Wakili Msomi Mwabukusi; Je, ndiye 'Daudi' wa Tanzania au tumtazamie mwingine?

Kwani maana ya kuishauri Serikali nini ?

Au unamaanisha kila anachoamua Raisi Bunge letu linakubali.

Basi hakuna haja ya kuwa na Bunge.

Raisi anatosha.
Bunge Livunjwe.
Viini macho hivyo ... Bunge lina wajumbe 393 ambao wote ni matokeo ya mbeleko za ccm isipokuwa mmoja wa upinzani!
Hapo common wananchi hasa bibi na babu zetu ndo wanarubuniwa!!
 
Nimeona Uturuki Kuna Bandari wamiingia Ubia na DP W Kwa mgao wa asilimia 52 Kwa 48 sio sawa na huu wa Mama
Nahuhakika mkataba wetu ilikuwa na jambo la Siri Sana ndiyo maana tukaanza kuona akina Abduli wanaenda Kwa Mu7 kuuza Ummeme Sola
Haya mambo yatakuja kujulikana tu
Kitenge na New modell Prado
Masikini akipata matako hulia mbwata walio andika methali sio wajinga tutajua tu nawatu wataabika mchana kweupeee
Makuwadi waliiba mchongo mzima wakibakia kuwasinginzia DP World!
Sina uhakika sana kama ule mkataba ulitokea Dubai Emirates!
Kama ndiyo basi DP World wana dharau sana!
 
Nasikitika sana kuhusu Bunge letu.
Yani Bunge limebaki kuitikia tu kila kinacholetwa na Serikali.

Leo hii tunawategemea watu binafsi kuliokoa Taifa letu dhidi ya uvamizi wa maharamia wanaokuja na vazi la kondoo.

Leo hii tunawategeme viongozi wachache wa Dini kufanya kazi ya Bunge.

Hivi Wabunge wote kweli hawakuliona hili?
Yaani Bandari zote za Bahari, Mito na Maziwa kamiliki kakampuni kamoja ka huko Dubai kweli ?

Kampuni ambayo tunaweza kuiajiri na tukailipa.
Hili Bunge tutaliamini vipi tena kesho ?

Binafsi nawashukuru sana SHURA YA MAIMAMU TANZANIA na BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA kwa kusimamia kidete bila kupepesa macho na kulitetea Taifa letu kwa jasho na Damu.

Kama Mlinzi wetu Mkuu anakavulia madaraka yake kakampuni ka mji wa Dubai hakika ametukosea sana.

Tulimwamini sana na kumtegemea bila wasi wasi.
Sasa hivi tuna wasiwasi mkubwa sana na vyombo vyetu vya ulinzi wa raslimali zetu.
tuna wawakilishi wa hovyo katika historia ya Tz toka tupate uhuru!
Sidhani kama aina hii ya uongozi itakuja tena kutokea huko mbeleni
 
Ndiyo maana tunawatamani Gabon
Lakini ni suala la muda tu Mkuu.
Maana hata Wagaboni wenyewe walivumilia kwa karibu miaka 60, wakachoka!
Ngoja na sisi wa kwetu waendelee kujisahau, Siku tukio likipigwa, watashangaa kuona hadi wagonjwa kwenye mawodi wanaahirisha kuugua kwa muda na kuingia mitaani/barabarani kusherehekea kama ilivyokuwa huko Gabon.
 
Kwa msiomjua, Wakili Mwabukusi anatoka ukoo wa Kichifu, kwa hiyo uongozi uko kwenye damu.
 
Siyo mnakuwa na kiongozi ambaye hata kabla hajaanza kuhutubia, unahisi usingizi kwa sababu ya kuboreka na hotuba zisizo na mvuto hata kidogo!
 
We want charismatic leaders like Advocate Mwabukusi, the Late JPM, the late Mwl. JKN and the like.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom