Wakuu, waziri Sitta ananichanganya kuhusu Richmond. Ukweli ni upi?

Mpui Lyazumbi

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
1,856
371
Heshima mbele watanzania. Katika kibwagizo cha kile kipindi cha dakika45 kinachorushwa na itv, waziri sitta anatupiwa swali na uchokozi kuhusu msimamo wake kwenye swala la Richmond. Bila kumumunya maneno anabainisha kuwa Richmond ni kikundi cha "wahuni" wachache na hivyo si haki wala wajibu wa watanzania kulipa deni/tozo yoyote. Hayo nimeyaona kwenye kibwagizo kunachoashiria kuwa kipindi hicho kitarushwa ama leo(jumatatu) au jumatatu yoyote saa 3 usiku. Anaponichanganya ni hapa:-
  • Kwenye ile ripoti ni kipi kilisalia anachokijua yeye?
  • Kama ni kikundi cha wahuni ni kwa nini tulitumia nguvu nyingi na kodi zetu kwenye swala la "wahuni".
  • Wakati ule alishindwa nini kusimamia haki na wajibu wa watanzania kwenye sakata hili.
  • Anashindwa nini kuweka ukweli bayana, na swala hili liishe ili tuanze ukurasa upya.
  • ....
  • .......aaagrr
 
Mimi namwelewa Mhe. Sitta kabisa kwamba Dowans iliyorithi Richmond ni uendelezo wa mafisadi wa hapa hapa nchini waliounda kampuni hewa na kuingiza mitambo ya umeme. Historia ya suala hili imedhihirisha kwamba ni kwa matumizi ya fedha zetu WaTz zilizokwapuliwa toka EPA ya Benki Kuu, zikatumika kununua hii mitambo. Nyingine zilipelekwa Kagoda Agriculture.

Kinara wa hawa mafisadi, Rostam ametajwa mara nyingi na alihusika kusaji kapuni huko Costa Ricca etc etc.

WaTz. sasa wanapinga kwamba hizi kampuni feki zisilipwe hii tozo. Mhe. Sitta ana uchungu na fedha za umma kutumika kulipia tozo iliyotokana na utapeli.
 
Kuna vitu unavionyesha, lakini kama hayo yanajulikana na 6, kwa nini haijibu wasiwasi wangu hapo juu?
 
Kipindi kitarushwa leo saa 3usiku. Hii ni mjibu wa taarifa ya habari ya sasa hivi ya itv. Inaonyesha mzee sitta anayo mengi. Naomba tufuatilie kipindi hicho wote tupeane taarifa vizuri. Hapa nilipo nina wasiwasi na mgao wa umeme.
 
Waziri wa EA Samweli sita atanguruma kwenye kipindi cha dak 45.
Sita ataelezea juu ya malipo ya Dowans .
Source Itv habari.
 
Nimeona vema nikidokeza hili kwa wana jamvi

Nasikiliza taharifa ya habari ITV wamegusia kuwa saa tatu waziri wa east africa Sitta atahojiwa(kihalisia kipindi kitarushwa maana kimesharekodiwa) na jamaa wa ITV kwenye kile kipindi cha dakika 45 .
jambo ambalo limeonjeshwa kwa ufupi ni kuhusu dowans.
 
Dowans lyrics have turned hackneyed among many Tanzanians ears. We need new songs!
 
Ndugu zangu wahi ITV saa 3.00 usiku huu kumsikiliza mh. Samwel Sitta katika kipindi cha dakika 45. Pamoja na mambo mengine atazungumzia ule anaouita msimamo wake juu ya malipo ya Dowans. Ninachojiuliza hivi hivi huu ni ukweli kutoka ndani ya moyo wake, naomba tuyachambue, nawasilisha.
 
Nimejipanga kumsikiliza mara ghafla TANESCO wamefanya mambo yao kama kawa, sijui ntamsikilizaje huyu mwanasheria asiyefuata sheria.

Waziri wa EA Samweli sita atanguruma kwenye kipindi cha dak 45.
Sita ataelezea juu ya malipo ya Dowans .
Source Itv habari.
 
Mods unganisheni uzi huu na ule niliyoanzisha maana maudhui ni yaleyale. Tafadhali!
 
Hi MWITA! Tanzanians will NEVER rest until the culprits of Dowans are brought before the justice¬ WImbo ndo unogire.
Dowans lyrics have turned hackneyed among many Tanzanians ears. We need new songs!
 
Hujuma hawa tanesco! na kwetu pia wamekata! nchi nzima. wanamchi hawatakiwi kuujuwa ukweli!
 
Back
Top Bottom