijini Dar es Salaam kabla ya leo kusafirishwa kwenda kijijini kwake Vunjo, mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.
majambazi waliomuuwa walichukua kitu gani?Au walikuwa na nia ya kumuua tu?Kama nia ilikuwa ni kumuua tu,ambako nchi yetu inaelekea kuhusu usalama wa viongozi wetu hali ni mbaya na inatisha.
 
Taarifa nilizopata kuwa huyo mwalimu ni mke wa yule jamma wa uhamiaji aliyenusurika kuuawa jana yake na polisi kwa kuisiwa ni jambazi. Inasemekana kuwaKamanda Barlow alitoa maagizo auawe ili abaki na mke wake. Sasa jamm wa uhamiaji kafanya kweli.
 
Mwanzoni tuliambiwa kuwa RPC alikuwa anamsindikiza dada yake.
Leo hii walimu hawataji kabisa uhusiano wa RPC na Doroth kuwa ni uhusiano wa 'kaka' na 'dada' !!
Labda kutoka nae kijiji kimoja ndio anakuwa 'dada' yake !!
Kama ni kweli, basi RPC alimpenda sana huyo 'dada' yake, mpaka akawa anamsindikiza 'nyumbani' usiku wa manane bila ulinzi !!!!
 
Sasa kwa nini wamemkamata Fumo Felician ati kwa kuwa ni mdogo/rafiki wa hawala wa Mwl. Doroth? Mungu ndiye anajua ukweli.
 
mimi nadhani tuachane na mwalimu na marehemu. ninayemsikitia ni huyu mama anaelia kwa uchungu mwingi na maswali mengi yasio kuwa na majibu. kufiwa na mume wake kisa usaliti ndani ya nyumba. sababu ni kweli mume wake alikuwa na mausiano nje ya ndoa. jamani wanawake/wanaume tumuombe sana tuwe waaminifu maana kwa akili zetu hatuwezi.....
 
Back
Top Bottom