Walimu kuandamana nchi nzima

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698

mukoba_1.jpg

BARAZA la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT), limetoa siku 14 kwa wakurugenzi wa halmshauri nchini kuwapa barua za kuwapandisha vyeo walimu wanaostahili la sivyo watafanya maandamano nchi nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema maazimio ya baraza hilo yalifikiwa tarehe 28 mwezi uliyopita mkoani Morogoro.

Mukoba, alisema ifikapo Septemba 15 mwaka huu kama wakurugenzi watakuwa hawajawapatia walimu wanaostahili barua za kuwapandisha vyeo, basi watarajie maandamano ya walimu kwenye ofisi zao.

"Baraza limetoa siku 14 kuanzia siku ya kikao na ifikapo siku ya tarehe 15 kama walimu wanaostahili kupandishwa vyeo watakuwa hawajapewa barua zao, kutafanyika maandano ya nchi nzima kuelekea kwa wakurugenzi wa halmashauri kudai barua hizo, hatupendi hali hii itokee lakini hatufurahishwi na hali ya kutojali haki zetu," alisema Mukoba.

Aidha, Mukoba alisema Baraza limekemea tabia ya serikali ya kuwanyang'anya walimu madaraja ambayo tayari wamekwishayapokea kwa kisingizio cha kutokuwapo fedha za kulipa.

Alisema hata nyongeza ya mishahara iliyotolewa Julai mwaka huu imepingwa na walimu nchi nzima, kwani mbali ya kuwa ndogo sana imetolewa kwa upendeleo na walimu wanataka kujua ni kwanini watumishi wengine waongezwe kwa asilimia kumi na walimu asilimia 6.35.

CHANZO: Tanzania Daima
 
hizo ni kampeni miezi mitano iliyopita mlisema mishahara juuuu!sasa mnangonjera nyingine cwt m&@?;k*&u!@?@n?;&_&d@&+&@u
 
Duh,vyeo hadi muandame?Nyie mnaleni tu chini ya pazia.
Kama kuandamana wangeanza askari Polisi,wanaosote vyeo hadi wanazeeka
Yaani nyie mkikaa kimya muda kisha mnaibuka na jipya.Sasa andamaneni kuna waalim kibao wamemaliza vyuo Ajira hawana,msitushughulishe.
Kisha na sie wazazi tutaandamana kwa michango yenu ya ujasiatumbo mashuleni..
 
Viongozi wote wa vyama wafanyakazi na baadhi ya vyama vya siasa ni matawi ya CCM.

Huyo KIPOCHI ndiyo walewale.
 
Hakuna lolote mnawafanya walimu kama hawajielewi kwa sababu mnawapeleka mnavyotaka. Mara mishahara isipopanda mtaandamana, wakiandamana dakika za mwisho mnatangaza kusitisha mgomo. Mkoba tumekuchoka sasa na ngonjera zako. Tumeshakujua wewe uko upande gani.
 
Mukoba nimeona taarifa yako kuhusu niseme matatizo ya walimu kwa wewe kutoa angalizo kuwa mnapango mgomo.Nauliza ni nani hasa atagoma?Hivi kweli walimu wa Tanzania wanaweza kufanya mgomo? Wanawezaje kujitoa ujuha na wewe umejaa uccm?

mukoba_1.jpg

BARAZA la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT), limetoa siku 14 kwa wakurugenzi wa halmshauri nchini kuwapa barua za kuwapandisha vyeo walimu wanaostahili la sivyo watafanya maandamano nchi nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema maazimio ya baraza hilo yalifikiwa tarehe 28 mwezi uliyopita mkoani Morogoro.

Mukoba, alisema ifikapo Septemba 15 mwaka huu kama wakurugenzi watakuwa hawajawapatia walimu wanaostahili barua za kuwapandisha vyeo, basi watarajie maandamano ya walimu kwenye ofisi zao.

“Baraza limetoa siku 14 kuanzia siku ya kikao na ifikapo siku ya tarehe 15 kama walimu wanaostahili kupandishwa vyeo watakuwa hawajapewa barua zao, kutafanyika maandano ya nchi nzima kuelekea kwa wakurugenzi wa halmashauri kudai barua hizo, hatupendi hali hii itokee lakini hatufurahishwi na hali ya kutojali haki zetu,” alisema Mukoba.

Aidha, Mukoba alisema Baraza limekemea tabia ya serikali ya kuwanyang’anya walimu madaraja ambayo tayari wamekwishayapokea kwa kisingizio cha kutokuwapo fedha za kulipa.

Alisema hata nyongeza ya mishahara iliyotolewa Julai mwaka huu imepingwa na walimu nchi nzima, kwani mbali ya kuwa ndogo sana imetolewa kwa upendeleo na walimu wanataka kujua ni kwanini watumishi wengine waongezwe kwa asilimia kumi na walimu asilimia 6.35.

CHANZO: Tanzania Daima
 
Walimu wa nchi hii hii au Kenya!? Hakuna mgomo hapo ni vinanda na zeze tu la mukoba
 
Labda siyo walimu watz hii,kama wataandamani mimi najinyonga,
 
Walimu hawawezi kugoma wamesha jua mchezo wanaochezewa na hawa viongozi wa chama chao tena huyu mkoba ndo hafai kabisa.
 
Haiwezekani, mkwara huu sijui WA nini, kama kugoma/kuandamana ilikuwa ule mwaka mukoba alipotaka kupigwa pale Diamond Jubilee.
 
Duh,vyeo hadi muandame?Nyie mnaleni tu chini ya pazia.
Kama kuandamana wangeanza askari Polisi,wanaosote vyeo hadi wanazeeka
Yaani nyie mkikaa kimya muda kisha mnaibuka na jipya.Sasa andamaneni kuna waalim kibao wamemaliza vyuo Ajira hawana,msitushughulishe.
Kisha na sie wazazi tutaandamana kwa michango yenu ya ujasiatumbo mashuleni..
kweli walimu wanakazi kubwa sana!
 
Back
Top Bottom