Wakili wa shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2022
- 1,689
- 3,267
Habarini. Mnakumbuka samaki aliokamata kutoka kwa wachina waliokuwa wanavua kwenye bahari yetu kwa Magendo? Basi wale samaki waligawiwa kwenye vyuo na mashule mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam. Samaki wale walinikuta nikuchukua diploma ya unesi kwenye chuo fulani jijini Dar. Chuoni pale tulikuwa tunapikiwa chakula na sisi tukapata mgao.
Kwanza samaki walikuwa ni wakubwa sana. Kuwacharanga ni kama mtu anacharanga ng'ombe. Mapanga na mashoka yanahusika. Sasa ukipewa kipande ni mnofu mtupu. Kipande kikubwa hakina mfupa hata mmoja. Kwa kweli wiki ile tulikula vizuri sana maana waliwapika mfululizo ili wasiharibike.
Uchumi wetu wa bluu ungekuwa sawa tungekuwa tunapiga vitu kama vile. Siyo unakula samaki mara utoe mfupa. Mara unakutana na likichwa lina makorokoro kibao. Harafu kutokana na ukapuku utasikia mtu, "Hujui kula kichwa" makorokoro kibao. Yale matamvua sidhani kama yanaliwa yale!