Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,899
- 3,201
Nawasalimu kwa jina la Bwana.
Leo nimekumbuka kisa kilichoandikwa kwenye Biblia, 1 Samweli 17.
Sura hii kwa ufupi inahusu kisa cha kijana mdogo Daudi na Goliathi. Daudi alikuwa ni mchunga kondoo ambaye hakuwa na uzoefu katika masuala ya vita ilhali Goliathi alikuwa ni mpiganaji mwenye uzoefu wa muda mrefu jeshini. Sifa za Goliathi na umbile lake la kutisha liliwaogopesha sana wanajeshi wa Kiisraeli ambao walikimbia kila shujaa huyo alipoinuka kuwatukana na hakuna aliyethubutu kwenda kupambana naye.
Hata Mfalme Sauli (kiongozi wa Israeli wakati huo) mwenyewe, alimwogopa sana. Kwa bahati mbaya alikuwa ameshavunja mahusiano yake na Mungu wa Mbinguni ambaye alikuwa akilipigania Taifa hilo dhidi ya maadui zao.
Ndipo katika hali ya kukata tamaa huko, akaibuka kijana Daudi na kujitolea kwenda kupambana na hilo jitu la kutisha Goliathi.
Mungu mwema, kupitia kwa kijana ambaye hakuwa na uzoefu wa kivita, wala hakuwa maarufu kwa watu, wala hata hakuwa na zana bora za kivita, aliweza kumwua Goliathi kwa kutumia kombeo (manati) na jiwe!
Vivyo hivyo, kwa hali inayoendelea hapa kwetu, ni kana kwamba tunakabiliana na Goliathi, ambaye kila mmoja anamwogopa.
Lakini kaibuka Wakili Msomi Mwabukusi kuhakikisha raslimali za nchi na wananchi vinalindwa dhidi ya mikataba ya hovyo.
Nimalizie kwa kumwombea shujaa wetu huyu, Mungu ambariki sana, yeye na familia yake pamoja na ukoo wake wote kwa ujumla. Mungu wetu amjalie kuwa kiongozi mkubwa kabisa wa nchi yetu kwa maana anastahili. Mungu azidi kumjalia hekima na busara za kuendelea kutututetea Wananchi pamoja na rasilimali zetu. Zaidi ya yote, Mungu amlinde na kumtunza shujaa wetu huyu dhidi ya kila baya kama alivyomtunza Mfalme Daudi. Wote watakaoinuka kinyume cha Wakili Msomi Mwabukusi, walaaniwe wao pamoja na vizazi vyao.
AMIN.