Walimu watatu, mzabuni kortini wakituhumiwa kuiba

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
WALIMU watatu wa Shule ya Msingi Tukoma, Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Mpanda na mzabuni wa halmashauri hiyo, wakikabiliwa na mashtaka 68 yanayohusiana na wizi ya zaidi ya Sh21 milioni.

Waliosomewa mashtaka hayo mbele Hakimu Mkazi Mfawidhi, Richard Kasele, ni Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Joel Mwakyusa (37) na walimu wenzake, Renatus Ngairo (50), Joackim Katabi (39) na mmiliki wa Kampuni ya Royal Stationary, Fredrick Mlenge (50).

Mwendesha Mshtaka wa Polisi, Finias Majura, alidai kuwa washtakiwa kwa pamoja walitenda kosa hilo Novemba 28, 2009 na Agosti 28, 2011 kwa nyakati tofauti.
Miongoni mwa mashtaka ni kula njama za kumuiba mwajiri wao wakiwa watumishi wa Serikali na kumdanganya mwajiri na kujipatia Sh21.8 milioni.

Pia, wanadaiwa kutengeneza hati bandia ya kujipatia fedha kupitia Benki ya NMB tawi la Mpanda kwa kutumia jina la Mwalimu Mkuu wa Shule, kwa kutumia hundi namba 002490788 yenye thamani ya Sh850,000.

Majura alidai kuwa watuhumiwa watatu ni walimu ya shule ya msingi, kwa nyakati tofauti wakishirikiana na mzabuni wa Kampuni ya Royal Stationary, walishirikiana kumuiba mwajiri ambaye ni Halmashari ya Wilaya ya Mpanda kiwango hicho cha fedha za ujenzi wa madarasa.

Washtakiwa hao walikana mashtaka yote na Hakimu Kasele aliamuru warudishwe rumande hadi mahakama itakaposikiliza ombi lao la dhamana.
 
Asante kamanda kwa taarifa.Ngoja sheria ichukue mkondo wake, huyo Joackim Katabi "39" tulikuwa naye chuoni Kasulu 1994-1996 alikuwa waziri wa chakula alikuwa akishirikiana wapishi pamoja na matron kuiba chakula matokeo yake ni baadhi ya wanachuo kumis chakula, na hivyo ufisadi hajaanza leo ni fisadi la miaka mingi.
 
Kumbe unamfahamu mkuu?
 
Back
Top Bottom