Ushuhuda: Inawezekana kupunguza gharama ya sherehe ya harusi na ikapendeza

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,925
7,952
Nimekuwa nikiona mara kwa mara humu ndani vijana wengi wakilalamika kuhusu costs za sherehe za harusi na kuona kama vile ni kikwazo kwa wao kuweza kuuaga ubachela.

Ninachopenda kuwaambia ni kuwa inawezekana kabisa kufanya sherehe kadri ya uwezo wako wewe,bila kukimbizana na watu kuchangishana au kubaki na madeni lukuki baada ya harusi.

Leo naleta ushuhuda wa harusi yangu binafsi ambayo bajeti ya ile sherehe ilikuwa chini ya 2.3milioni na sikuchangisha hata mia kutoka kwa mtu(huu ndio ulikuwa uwezo wangu mimi na mwenzangu). Hivyo tulihakikisha kuwa bajeti ya kitu tutakachofanya kinaendana na uwezo wetu na si vinginevyo.

Hivyo basi,hata kama huna milioni 2,unaweza kuandaa sherehe hata ya shilingi elfu 70 kama huo ndio uwezo wako. Inawezekana!!!

Maana kuna watu wanaamini kuwa bila milioni 20 au 15 huwezi fanya kitu kizuri. Cha msingi ni kupanga bajeti na kuhakikisha kuwa inaendana na mlicho nacho mfukoni,mnapunguza vitu unnecessary mpaka pale bajeti yenu itakapokuwa ndani ya uwezo wenu!! Niliwahi kuhudhuria harusi ambayo bajeti yake ilikuwa ni shilingi elfu 50.

Bahati nzuri pia, menzangu sio mtu wa kupenda masherehe makubwa makubwa kwa hiyo tulikibaliana vizuri tuu wala hakukuwa na shida.

Hatukutaka kuanza kukimbizana na watu michango ya harusi mpaka iwe kero, au tumalize harusi tuanze maisha na madeni kwa sababu ya sherehe ya masaa machache tuu. Hasa ukizingatia kuwa uwezo wetu kiuchumi ulikuwa ni.mdogo pia. Tulifanya kitu simple sana.

Bajeti ilikuwa kwa watu 60; ambao walikuwa ni ndugu zetu wa karibu ma close friends wachache.

Pesa kubwa ilienda kwenye chakula na vinywaji; ukumbi tulipewa bila kuulipia as i said hoteli ya nemax royal iliyopo kinondoni(kwa sababu vinywaji na msosi tulichukua hapo hapo).

Hakuna cha maids wa bibi harusi zaidi ya matron wa bi harusi na mpambe wangu.

Gharama nyingine ndogo ndogo zilikuwa ni keki,picha,shampeni. Ukumbi walitupangia tuu viti na meza vizuri na high table(no mapambo complicated).

MC akawa dada yangu, na tulitumia Public addressing system ya ukumbi tuka connect our laptop bro akawa DJ.

Mimi binafsi nilipenda sana jinsi ilivyokuwa kiukweli,it was nice and no stress!!! Na,hata waliohudhuria walisema nimefanya,kitu kizuri sana.

Bajeti(kadri ninavyokumbuka)
1.chakula
20,000 @ plate X 60=1200000
2.vinywaji(bei ilikuwa ni moja, Tshs 2,000 kwa bia au soda)
Kwa bia 4 @ 2000X 40=320000(kwa watu wetu tuliowaalika coz ni wa karibu,tunawajua personally,i tulijua wanywaji hawatazidi 40)
Kwa soda 3@ X 2000 X 20=120000
Picha za mnato=140,000
Keki= 250000
Usafiri wa wakwe(tulichukua noah ya mshikaji tukampa 40,000 na kuijaza mafuta)
Gari ya maharusi tulitumia ya sister
Kupambwa bi harusi + kupamba gari ya maharusi 150,000
Champane @ 15,000 X 3=45,000
TOTAL 2,265,000.

FANYA MAMBO KWA KADRI YA KIPATO CHAKO,INAWEZEKANA, IT BEGINS WITH YOU.
Ahsanteni
 
Hongera sana.

Ukweli kinachowaponza wengi ni kuiga, kufuata mkumbo au sijui niseme mashindano.

Kwa kweli Ndoa kwa upande wa Imani yangu(Kidini) ni rahisi sana, na mengi wanayoyafanya baadhi ya watu wa upande wangu ni kukiuka maadili.

Lakini kama kweli Wahusika wakafanya kama vile taratibu za Imani(Kidini) yangu inavyotakiwa, kwa kweli Ndoa haina gharama kabisa
 
shida kubwa ya jamii ya sasa ni ndugu hasa wanawake.
kuna watu wanaanza kulalamika kuwa wanachangia sherehe zingine hivyo nao wanahitaji kuchangiwa.

lakini hapo juu umesahau bajeti ya shela na suti yako na nguo za wapambe pia

Uko sawa kabisa chief; mara,nyingi wanawake ndio hupenda complications aisee..
Na pia hapa nimeongelea cost za SHEREHE tuu!!! Of coz kuna additional costs za mavazi na vitu kama hivyo.
 
Hongera sana.

Ukweli kinachowaponza wengi ni kuiga, kufuata mkumbo au sijui niseme mashindano.

Kwa kweli Ndoa kwa upande wa Imani yangu(Kidini) ni rahisi sana, na mengi wanayoyafanya baadhi ya watu wa upande wangu ni kukiuka maadili.

Lakini kama kweli Wahusika wakafanya kama vile taratibu za Imani(Kidini) yangu inavyotakiwa, kwa kweli Ndoa haina gharama kabisa
Ni kweli kabisa, katika hilo nakuunga mkono kuna ndoa mimi niliwahi kujudhuria bajeti yake ilikuwa elfu 70 tuu!!!
 
Hongera sana. Mie ninachokufurahia ni kuwa mlialika watu walio karibu na nyie na mnaowajua. Bi harusi unaingia ukumbini total strangers, rafiki wa shosti wa nyumba ndogo ya wifi. Zawadi ukisoma card mr and mrs matembele hata hamwajui, unashindwa kuithamini!

Japokuwa kuna familia zina makuu pia. Ukisema hutaki sherehe ya kuchangiwa wanakuona una dharau. Tubadilike na wakati.
 
Kuna mtu alichukua mkopo 15m kwa akaunti ya salary kwa ajili ya harusi!

Maharus walibadili nguo mara tatu
Ya kanisani, ukumbini na nyingine ukumbini!

Analipa deni, nyumba ya kupanga gari la ofc!

Pata picha akifukuzwa kazi huyu! !

Harusi rahisi sana watu wanajichanganya tu
 
Nimekuwa nikiona mara kwa mara humu ndani vijana wengi wakilalamika kuhusu costs za sherehe za harusi na kuona kama vile ni kikwazo kwa wao kuweza kuuaga ubachela.

Ninachopenda kuwaambia ni kuwa inawezekana kabisa kufanya sherehe kadri ya uwezo wako wewe,bila kukimbizana na watu kuchangishana au kubaki na madeni lukuki baada ya harusi.

Leo naleta ushuhuda wa harusi yangu binafsi ambayo bajeti ya ile sherehe ilikuwa chini ya 2.3milioni na sikuchangisha hata mia kutoka kwa mtu(huu ndio ulikuwa uwezo wangu mimi na mwenzangu). Hivyo tulihakikisha kuwa bajeti ya kitu tutakachofanya kinaendana na uwezo wetu na si vinginevyo.

Hivyo basi,hata kama huna milioni 2,unaweza kuandaa sherehe hata ya shilingi elfu 70 kama huo ndio uwezo wako. Inawezekana!!!

Maana kuna watu wanaamini kuwa bila milioni 20 au 15 huwezi fanya kitu kizuri. Cha msingi ni kupanga bajeti na kuhakikisha kuwa inaendana na mlicho nacho mfukoni,mnapunguza vitu unnecessary mpaka pale bajeti yenu itakapokuwa ndani ya uwezo wenu!! Niliwahi kuhudhuria harusi ambayo bajeti yake ilikuwa ni shilingi elfu 50.

Bahati nzuri pia, menzangu sio mtu wa kupenda masherehe makubwa makubwa kwa hiyo tulikibaliana vizuri tuu wala hakukuwa na shida.

Hatukutaka kuanza kukimbizana na watu michango ya harusi mpaka iwe kero, au tumalize harusi tuanze maisha na madeni kwa sababu ya sherehe ya masaa machache tuu. Hasa ukizingatia kuwa uwezo wetu kiuchumi ulikuwa ni.mdogo pia. Tulifanya kitu simple sana.

Bajeti ilikuwa kwa watu 60; ambao walikuwa ni ndugu zetu wa karibu ma close friends wachache.

Pesa kubwa ilienda kwenye chakula na vinywaji; ukumbi tulipewa bila kuulipia as i said hoteli ya nemax royal iliyopo kinondoni(kwa sababu vinywaji na msosi tulichukua hapo hapo).

Hakuna cha maids wa bibi harusi zaidi ya matron wa bi harusi na mpambe wangu.

Gharama nyingine ndogo ndogo zilikuwa ni keki,picha,shampeni. Ukumbi walitupangia tuu viti na meza vizuri na high table(no mapambo complicated).

MC akawa dada yangu, na tulitumia Public addressing system ya ukumbi tuka connect our laptop bro akawa DJ.

Mimi binafsi nilipenda sana jinsi ilivyokuwa kiukweli,it was nice and no stress!!! Na,hata waliohudhuria walisema nimefanya,kitu kizuri sana.

Bajeti(kadri ninavyokumbuka)
1.chakula
20,000 @ plate X 60=1200000
2.vinywaji(bei ilikuwa ni moja, Tshs 2,000 kwa bia au soda)
Kwa bia 4 @ 2000X 40=320000(kwa watu wetu tuliowaalika coz ni wa karibu,tunawajua personally,i tulijua wanywaji hawatazidi 40)
Kwa soda 3@ X 2000 X 20=120000
Picha za mnato=140,000
Keki= 250000
Usafiri wa wakwe(tulichukua noah ya mshikaji tukampa 40,000 na kuijaza mafuta)
Gari ya maharusi tulitumia ya kwangu.
Kupambwa bi harusi + kupamba gari ya maharusi 150,000
Champane @ 15,000 X 3=45,000
TOTAL 2,265,000.

FANYA MAMBO KWA KADRI YA KIPATO CHAKO,INAWEZEKANA, IT BEGINS WITH YOU.
Ahsanteni

Hata mimi ya kwangu sikuchangisha mtu. Kulikuwa na jumla ya watu 50 ndugu na marafiki wa karibu. Tulichanga watu wanne tu mimi , mwenzangu na shemeji zangu wawili. Sherehe ilikuwa nzuri na kuna mtu alikuwa amefunga ndoa one week kabla yangu alikuja akaniambia taabu na shida alizopata kwenye arusi yake ningefunga kabla yake naye angefanya kama niliyofanya mimi. Huwa nashindwa kuelewa watu wanataka kufanya sherehe expensive kuliko uwezo wao.
 
Hongera sana mkuu; unaweza kutupa mchanganuo wa bajeti yako kama unakumbuka? Its good ili tuzidi kuwaonyesha watu kuwa inawezekana
 
Kuna mtu alichukua mkopo 15m kwa akaunti ya salary kwa ajili ya harusi!

Maharus walibadili nguo mara tatu
Ya kanisani, ukumbini na nyingine ukumbini!

Analipa deni, nyumba ya kupanga gari la ofc!

Pata picha akifukuzwa kazi huyu! !

Harusi rahisi sana watu wanajichanganya tu

mi nilishasema siwezi kukopa kwa ajili ya mambo ya kipumbavu.
mkopo wangu ni wa nyumba tu!!
vingine ni juhudi yangu na uwekezaji wangu ndio unanitoa.
 
unfortunately harusi zenyewe zinaisha baada ya mwezi mmoja.
watu wanaamua kufanya vitu ambavyo havidumu.
ndio hawa kila mwaka unakuta, HAPPY ANNIVESARY to us!! mwaka mmoja??
wakati kuna watu wana miaka 30!!!
 
Hahaaa tatizo kubwa ni kushindana na presure kutoka kwa Ndugu, jamaa na marafiki, Ukitazama harusi nyingi sana zimekaa kimashindano na wale sijui wana kamati ndo wanafanya harusi ziwe ngumu make utakuta mwanakamati ana experiance ya 10 years katika hayo maswala so ni full complication.

Hiyo kwanza ni pesa nyingi sana, Kuna jamaa angu alifunga ndoa alitumia laki 3 na nusu, hadi suti aliazima anakumbia hawezi shona suti wakati ataivaa siku moja tu na hataivaa tena, best man wake yeye alivaa ngua za kawaida tu, na baada ya hapo ndugu tena wa kariba kabisa wakapelekwa baa ikachomwa nyama, na vinywaji kazi ikasiha na mpaka sasa maisha yanaendelea.

Tatizo watu hufanya kana kwamba maisha hayapo tena na mbaya zaidi mtu anadiriki kukopa kwa ajili ya harusi
 
Tatizo ni sisi.
Mashoga zangu watanionaje!
Dada zangu nataka wanikome!
Kuna yule binamu nae alijifanya anajua lazima nimkomeshe.
Yaani mambo mengi ambayo katika hali halisi ni ujinga
 
Ni kweli mkuu, uko sawa. Kukopa kwa ajili ya harusi ni ulimbukeni wa kiwango cha juu!!
Complications zisizo na msingi na kupenda mashindano na ufahari tusiouweza ndio tatizo kubwa
 
Tatizo ni sisi.
Mashoga zangu watanionaje!
Dada zangu nataka wanikome!
Kuna yule binamu nae alijifanya anajua lazima nimkomeshe.
Yaani mambo mengi ambayo katika hali halisi ni ujinga
Ni kweli kabisa!! Wadada wengi wana akili fulani hivi za kitoto sana za kupenda mashindano na sifa ambazo kimsingi ni za kijinga! Na hao ndio hulazimisha sherehe ya harusi kuwa na gharama kubwa. Atakwambia anataka shela la milioni; akapambwe kwa laki nane, mara ooohh baby i want our day to be memorable,watu washangae!! Sasa for what??
Mimi namshukuru sana Mungu mwenzangu hana hayo mambo kiukweli.
 
Tatizo wanawake hasa kina mama wanafanya mambo yawe magumu kisa yeye anachangia za watu nae anataka achangiwe..kila siku namdokezaga mama kua harusi yangu mie itakua simple tu hamna hata haja ya ukumbini ila hua anapinga kabisa hadi tuna nuniana kabisa
 
Back
Top Bottom