Walimu wapya Dodoma walipwa posho za kujikimu

Sumasuma

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
342
110
Hamisi Mwesi, Dodoma
HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma, imetumia Sh54 milioni kulipa posho za walimu 133 wa shule za sekondari waliopangiwa kufanya kazi katika halmashauri hiyo.

Juzi walimu hao wapaya waliandamana kwenda katika viwanja vya bungeni kushinikiza kulipwa posho hizo.

Jana mwandishi wa habari hizi, alishuhudia mkusanyiko wa idadi kubwa ya walimu hao katika ofisi za elimu ya sekondari za halmashauri ya manispaa hiyo, wakisubiri kulipwa fedha zao.

Kulipwa kwa posho hizo ni utekelezaji wa ahadi iliyokuwa imetolewa na uongozi wa manispaa hiyo ya kulipwa walimu fedha hizo jana.

Kaimu Ofisa Elimu wa Shule za Sekondari katika Manispaa ya Dodoma, Suma Mwampulo, alisema fedha hizo ni kwa ajili ya posho ya kujikimu kwa siku saba na nauli walizotumia kutoka makwao kwenda katika manispaa hiyo.

“Tumetumia zaidi ya Sh54 milioni kuwalipa walimu hawa 133 posho zao za kujikimu kwa siku saba na nauli walizotumia kutoka makwao kuja Dodoma,” alisema Mwampulo.

Alisema walimu hao wamepangwa katika shule mbalimbali za manispaa hiyo na kwamba wameajiri hivi karibuni, katika jitihada za Serikali za kupunguza tatizo la upungufu wa walimu katika shule za sekondari hasa za kata.

“Tunaishukuru serikali kwa kusikiliza kilio chetu lakini bado kuna upungufu katika baadhi ya shule tunazidi kuiomba Serikali iajiri walimu zaidi ili kumaliza kabisa tatizo la walimu nchini, ”alisema Mwampulo
Pia aliwataka walimu hao kuwa wavumilivu katika utendaji wao na kukubali kuwa na moyo wa kujitolea katika kuitumikia nchi yao.
 
Hongera Halmashauri kwa kutekeleza wajibu wenu, haya waalimu wapya shime muwasaidie wadogo zetu sasa. Najua mtakutana na changamoto nyingi, but naamini utendaji wetu na ubunifu utawaweka panapo nafasi.
 
Kuna thread inayohusu ndugu zetu. seminary za kiislamu dodoma vipi matokeo yake?
 
safi lakini kuna halmashauri zingine zinzingua kuwalipa walimu wanatakiwa waadhibiwe
 
Back
Top Bottom