Wakulima wa kilimo cha mahindi piteni hapa tafadhali

Wakuu kheri ya mwaka mpya kwenu nyote, natumai mko poa. Hongereni pia kwa mapambano ya kilimo.

Wakuu nahitaji muongozo kadhaa kuhusu kilimo Cha mahindi. Nahitaji kwenda kufanya kilimo cha mahindi mkoani Morogoro. Nina ndugu yangu huko nae anajihusisha na kilimo katika kuwasiliana nae alinieleza kuwa kule hupanda mahindi mara mbili kwa mwaka katika nyakati tofauti. Ile ya kwanza ilinipita sasa nataka niende hii ya pili ambayo katika maelezo yake ni mwezi wa pili baada ya mavuno ya kwanza.

Nondo ninazo taka kujua ni kama ifuatavyo, kwanza kabisa kwa wale wanao fanya kilimo cha mahindi mkoani Morogoro huo muda nimeambiwa ni sahihi? Yaani kwa mwezi huu wa kwanza ni kuandaa shamba kisha mwezi wa pili ni kupanda na vipi kuhusu mvua kwa kipindi hicho huwa zipo kweli?

Nahitaji kwenda kufanya kilimo cha utaalamu zaidi maana kule wanafanya kienyeji tu sasa mimi naenda kivingine. Kwa maana hiyo napenda kujua ni mbegu aina ipi inakubali na kuzaa kwa wingi ukanda huo? Kwenye heka moja nitahitaji kuwa na mbegu kiasi gani kwa kilogram maana nitanunua zile zilizo kwenye pakti. Kwenye shimo niweke mbegu ngapi na kila umbali wa shimo na shimo uwe urefu upi?

Baada ya kupanda nisubili muda kiasi gani mpaka napiga palizi ya kwanza, hapo hapo baada ya kulima nisubili pia muda gani kwa kupiga madawa? Kule hawatumii mbolea ila mimi nataka nikatumie, mbolea kama DAP, CAN na UREA niweke muda gani kwa kila aina ya mbolea na kwa kila heka nitumie kiasi gani kwa kilogram? Madawa nitumie aina zipi kwa kila hatua itapendeza zaidi mkinitajia majina ya hizo dawa. Yapo mengi ya kuuliza nadhani tuta kuwa tunajulishana hapo chini kwenye reply.

Nisiwachoshe wakuu lengo kuu nahitaji kuingia na kufanya kilimo cha mahindi. Mimi sijawahi jihusisha na kilimo hicho ndio maana nimekuja hapa kuomba muongozo sahihi. Natambua kuwa katika jukwaa hili kuna wakulima wakubwa na wataalamu katika kilimo hichi cha mahindi hivyo napenda kupata muongozo sahihi kutoka kwenu.

Karibuni sana, niko hapa.
Miongoni mwa miradi ya serikali usikute,

Maendeleo yapo kasi sana
 
Kujazia kidgo. M mzawa wa Ruvuma. Kule kuvuna uhakika, mvua ya kutosha karibu Kila mwaka ila kulima n msimu mmoja tu. Risk ya mahindi ni bei, kuombea Bei tu iwe vizuri. Now Niko morogoro.

Habari mkuu,kati ya watu ambao nimetokea kujua kwamba wanapenda kilimo wewe ni mmoja wapo.
Hakuna thread ya kilimo itapita hapa bila kuchangia,nakushauri muulize uyo jamaa yako yuko wilaya gani hapo morogoro? maana kilimo tunachofanya sisi cha kujitafuta kinataka mvua za uhakika sio za kukadilia.Nakushauri fanya utafiti wa eneo hilo je kuna mvua za kutosha?
Pia kama una dreams kubwa za kufanya kilimo kizuri tafuta maeneo mazuri ambayo kilimo cha mahindi kinafanyika kwa uzuri na kuna mvua za kutosha E.g Rukwa,Katavi,Ruvuma nk.
Asante mkuu yangu ni hayo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom