Wale MAFISADI wa elimu mbona hawajajisafisha, wanapeta tu na wengine ni mawaziri

Lyimo

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,826
2,017
Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi nchini Ujerumani Bw. zu Guttenberg amewajibika kwa kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kubainika sehemu kubwa ya degree yake ya filosofia (uzamivu) alinakili kwa wengine bila kuwataja (Plagiarisim).
Habari zaidi BBC News - German Defence Minister Guttenberg resigns over thesis

Hapa Tanzania kunamalalamiko ya viongozi wetu kadhaa kuwa taaluma zao si za kiuhalali na hivyo kupewa majukumu mazito kulingana na taaluma hizo. Hawa walibainishwa kama MAFISADI WA ELIMU na Bw. Kainerugaba Msemakweli ambaye aliandika kitabu kuhusiana, ila nNi mawaziri wawili tu kwa kumbukumbu zangu (Mbunge wa Ukonga) Bw. Makongoro na Diallo walifungua kesi lakini wanazikimbia, na karibuni zitafutwa. Wengine hawakujitokeza hata kujisingizia kukanusha. Kwanini watanzania hatulipigii kelele hili, inawezekana aina hii ya ufisadi ni kikwazo katika maendeleo ya nchi yetu. Na pia inachochea wengine kutafuta njia za mkato kama hizi. Nawakilisha.
 
kuna mifumo kweli imekaa vizuri yaani plagiarism tu inamchomoa mtu kwenye cheo chake.
Bongo ni PhD feki na bado ni viongozi wetu.
 
Hiyo ndo nchi yetu bwana... Nadhani kunahitajika mdahalo huru, ili huyo anaewateua aulizwe maswali hayo. Aibu.... Vigezo vya Uwaziri Tanganyika ni ushemeji, ukwe, ushenga, ukuwadi, ukimada na mengine kama hayo!
 
Nchi imeuzwa viongozi wengi wameghushi phd hata vyeti lakin wanaongoza wizara wanatoka wanarudi hakuna sheria ya kuwaengua?
 
Back
Top Bottom