Wale samaki wa Hayati Magufuli walikuwa watamu sijapata ona

Wakili wa shetani

JF-Expert Member
Nov 22, 2022
1,689
3,264
Habarini. Mnakumbuka samaki aliokamata kutoka kwa wachina waliokuwa wanavua kwenye bahari yetu kwa Magendo? Basi wale samaki waligawiwa kwenye vyuo na mashule mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam. Samaki wale walinikuta nikuchukua diploma ya unesi kwenye chuo fulani jijini Dar. Chuoni pale tulikuwa tunapikiwa chakula na sisi tukapata mgao.

Kwanza samaki walikuwa ni wakubwa sana. Kuwacharanga ni kama mtu anacharanga ng'ombe. Mapanga na mashoka yanahusika. Sasa ukipewa kipande ni mnofu mtupu. Kipande kikubwa hakina mfupa hata mmoja. Kwa kweli wiki ile tulikula vizuri sana maana waliwapika mfululizo ili wasiharibike.

Uchumi wetu wa bluu ungekuwa sawa tungekuwa tunapiga vitu kama vile. Siyo unakula samaki mara utoe mfupa. Mara unakutana na likichwa lina makorokoro kibao. Harafu kutokana na ukapuku utasikia mtu, "Hujui kula kichwa" makorokoro kibao. Yale matamvua sidhani kama yanaliwa yale!
 
Acha uroho....inamaana...tangu umalize chuo..hujala tena samaki.

Kapuku mkubwa
 
🤣🤣🤣 umenikumbusha mbali sana kipindi hicho nipo UDSM kama 2011 au 2012 kama sijakosea walivokamatwa wale samaki bhana weeh nilijua mimi tu nawakumbuka..Sijapata kula samaki watamu kama wale..zile Canteen za udsm huku juu..those beutiful Days daah
 
Habarini. Mnakumbuka samaki aliokamata kutoka kwa wachina waliokuwa wanavua kwenye bahari yetu kwa Magendo? Basi wale samaki waligawiwa kwenye vyuo na mashule mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam. Samaki wale walinikuta nikuchukua diploma ya unesi kwenye chuo fulani jijini Dar. Chuoni pale tulikuwa tunapikiwa chakula na sisi tukapata mgao.

Kwanza samaki walikuwa ni wakubwa sana. Kuwacharanga ni kama mtu anacharanga ng'ombe. Mapanga na mashoka yanahusika. Sasa ukipewa kipande ni mnofu mtupu. Kipande kikubwa hakina mfupa hata mmoja. Kwa kweli wiki ile tulikula vizuri sana maana waliwapika mfululizo ili wasiharibike.

Uchumi wetu wa bluu ungekuwa sawa tungekuwa tunapiga vitu kama vile. Siyo unakula samaki mara utoe mfupa. Mara unakutana na likichwa lina makorokoro kibao. Harafu kutokana na ukapuku utasikia mtu, "Hujui kula kichwa" makorokoro kibao. Yale matamvua sidhani kama yanaliwa yale!
TCU mnaombwa kuongeza viwango vya Ufaulu kwa Universities... kutoka DD mbili hadi CC mbili kama miaka ya nyumA... vijana wengi wanaodahiliwa Vyuo vikuu hawana uwezo wa kuchambua Mambo...
 
Back
Top Bottom