Walimu kupongezana kwa matokeo mabovu ya wanafunzi ni uzalendo?

Seif al Islam

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
2,156
638
mara baada ya kutoka kwa matokeo ya mtihani ya kidato cha nne mwaka 2012 yanayoonyesha kufeli kwa wanafunzi zaidi ya 60% waalimu wamekuwa wakisambaziana meseji za kupongezana na kuhimizana kuendelea na msimamo wao wa mgomo baridi.hili limejidhihirisha hata katika kipindi cha kipima joto itv.hebu tuulizane jamani huu ni uzalendo?
 
ni uzalendo tena haswa lakin kama huna akili timamu na una akili mgando huwezi ona uzalendo upo wapi walimu kazaneni hadi tanzania one atote na 4 ya 30 ili serikali itie akili itambue mchango wa mwalimu
 
Wewe unapojilipa posho kwa siku dola 430,mwalimu ukampa mshahara sh 350000 bila makato unategemea nini?
 
mara baada ya kutoka kwa matokeo ya mtihani ya kidato cha nne mwaka 2012 yanayoonyesha kufeli kwa wanafunzi zaidi ya 60% waalimu wamekuwa wakisambaziana meseji za kupongezana na kuhimizana kuendelea na msimamo wao wa mgomo baridi.hili limejidhihirisha hata katika kipindi cha kipima joto itv.hebu tuulizane jamani huu ni uzalendo?

kwanza unapaswa kuelewa nini maana ya uzalendo,na kwa mujibu wa mada yako unamaanisha kuwa kupongezana kwao si uzalendo,unadhan mtu afanye kitu gani ili awe mzalendo au aitwe mzalendo(kwa mtazamo wako)na pia je ww ni mzalendo?unatumia kipimo gani kumjua mzalendo na ndumilakuwili?
 
Hiyo ndio silaha yao japo ina madhara makubwa kwa taifa na maadam ujumbe wao umefika bila shaka watajipongeza bila kujali athari zake.
 
Hapana! Uzalendo ni waalimu kudai haki zao na za wanafunzi lkn wakapewa majibu ya chooni, wanyama kutoroshwa wahusika wakaendelea kutanua wakiwemo usalama wa Taifa, mabomu kuuwa mbagala na go/mboto waziri na wahusika wengine wakaendelea kupeta, mawaziri na watendaji wa serikali kudanganya uma bila kuwajibishwa, 'uzalendo uko mwingi kweli ndani ya serikali yako wala usiwe na wasiwasi...
 
mkuu unanivunja mbavu zangu, hata me nawaunga mkono wagome hadi tanzania one awe na four ya 32
ni uzalendo tena haswa lakin kama huna akili timamu na una akili mgando huwezi ona uzalendo upo wapi walimu kazaneni hadi tanzania one atote na 4 ya 30 ili serikali itie akili itambue mchango wa mwalimu
 
na bado yatakuja maana nazi ni nazi tu, basi yawezekana akaenda mahakamani jk kupinga zero za watoto
 
Kwa jinsi walivyorudishwa kazini kwa nguvu huku wakidhihakiwa kuwa mgomo wao hauna madhara isipokuwa wamejirundukia kazi tu maana ni lazima wakamilishe syllabus kwa nini wasipongezane kwa kuikamilisha vyema? Viongozi wetu wanafikiri ki Masaburi sana, angalia Kenya wanaojua umuhimu wa elimu wamemaliza tatizo la waalimu kiustaarabu bila vitisho na bado wamewahaidi kuwaboreshea mazingira ya kazi si umeona matokeo yao ya kidato cha nne? Tutaendelea kuwa vibarua tu kwenye jumuiya ya EA maana wenzetu wanapaa kielimu sisi tunaleta siasa tu.
 
Hivi unaweza kututhibitishia kuwa walio fanya hivyo ni walimu?
Kwani si mtu yeyote anaweza kutunga sms akaanza kuisambaza alaf ikaonekana ni walimu?

Lakini hii inaonesha jinsi walivyo choka hadi wana ona wapongezane maana wanaona kupitia hili janga pengine matatizo yao yatapata ufumbuzi!

mara baada ya kutoka kwa matokeo ya mtihani ya kidato cha nne mwaka 2012 yanayoonyesha kufeli kwa wanafunzi zaidi ya 60% waalimu wamekuwa wakisambaziana meseji za kupongezana na kuhimizana kuendelea na msimamo wao wa mgomo baridi.hili limejidhihirisha hata katika kipindi cha kipima joto itv.hebu tuulizane jamani huu ni uzalendo?
 
Kwa jinsi walivyorudishwa kazini kwa nguvu huku wakidhihakiwa kuwa mgomo wao hauna madhara isipokuwa wamejirundukia kazi tu maana ni lazima wakamilishe syllabus kwa nini wasipongezane kwa kuikamilisha vyema? Viongozi wetu wanafikiri ki Masaburi sana, angalia Kenya wanaojua umuhimu wa elimu wamemaliza tatizo la waalimu kiustaarabu bila vitisho na bado wamewahaidi kuwaboreshea mazingira ya kazi si umeona matokeo yao ya kidato cha nne? Tutaendelea kuwa vibarua tu kwenye jumuiya ya EA maana wenzetu wanapaa kielimu sisi tunaleta siasa tu.

Mzaha mzaha hutumbua usaha! Japo wanaoumia ni watoto wa maskini, lakini tutafanyaje, wazazi wao ndio wanaichagua ccm kila mwaka, na sisi tunakula nao sambamba, no way out, kama walisema mzigo unazidi kuwa mkubwa kwani ni lazima tuikamilishe syllabus, sasa syllabus imekamilika, tatizo nini? Naamini matokeo ya form four mwakani, yatakuwa ya hatari zaidi, UNLESS WAJIFUNZE NA WASIKILIZE KILIO CHETU, VINGINEVYO.....KAZI WATANZANIA WATAIONA...MWALIMU SIYO MTU WA KUDHARAULIWA KIASI HIKI, AMINI NAWAAMBIA, MWAKANI KUTAKUWA KILIO NA KUSAGA MENO!!!!
 
tushangilia kama mazuzu wakati Akina kawambwa, mulugo na jimii yao hawasomi kwenye shule zetu. tunalostishana wenyewe halafu tunapongezana. wanaofeli ni watoto wetu, wadogo zetu, kaka zetu, dada zetu, wapwa zetu, binamu zetu na wanaofanana na hao. hivi nyie watu akili zetu mlizipeleka wapi? tunashangilia mkuki unaokuja kutuchoma wenyewe. kwenye JF kuna mataahira wengi. aheri hata ya mbowe anayesema tuandamane kuwaondoa akina kawambwa, mulugo na wanaofanania. angalau kuna mantiki.
 
Mzaha mzaha hutumbua usaha!
Japo wanaoumia ni watoto wa maskini, lakini tutafanyaje, wazazi wao ndio
wanaichagua ccm kila mwaka, na sisi tunakula nao sambamba, no way out,
kama walisema mzigo unazidi kuwa mkubwa kwani ni lazima tuikamilishe
syllabus, sasa syllabus imekamilika, tatizo nini? Naamini matokeo ya
form four ''mwakani'', yatakuwa ya hatari zaidi,

UNLESS WAJIFUNZE NA WASIKILIZE KILIO CHETU,
VINGINEVYO.....KAZI WATANZANIA WATAIONA...MWALIMU SIYO MTU WA
KUDHARAULIWA KIASI HIKI, AMINI NAWAAMBIA, MWAKANI KUTAKUWA KILIO NA
KUSAGA MENO!!!!

Jamani mtihani tunaouzungumza ni wa mwaka jana ila matokeo yalitangazwa mwaka huu. Mtihani wa mwaka huu bado!
 
Back
Top Bottom