Wakuu Msaada kila nikienda Makao makuu ya Kampuni Fulani

Good People

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
945
1,817
Wakuu katika Kutafuta kazi nimeenda Makao makuu ya Organizations nyingi ambayo yako Dar es Salaam imekua kama kazi bure wakuu

Nimeenda Ofisi moja nikamuulizia HR nikaambiwa una appointment naye? daah nikasema ndiyo akaniambia haya nimwambie nani anamuita nikamwanbia yule Dada akasema sorry huwezi kumuona.

Nikaenda Ofisi nyingine nayo hivyo hivyo tena nilisema sina appointment naye akasema huwezi kumuona nikawa mkweli nikasema Dada mimi natafuta kazi akasema Kaka wamekuja wengi naona hautapata

Hii technique imesha fail wakuu nikienda kwenye Branch naambiwa Hawana mamlaka ya Kuajiri naombeni msaada wakuu!
 
Kwetu hawapokei cv wala kumuona hr.... Yupo busy na cv ni mpaka matangazo ya kazi yabandikwe magazetini na uapply online
 
Nani anatafuta kazi kizamani hivyo chukua laptop yako weka bundle cheki zoom na tayoa online omba kazi aiseee...
Ni Rahisi sana kuhara kwenye huu Uzi maombi yaliyoombwa humu katika Email yangu ni mengi mpaka najiuliza kama huwa wanasoma kweli ndo nikaamua Ku change approach na kuwafata japo kuna ugumu.
 
Ni Rahisi sana kuhara kwenye huu Uzi maombi yaliyoombwa humu katika Email yangu ni mengi mpaka najiuliza kama huwa wanasoma kweli ndo nikaamua Ku change approach na kuwafata japo kuna ugumu.
Mkuu kuna sehemu tu utakua unakosea either cover letter mbovu na cv ni mbovu..mimi nishawahi itwa kazi sehemu ambazo sijawahi tarajia ingawa sikupata hizo kazi na hii yote ni kwenye hayo hayo mambo ya zoom mkuu..nishawahi omba kazi qualification ni masters na mimi sina,ila niliitwa ingawa sikuipata...amini nakwambia
 
Kazi kupata kazi na ni kazi kuacha kazi,acha kazi uone kazi kumuona HR,tafuta mbinu mbadala ndugu jua linawaka mpaka mifukoni.
 
ingia web yao,andika email,itamfikia muhusika moja kwa moja,tatizo mna smartphone mnatumia kwa whatsapp na jf tuu,this is an information age,mtandao ndio kila kitu,search job kwenye cm yako
 
ingia web yao,andika email,itamfikia muhusika moja kwa moja,tatizo mna smartphone mnatumia kwa whatsapp na jf tuu,this is an information age,mtandao ndio kila kitu,search job kwenye cm yako
simply tu !!shm
 
Usihangaike na ma secretary uchwara. Ingia online apply uta save time, costless, accuracy, professional and fast.
 
Back
Top Bottom