Wakurugenzi wa CRDB Bank na NMB Bank wawekeeni mitego ya rushwa ma Afisa Mikopo wenu wanasumbua sana

Alikaeli

Senior Member
Jul 30, 2016
169
193
Niwaombe wakurugenzi wa Benki ya CRDB na NMB wawekeeni ma afisa mikopo wenu mitego ya Rushwa maana wanasumbua sana, wekeni katika Wilaya zote na Branch zote nchi nzima, nilifikiri ni peke yangu nahitaji mkopo halafu nazungushwa kama vile napewa hela ya bure au ni msaada.

Niliomba Mkopo CRDB Bank tawi la () wamenisumbua mno utafikiri hawajui kazi kumbe wanajua wanacho kifanya, nikaenda NMB tawi la () hivyo hivyo nikamtamkia nitampa chake ghafla akanambia mkopo utatoka ndani ya siku 3 hapo nikiwa tayari ni miezi 3 toka nimekamilisha taratibu zote kama mtumishi wa umma.

sitotaja Tawi wala Mkoa ila Wakurugenzi wa mabenki haya wakiweka mtego watabaini matawi ambayo yana mchezo huu, ni meongea na wenzangu wa 3 wote wamepitia haya sasa naomba wakurugenzi fanyeni hima kumaliza tatizo hili ni kero mno.

PS. Waangalie ma file ambayo ni ya maombi yamekaa mezani kwao zaidi ya wiki 2 kuendelea wawaulize kwann yapo huku yakiwa yamesha kamilisha taratibu zote, watakua a kigugumizi ndio hao hao.
 
watumishi wa uma mnaonewa sana sababu hamjui kukaza..

yaani mkopo naokatwa kwenye mshahara wangu uniombe rushwa.. na nikupe kama utanisaidia kulipa...
 
Safi sana ewe afisa mikopo, weka faili pembeni hata miezi nane ikibidi. Baadhi yenu watumishi wa Serikali mnajifanyaga Miungu watu sana kwa kutuzungusha wananchi tunapoenda kufata huduma maofisini kwenu, tena mnatulipisha mpaka pesa ya maziwa eti kisa stoo ilipo faili yangu pamejaa vumbi!!!

Sasa leo mbwa kala mbwa.

Afisa mkopo zungusha hio mutu, piga danadana mpaka ilie meeeee,,, kama mbuzi!!!!!
 
Bora wa Bank hizi nyingine wanakua faster kukufuatilia mkopo hadi unaona aibu ukizipata kutotoa tip ila kwa huduma za kulegea alafu uniombe rushwa nakupa za moto
 
Niliomba Mkopo CRDB Bank tawi la () wamenisumbua mno utafikiri hawajui kazi kumbe wanajua wanacho kifanya, nikaenda NMB tawi la () hivyo hivyo nikamtamkia nitampa chake ghafla akanambia mkopo utatoka ndani ya siku 3 hapo nikiwa tayari ni miezi 3 toka nimekamilisha taratibu zote kama mtumishi wa umma.
CRDB ya kweli haya ?
 
Ubaya hawawezi kufanya hivo wataidhalilisha bank yao na itaingia katika mdororo wa aina flan hawata aminika tena.kwasababu itakuwa publicity tyr kila kona itajulikana kama maafisa wa crdb amekamatwa na rushwa.kwaio mkuu wee hangaika nao tu hivo hivo.
 
watumishi wa uma mnaonewa sana sababu hamjui kukaza..

yaani mkopo naokatwa kwenye mshahara wangu uniombe rushwa.. na nikupe kama utanisaidia kulipa...
Basi Kama hutaki,sio lazima,kwani Nani mwenye shida?
 
Ukiona unatoa rushwa.. jua una kona kona kwenye utaratibu...kama umenyooka huitaji kumsujudia mtu
Mimi sipendi rushwa Sana,,ila sioni ubaya wa takrima,,maisha menyewe haya,yamejaa Kona Kona nyingi
 
Back
Top Bottom