Wako wapi wale waliokuwa wanajipangia mshahara wakiona wanakaribia kumaliza chuo

Amos David Mathias

JF-Expert Member
Sep 3, 2022
1,574
3,038
Maisha ni mwalimu mzuri.Kuna Ile tabia mtu anakaribia kumaliza chuo au anakuwa amemaliza kabisa chuo anakuwa anapanga kabisa kwamba Mimi nikienda mtaani sifanyi kazi chini ya hela kiasi Fulani.

Watu wanajipangia mishara mikubwa sana na kujiaminisha.Wakija kuingia na mtaani Kwanza wanakutana na ukosefu wa ajira, kwahiyo wanabaki kusugua benchi nyumbani.Baadaye mtu ana learn the hard way.Na mwisho wa siku akipata hata tenda ya Kiasi kadhaa(kidogo) unakuta anakimbilia haraka Sana na kuona hili nalo embe dodo mchangani.

Achaneni kabisa.
 
Ukute mmekua madalali viwanja goba na kigamboni🤣🤣
Baada ya kumaliza mmoja akawa anatembeza mashuka na vipodozi vya oriflame, ila Mungu alimkumbuka yuko NSSF, mwingine akawa sales wa kampuni ya sigara ila maisha yakawa sio akaacha now ni dalali, mwingine akawa bank teller, mshahara haukuwa unafika hata milioni, wengine hata sijui walipo. Mimi sasa ... hebu nisimalizie kusema.
 
Baada ya kumaliza mmoja akawa anatembeza mashuka na vipodozi vya oriflame, ila Mungu alimkumbuka yuko NSSF, mwingine akawa sales wa kampuni ya sigara ila maisha yakawa sio akaacha now ni dalali, mwingine akawa bank teller, mshahara haukuwa unafika hata milioni, wengine hata sijui walipo. Mimi sasa ... hebu nisimalizie kusema.

Yote maisha mkuu kazi ziendelee 😁
 
Mimi hata sielewi imekua kuaje mpaka nimejikuta ni dereva tax nyie maisha yasikie tu

Wale wanangu hata sijui walipo sasa na matumaini yote tuliokuwa tunapeana imekuwa tofauti kabisa.

Unazingua mtaani unakutana na msoto wa kiwango cha lami, mpaka sipati majibu
 
🫢 maisha kweli ni mwalimu kabisa. Watu kwa sasa wanaitafuta kazi ya laki moja. Si mamilioni kama walivyokuwa wakiwaza.
 
Mishahara haikuwa kama wengi walivyotamani ila namshukuru Mungu wanangu wote walikuwa ni mahustlers na ni kipindi ambapo ajira zilikuwa nje ila uamuzi wa kukataa tulikuwa nao , thanks lord wanangu wote wapo maeneo ya ndoto zao kwa kiasi kikubwa wanapiganisha ila mishahara tulidanganyana sana yaani .

Hivi kweli serikali yakumlipa mtu laki nne naye ukoo mzima unajua ameajiriwa ?
God have mercy , maisha ni tafsiri fichike sana .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom