Walimu wachapwa viboko na wazazi

NAPITA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
5,076
2,244
[h=3]WALIMU WACHAPWA FIMBO NA WAZAZI SHULENI.[/h]
Itakumbukwa kuwa Mwaka 2009 ilitoke tukio la Mkuu wa Wilaya Bukoba wakati huo Bw, Albert Mnali aliyeamuru polisi mmoja kuwachapa viboko walimu katika shule tatu za msingi zilizoko wilayani kwake kutokana na kushika mkia katika matokeo ya darasa la saba. Sasa hali imekuwa tofauti uko Morogoro baada ya safari hii walimu kuchalazwa na wazazi
[h=2]Kundi la wazazi wa watoto wanaosoma katika Shule ya Msingi Kinole, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, mkoani Morogoro, wamevamia shule hiyo na kuwachapa walimu bakora na kusababisha baadhi yao (walimu) kujeruhiwa.

Habari kutoka shuleni hapo zilizothibitishwa na Ofisa Elimu wa Halmashauri hiyo, Donald Temba, zinaeleza kuwa wazazi hao walifanya kitendo hicho juzi wakidai kuchoshwa na vitendo vya walimu hao vya kuwachapa watoto wao.

Kutokana na tukio hilo, uongozi wa halmashauri umeifunga shule hiyo hadi hapo maamuzi mengine yatakapotolewa.

Akielezea tukio hilo, Temba alisema lilifanywa na wazazi hao baada ya walimu kutoa adhabu kwa wanafunzi kwa makosa waliyofanya.

Alisema wazazi hao walivamia shule hiyo wakimtuhumu Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Jaka Lukome, kuwachapa wanafunzi wawili bakora.

Kwa mujibu wa Temba, wanafunzi hao walichapwa bakora siku mbili zilizopita kutokana na kosa la kupigana wakiwa shuleni.

“Kuna adhabu zilikuwa zimetolewa kwa wanafunzi wawili wa shule hiyo. Ndiyo kikawa chanzo cha wazazi hao kuandamana na kuvamia shuleni hapo na kuwapiga bakora walimu,” alisema Temba.

Hata hivyo, alilaani kitendo cha wazazi kuvamia shule na kuwachapa walimu bakora.

Alisema kitendo hicho kinaweza kuzorotesha maendeleo ya elimu katika kijiji cha Kinole kutokana na walimu kuogopa kufanya kazi katika shule hiyo.

Aliutaka uongozi wa serikali ya wilaya ya Morogoro kuwachukulia hatua za kisheria wazazi waliofanya kitendo hicho kwa kuwa kimewadhalilisha walimu mbele ya wanafunzi wa shule hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Julius Madega, alisema wamefikia hatua ya kuifunga shule hiyo baada ya kutokea vurugu hizo na hivyo kuhatarisha amani dhidi ya wazazi na walimu.

Alisema wanakusudia kuwahamisha baadhi ya walimu na kuwapeleka shule nyingine, akiwamo mwalimu mkuu wa shule hiyo.

Nao wakazi wa wilaya hiyo, Gladness Masimba na Abdallah Mwombosa, walilaani kitendo cha wazazi hao kuwachapa walimu bakora.

Walisema kitendo hicho ni kibaya kwani kitachangia kuua elimu katika kijiji hicho.

Waliutaka uongozi wa wilaya kuwachukulia hatua kali wazazi hao ili kukomesha tabia hiyo kwa wengine wanaofikiria kufanya kitendo hicho.

Hata hivyo, kufuatia vurugu hizo Jeshi la Polisi Wilaya hiyo ya Morogoro inawashikilia wahusika wa tukio hilo na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.[/h]Source:Bapromas.blogspot.com
 
Baada ya kuisoma hii nimemkumbuka yule mkuu wa wilaya aliewachalaza bakola sijui yuko wapi kwa sasa ila pole yao.
 
Poleni sana walimu,hapo ndipo tulipofika baada ya miaka 50 ya uhuru kwa mwl. Kuchapwa viboko.Alianzisha Mkuu mmoja wa wilaya bila kuchukuliwa hatua za kisheria,na sasa wazazi.baadaye hata wanafunzi watawachapa.
Ni wapi walimu wanaelekea?Nani wa kuwatetea?
"nasema wapigwe tu"

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums
 
mtoto umleavyo ndivyo akuavyo hao wazazi watajua hili baadae sio sasa...
 
Hao wazazi ni vilaza pia, mwalimu ni mlezi hivyo anapomwadhibu mwanafunzi anayekosea lengo lake ni kumkanya.Hawa wanafunzi wanaofanya makosa na kuachwa baadaye huandika mazombi kwenye mitihani harafu wazazi hao hao huwajia juu walimu. Jeshi la polisi lifanye upelelezi wa haraka na kuwatia nguvuni wahusika wote maana hatuwezi kujenga taifa imara na endelevu huku tukiwa na wajinga wengi kiasi hiki!

Hapo sasa kwenye RED huwa wanachelewa sana hadi watu wanasahau na maisha yanasonga.
 
walim walikisea kulichukulia hatua hilo kosa kwan adhab ya kosa hilo ni kufukuzwa shule huruma yao imewaponza
 
Hawa wazazi nahisi walikuwa wamelewa pombe za kienyeji na Walimu msiwe wepesi wa kukubali mambo ya kijingakijinga kama haya angalieni na nyie msiwe vichwa vya mwendawazimu.

Ishu halisi sio viboko, ni michango iliyokithiri bila maelezo aliyokuwa anachangisha huyo m/mkuu. Viboko vimetumika tu kama tafsida kulinda watu
FROM RELIABLE SOURCE.
 
Ishu halisi sio viboko, ni michango iliyokithiri bila maelezo aliyokuwa anachangisha huyo m/mkuu. Viboko vimetumika tu kama tafsida kulinda watu
FROM RELIABLE SOURCE.
?????mhh kazi kweli kweli
 
Waalimu wa Tz tuna matatizo ya kifikra,hebu jiulize ww kama mtu mzima achilia mbali mwalimu hata kama ni msukuma mkokoteni ama muuza karanga unawezaje ukakubali binadamu mwenzio akakugonga bakora?

Tena wamekufata kwako? Kweli? Kwanini isiwe vita hata kama wao wana bakora kwanini ww usichukue mawe? Kweli mtu akufate kwako akufanye anavyojisikia na ww upo tu?

Waalimu mmezidi kuwa mapwoyoyo,serikali inawapiga na mishahara duni bado na wahuni wawagonge bakora? Wajinga kabisa nyinyi tena hamfai hata kuwafundisha watoto kama hamuwezi kupinga uonevu si mtawaambia watoto nao wawe watiifu hata kwa serikali za kidikiteta kama hii ya hapa? Shenzi sana nyie.
 
Hii habari ipo biased sana!Hainiingii akilini wazazi wafikie hatua ya kuwachapa walimu kisa eti wamewachapa watoto wao waliokuwa wanapigana tena mara moja tu.Kuna kitu zaidi ya hicho hao walimu wamekifanya waache kutufanya sisi wajinga kwa habari za kizushi kama hizi.
 
Ni dhuluma kwa wanaofundisha hawana wa kuwatetea maana hata chama chao/ umoja wao ni wa kinafiki
Umoja wa waalimu ni kukata mishahara yao midogo na wakila makato yao tu na matatizo kama haya hayashughulikiwi hata kidogo. "WALIIMU UNGANENI HATA MISHAHARA MTABORESHEWA LAKINI BILA HIVYO NI KELELE TU KAMA ZA CHURA KWA MTEKA MAJI
"
Na wakiambiana wagome wanakataa sasa hii ndo shukrani ya mwananchi maana hajui taabu ya mwalimu
(mwalimu anamkopo/anabili dukani/anamadeni mtaani/anafanyabiashara ndogondogo nk) bado ukamchape kwa kukusaidia mwanao katika mazingira haya
Ombi
"Hasira za wananchi zisiichie kwa walimu bali ziende kwa walengwa waliosababisha ugumu wa wao kutafuta riziki na pia waache unafiki wakati wa kura na kwasasa wavumilie waliyoyataka wao kwa mikono yao huku wakifurahi na kunywa"
 
huu ni ukosefu wa nidhamu hata iwe ni kwasababu gani. Viongozi wa walimu toeni kauli haiwezekani walimu wapigwe wakiwa kazini halafu mkae kimya mkisubiri kuandaa maandamano ya kudai mshahara mpya.
 
Usitukane mamba kabla hujavuka MTO. Najua madhara ya kukolofishana na walimu. Nilipata mswaki malidadi Wa history hata niliporeseat tens nikagundua nilikuwa simpendi Yule Mwl. Kiukwel mtoto wako kama hawezi kumuheshimu anaemtoa moshi kichwani chelea chelea atakuja kukutoa wwe mzazi moshi wako Wa kutikumtambulisha majukumu yake.
 
au nawe uliwacharaza?mi naona,hata kama wazazi kuna mambo yanawakera kuna sehemu za kulalamika na sio kuchukua sheria mkoni,wakifikishwa mbele ya sheri watajibu mambo maswali yafuatayo;- kufanya tendo la shambulio la mwili na udharirishaji.
 
haya mambo serikali itoe elimu kwa wananchi na kuboresha mahusiano baina ya walimu na wazazi(jamii kwa ujumla).kuna shule moja kigoma,mwl wa jiog amchapa mkononi binti aitwaye hadja f3 2014 akajifanya amezimia,wazazi waliandamana kila mmoja akisema yake,walimchukua na kumpeleka zahanati,lkn mganga na wahudumu nao walikataa kupokea.baadae aliamka na maisha yakaendelea.so naona kuna sababu ya kuporesha mahusiano.
 
Back
Top Bottom