Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 233
- 563
Kama mdau wa Elimu na maendeleo ya kijamii, taarifa za wakuu wa shule kumchangia Mama Samia fedha za kuchukua fomu ya Urais kabla ya mchakato husika kuanza linaleta ukakasi na maswali mengi juu ya uwezo wa kupambanua mambo wa hawa viongozi walioaminiwa kusimamia elimu ya watoto wetu.
Je, kiongozi wa umma anaruhusiwa kuonyesha msimamo wake wa kisiasa hadharani?
Je, wamejuaje kama Rais Samia atagombea 2025?
Je, wana uhakika gani chama chake kitampitisha?
Kulikuwa na haraka gani kufikia hili azimio kipindi hiki ambacho hata mchakato haujaanza?
Tuamini kuwa hili nalo ni sehemu ya kujipendekeza? Kama ni kujipendekeza, wanawezaje kupandikiza ujasiri na kujiamini kwa walimu wanaowasimamia na watoto wetu?