Wale mliofanya harusi ya gharama ndogo ninawaita hapa.

Mi nilifunga ndoa kanisani saa 10 jioni then nikaenda hotelini kupiga picha badae kuanzia saa 12 jioni tafrija ikaanza nyumbani yani wamama wananzengo wakaingia jikoni msosi wa laki sita au saba hata ikija mitaa miwili hawamalizi ...changamoto ipo kwenye vinywaji
 
Chini ya 500k pia inawezekana jombaa
Yeah nalijua hili, nalijifunza kwa rafiki
angu aliyenialika Zanzibar march mwaka huu: tulienda oa alfajiri baada ya ndoa tukala bites kadhaa na nyama tukachukua mke wetu.

Na sio kwamba jamaa ni mnyonge mfukoni
Yupo vizuri tu; kiukweli nilimwambia nami ntaja funga ndoa kama yako hii.

Maswala ya kuwekeza 200m plus kwenye harusi kwa mtu ambaye siku akiamka vibaya anakuambia tuachane nimewaachia wachaga na wahaya.
 
Mm nimefanya mwaka huu, harusi ndogo na gharama nafuu mpaka watu walishangaa, kwanza ni kaweka michango midongo sana kias kwamba kila mtu aliimudu.

PILI sikutaka purukushaniza watu, ni katengeneza kadi 100 tu ambazo waliokuja Kwa waliochukua kadi hawakufika hata nusu ya kadi.

Tatu nikatafuta mpishi a nipigie hesabu ya chakula cha watu 150,pamoja na makolokolo yote yahusio chakula. Sikutaka kuagiza wale ndugu zetu wa sahani moja 15, 000 maaaa ni gharama kubwa sana.

Nne hapa kwenye mavazi, inataka uwe na roho ngumu na msimamo mkubwa sana, maaana wanawake wanajijua wenyewe, hili suala la mavaz nikajaribu kuwaachia ndugu, basi ikawa kila mtu anataka vikolombwezo mbavyo ni gharama. Nilichofanya nikasimamia mwenyewe show.

Tano soda na maji tukae da kufuata wenyewe kwa wateja wa jumla ambao ni bei nafuu sana

Sita tu kaenda sokoni Ilala kuchukua kama, nyanya, matunda, ndizi, viazi, kuku na vitu vingine ambayo ukiwa na 100K tayari mzigo.

Saba tukatafuta mpishi ambaye ametupikia tu, nakumbuka Kwa kazi zote tulimpa 150,000.

Sasa ukipiga hesabu ni hela ndogo sana, lakini Ndio hivyo kila mtu ana uwezo wake
 
Hapana sio hapo ni maeneo fulani Tabata ila muda maana nina mabinti wawili wazuri sana, sina mtoto wa kiume,huyu wa pili anasema nae hataki harusi ya makeke , kaona mkanda wangu wa video.

500k INATOSHA SANA, ila ndani ya 500K uwe tayari una suti yako na wife ana shela na viatu na pia uwe ume andaa usafiri wako ambao utapambwa na sister zako pia andaa usafir wa wakwee hili muhimu sana sana, kwenda na kurudi, Vinginevyo inatosha, Camera ya Video ni elfu hamsini per day kukodi.

Lazima siku ya Harusi rafiki yako wa karibu awe kama coordinator cum floormanager cum MC vinginevyo wife akikubali tu unaoa .

Wakati fulani nilikuwa nina fanya video shooting kama Hobby. Nilipata kazi ya ku record video ya dada mmoja aliolewa na mzungu. aliniambia tumfuate Serena Hotel pale Salon. Kufika pale wala hakupambwa kabisa aliajiangalia kama yuko sawa kwenye kioo na kupaka mafuta kidogo halafu kuna mtu alimletea maua yale ya order, tukapiga picha mbili au tatu akaondoka kueleka ukumbini mikocheni kule, kwenye utoaji wa zawadi alikabidhiwa vyombo vya kunywea chai full set basi. hamna zawadi nyingine. Nilishangaa ilikuwa rahisi kasoro pale serena naona alilipa hela kidogo
 
Huwa ninashangaa tu, watu wanavyoteseka kuchangisha michango ya harusi. Nowdays ukisema unaoa ni full stress. Bwana harusi stress, wazazi stress, marafiki stress, nk. Hii inatokana na mentality waliyo nayo watu wengi kwamba, harusi inahitaji mamilioni ili ifanikiwe. Yaani ukisema harusi watu wanawaza mchango tu. But to me I think different .

Ninapanga kufanya harusi ya gharama ndogo kadri itakavyowezekana. Hii inahusu kuwahusisha watu wa karibu tu ie Wanafamilia pande zote, marafiki wa karibu na viongozi wetu wa dini. Kwangu mimi harusi siyo kitu cha kushadadiiia kivile.

Ninaamini kuna watu walishafanya ninachokiwaza. Tukishare experience siyo vibaya. Ninaombeni fikra zenu hapa, hata kama ni kunipinga kwa hoja its okay. Kuna changamoto gani zinazoweza kunikumba mbeleni katika kutekeleza uamuzi wangu huu? Shukran in advance
Kuoa ni suala binafsi na kifamilia au ukoo. Fanya kulingana na uwezo wa familia aunt upon. Usisumbue watu. Nakuunga mkono mkuu
 
Ni using kuchangisha mil 20 kwa stress na kusumbua watu halafu baada ya harusi unalipa madeni. Harris ni mwanzo wa maisha so mwisho
 
Safi sana. mwenye akili achukue point hapa
sio ubahili ila inategemea unaoa wapi na uko dhehebu au dini gani.

Mimi nilioa katika kanisa la TAG au walokole. Sikuchangisha kabisa. Ila nilitangaza kuwa harusi yangu itafanyika siku fulani, jamaa zangu wa karibu niliwataarifu. Nilikadiria watakuja watu wangapi kula kwenye harusi yangu. Nilitayarisha pesa ya gunia la mchele na mboga ikiwa ni nyama yake na viungo. Kule hamna bia hivyo soda ilikuwa bei rahisi. na maji mengi tu.

Kabla ya hapo nilishona suti na shela la wife siku hizi yanakodishwa na pia nilitayarisha hela za gesti kwa ajili ya honeymoon. na pia inabidi kununua dress nyingine zuri kwa ajili ya wife akivua shela anavaa na viatu safi.
Nilioa kanisani na baada ya ibada watu wakatoka vijana wakageuza viti vikawa vinatazamana chakula kikaletwa kila mtu kashiba.

Ila nilichogundua watu wengi walipoona harusi inakaribia sana na hawaletewi kadi ya mchango waliona aibu kuja kwenye harusi bila kuchanga walichanga wenyewe nikakuta ndizi na kuku na misosi mingine ambayo haikuwepo kwenye bajeti yangu

Keki kama kwaida lazima iwepo.

Video kodisha tu camera inayotumia card baada ya harusi unacheki moja kwa moja kwenye laptop mpe rafiki yako anaejua kutumua ila iwe HD

Ina maana harusi yangu baada tu ya Ibada kuna kupiga picha baada tu ya picha sherehe ya harusi ikaanza na ikaisha kabla ya saa 1 usiku.

Ukitaka kufanya kitu kama hiki usitoe taarifa ya harusi mapema huko ni kuomba mchango. siku chache kabla ya Harusi wambie ndugu na jmaa zako unawaalika kwenye harusi na tafrija fupi basi, tatizo hapa ni wife inabidi akubali hii harusi ya namaa hii
 
Inategemea dini, Dhehebu na kabila lako na mke huyo.

Wadada wengi wanapenda sifa,
Dini ya Kikristo imeingiza mambo ya Kimagaribi sana.

Huwa ninashangaa tu, watu wanavyoteseka kuchangisha michango ya harusi. Nowdays ukisema unaoa ni full stress. Bwana harusi stress, wazazi stress, marafiki stress, nk. Hii inatokana na mentality waliyo nayo watu wengi kwamba, harusi inahitaji mamilioni ili ifanikiwe. Yaani ukisema harusi watu wanawaza mchango tu. But to me I think different .

Ninapanga kufanya harusi ya gharama ndogo kadri itakavyowezekana. Hii inahusu kuwahusisha watu wa karibu tu ie Wanafamilia pande zote, marafiki wa karibu na viongozi wetu wa dini. Kwangu mimi harusi siyo kitu cha kushadadiiia kivile.

Ninaamini kuna watu walishafanya ninachokiwaza. Tukishare experience siyo vibaya. Ninaombeni fikra zenu hapa, hata kama ni kunipinga kwa hoja its okay. Kuna changamoto gani zinazoweza kunikumba mbeleni katika kutekeleza uamuzi wangu huu? Shukran in advance
 
Kuna rafiki yetu aliwahi kwenda kanisani na wadhamini tu, alipotoka wakawa washaandaa hoteli wakalala zao km 3 days walivyotoka kule aliandaa kam milion moja akanunua vinywaji, chakula kikapikwa home akaalika wazaz, ndugu wachache na marafiki watu hawakuamini,anasema jamani siku fulani tulifunga ndoa, picha hizi hapa mtanisamehe,tukamuuliza kwann akasema hakutaka kusumbua watu
 
Yes nipo hapa, niulize chochote. Japo nilifunga mwaka 2016
 
Kuna rafiki yetu aliwahi kwenda kanisani na wadhamini tu, alipotoka wakawa washaandaa hoteli wakalala zao km 3 days walivyotoka kule aliandaa kam milion moja akanunua vinywaji, chakula kikapikwa home akaalika wazaz, ndugu wachache na marafiki watu hawakuamini,anasema jamani siku fulani tulifunga ndoa, picha hizi hapa mtanisamehe,tukamuuliza kwann akasema hakutaka kusumbua watu
Naichukua hii ...
 
Inaonekana suala la kupenda harusi kubwa Hawa wadada ndo wanapenda yani lakini inatakiwa waangalie na hali ya mtu,habar za kupanga sherehe kwa kutegemea michango siyo kabisa ,michango iwe nyongeza tu kwenye budget yenu......
 
Huwa ninashangaa tu, watu wanavyoteseka kuchangisha michango ya harusi. Nowdays ukisema unaoa ni full stress. Bwana harusi stress, wazazi stress, marafiki stress, nk. Hii inatokana na mentality waliyo nayo watu wengi kwamba, harusi inahitaji mamilioni ili ifanikiwe. Yaani ukisema harusi watu wanawaza mchango tu. But to me I think different .

Ninapanga kufanya harusi ya gharama ndogo kadri itakavyowezekana. Hii inahusu kuwahusisha watu wa karibu tu ie Wanafamilia pande zote, marafiki wa karibu na viongozi wetu wa dini. Kwangu mimi harusi siyo kitu cha kushadadiiia kivile.

Ninaamini kuna watu walishafanya ninachokiwaza. Tukishare experience siyo vibaya. Ninaombeni fikra zenu hapa, hata kama ni kunipinga kwa hoja its okay. Kuna changamoto gani zinazoweza kunikumba mbeleni katika kutekeleza uamuzi wangu huu? Shukran in advance
Nilitumia 100000/= nakumbuka ilibaki1800
 
Nimepanga ndoa yangu isizidi dola 45 USD yaani usizidi laki moja ya kitanzania usiniulize kivipi na kwanini!
 
Siku nikioa nitaenda kanisani na wadhamini pamoja na wazazi wa pande zote mbili, baada ya hapo tutarudi kufanya tafrija isiyozidi watu 50
 
Mkuu nilifanya harusi ya watu 100 plus kwa 4milion; vikao viwili tu ndo tulifanya ya kwanza ya ufunguzi na ya pili ya kupeana majukumu
 
Back
Top Bottom