Ninawafahamu watu wema na wabaya wengine Wakristo na wengine Waislamu. Ninawajua watu wenye akili nyingi na nzuri sana kutoka dini hizi mbili. Wapo warembo na watanashati wenye mvuto, Wakristo kwa Waislamu. Binafsi nina marafiki wengi kutoka kila upande. Japo nimelelewa katika familia ya kikristo sana, mchumba wangu ni muislamu mzuri.
Nimetembea pande zote za nchi hii nimeona matajiri na maskini katika kila mkoa na kila wilaya, waislamu kwa wakristo. Nimesoma shule na vyuo mbalimbali Tanzania nimeona vijana wakristo kwa waislamu wakipasi ama wakifeli. Nimewaona wahuni, majambazi sugu, matapeli, wakware na ma-masters, waliobobea wakiitwa John na wengine Hamisi. Kati ya makahaba wakubwa wa nchi hii, wapo akina Asha na akina Joyce pia.
Nimechukizwa na mila na desturi mbaya za baadhi ya waislamu na wakristo vile vile. Nimefurahishwa na ukarimu na upendo wa waislamu na wakristo kila nilipopita. Ninavutiwa na viongozi shupavu wa nchi hii, kama Nyerere na Karume. Mafisadi wakubwa wa nchii yetu, wawe papa au nyangumi wengine ni Wakristo na wengine ni Waislamu. Wapo watu nchi hii hawafanyi kitu bila ushirikina ilhali wakidai kwamba wao ni wailslamu na wengine ni wakristo.
Nimeshuhudia viongozi wengi wa dini wakiwaongoza watu kwenye ukweli na wengine wakiwa kikwazo kwa waumini wao, makanisani na misikitini.
Nakumbuka nilipougua wakati fulani walikuja kunifariji waislamu na wakristo.
Kati ya mkristo na muislamu hakuna bora zaidi ya mwingine. Kama ni hali duni kimaisha hili ni tatizo kwa wote. Nimesaidia ombaomba wengi wakristo kwa waislamu. Kama ni kuporwa rasilimali zetu sote tunaibiwa bila kujali imani zetu. Kama ni kufa kwa magonjwa yanayotibika hili linawakumba wote. Malaria inaua Kaskazini Unguja, malaria inaua Kilimanjaro. Kama ni kudharauliwa na wageni tunaowamilikisha rasilimali zetu nimeona waislamu kwa wakristo wakidharauliwa na hata kuuwawa.
Sote tunahitaji kujinasua kutoka katika umaskini, ujinga na maradhi. Hawa ndio maadui zetu wakubwa. Waswahili wanasema usilaumu ulipoangukia laumu ulipojikwaa. Wengi wetu tumejikwaa katika ujinga tukaangukia kwenye umaskini na maradhi. Chanzo cha umaskini na maradhi yetu sio dini ya mwenzetu au hata si dini zetu wenyewe. Tatizo ni ujinga wetu.
Katika maisha yangu nimeona wakristo wajinga, nimeona waislamu wajinga.
Tuache fitina na majungu kati yetu, tuache kudharauliana na kuchukiana, kufanya hivyo tunampa adui yetu nguvu, badala yake tushirikiane bega kwa bega, tupendane na kusaidiana, na dini zetu zitusaidie kuona kwamba sisi ni watoto wa Baba Mmoja ambaye naamini hafurahii hata kuona tukijiita Wakristo ama Waislamu bali anapenda kutuona tukishirikiana kama ndugu!