Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala(PhD) aitwa Polisi kutokana na maoni yake kuhusu bandari

Hii safi sana, maana kuna watu wanasambaza uongo, inatakiwa upelelezi chunguze namba zote wanazowasiliana nazo kwa simu na kwa messgaes. Vyanzo vitajulikana tu.

Hii ni vita ya kiuchumi kwa nchi yetu. Aidha watangazie waende wenyewe kwenye vyombo vya uchunguzi au waitwe namna hii.

Nashauri watazamwe ma group yao yote ya wharsapp, telegram, twitter, facebook na jadhalika. Ili vyanzo vijulikane.

Mimi nakisia. vyanzo vya haraka haraka:

1) Anna Tibaijuka.
2) karamagi
3) Adani
4) AD Ports
5) DP World
6) Wakurugenzi waliovunjiwa bodi yao bandarini.
9) Wakurugenzi wa shirika la meli lilitojajwa namba moja.
10) Taasisi za kidini.
11) Sukuma gang
12) Vyama vya siasa ikiwemo CCM yenyewe.

Naamini wengi humu JF ni makondoo tu yaliyokosa mchungaji. Vyanzo vitajulikana tu.

nawapa pongezi sana serikali kwa kuanza kuchukuwa hatua. Maana uongo ukizidi utaonekana ni ukweli.
Baada ya kuuza Bandari za Tanganyika kwa Waarabu mmeanza kusema ni vita ya Kiuchumi.
 
Waandishi wa habari huru, wenye youtube channels zao.

Waitwe mmoja mmoja na kujieleza ni nani anawalipa.

Simu na mawasiliano yao yachunguzwe kwa kina. Naamini serikali inaweza kufanya uchunguzi mzuri na wa haraka na unaofata sheria.
Ooh 'tunatanka' demokrasia huku unabinua pua juu. Ooh magu aliminya demokrasia. Demokrasia ndio hiyo acha watu waongee
 
Nidhamu ya uwoga ilitengenezwa back in the day na Nyerere himself , hata alipoondoka madarakani alitoa kauli za kukemea hiki kitu.
Miaka ya hapa kati imekuwa branded, inaitwa uzalendo na wanasiasa.

Hii kitu ndio imetengeneza kizazi cha hovyo
Yeye mwenyewe Nyerere hakuvumilia ukosoaji, hata Ccm yake aliyoirithisha nchi imeiga kutoka kwake.
 
Hawa watu wanabadilisha watu neutral kwenda nao against...

Why kutumia nguvu Kiasi hiki

Mimi kama mtanzania naona ifike wakati sasa sio tuangalie tu huu Mkataba bali kuhakikisha kwamba mikataba yote kuanzia huu wa sasa na ijayo yote inakuwa wazi (Transparency)
Hawa watu sio wakuwaamini tena waondolewe kwanguvu kwenye office za umma wakauze baa.
 
Barua hiyo ya wito kutoka ofisi ya DCI inamtaka Dkt. Nshala kufika kwa ajili ya mahojiano


Ofisi hii inafanya uchunguzi kuhusiana na kauli ulizotoa tarehe 03 Julai 2023 na kisha kusambazwa katika vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam

Ili tuwe kukamilisha uchunguzi wetu, ofisi hii inakutaka ufike ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Kanda Maalum Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2023 saa 09:00 asubuhi bila kukosa kwa ajili ya mahojiano.




Pia soma:
Rugemeleza Nshala: Tutafungua Kesi kupinga Mkataba wa DP World na Tanzania
Dkt. Rugemeleza Nshala: Nimetishiwa maisha baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World
Kuna wale wa ndege, wapo wale wa ripoti ya CAG pia wapo wale wa hazina wakti wenzao wapo Mei Mosi wao wakawa wanazikwapua hatujasikia DCI akiwaaita hadharani, pia yupo Jussa na Ali Karume hatujawasikia wakiitwa kujieleza. Haya bana haya yana mwisho lakini. Mwisho wa yote sote tutabaki raia wa kawaida.
 
Wamefanya vizuri tena sana, watu wachache hawawezi kusambaza chuki, kuleta mgawanyiko wa nchi kwa sababu zao binafsi. Zile siyo lugha ya mtu mwenye akili timamu kwanza apimwe akili. Utafikiri hajalelewa na wazazi, huwezi kumtukana mwanamke mtu mzima kiasi kile achilia mbali ndiyo eais wa nchi yetu. Vyombo vya ulinzi na usalama visicheke na watu km hao hata kidogo. Bado yule mnyakyusa Mwabukusi. Km wana stress zao watafute namna ya kuzimaliza huko huko wasitumie mipango mizuri ya serikali.

Ndo maana tutafika tumechelewa, izo nchi zilizo endelea raisi anatukanwa vizuri tuu akijivuruga, izo mila sijui desturi na dini ndo zinapumbaza bongo zetu, ye ni mtanzania kasoma mkataba kaona shida zilizopo kwenye mkataba ndo kaamua kupaza sauti kwa namna anayoona ipo sahihi kosa lake ni lipi apo? Hii nchi huwezi sikilizwa bila ya kua ivo ndo maana katimia lugha inayofichwa fichwa na wengi kusemea taifa lake.
 
Ebu iweke hiyo mipaka na utuambie sheria inayoweka hiyo mipaka.

Kama wanaona ana jinai,wampeleke mahakamani ili ujinga wao umaonekane wazi, siyo kumtishia.
Zipo laws of natural justice ambazo sio lazima ziwe coined na katiba yoyote ila kila mmoja mwenye akili timamu anapaswa kufahamu lakini pia tuna tamaduni zetu ambazo ndio msingi na uhai wa taifa letu. Wakili anapayuka sana mpaka kupoteza stara licha ya kujenga hoja zinazoeleweka. Anafoka as if anawafokea watoto wake, mamlaka huwa zinalindwa na kuheshimiwa duniani kote sio busura kwa mtu msomi kama huyo jamaa kutoa kauli zingine kama kejeli, aadhibiwe.
 
Barua hiyo ya wito kutoka ofisi ya DCI inamtaka Dkt. Nshala kufika kwa ajili ya mahojiano


Ofisi hii inafanya uchunguzi kuhusiana na kauli ulizotoa tarehe 03 Julai 2023 na kisha kusambazwa katika vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam

Ili tuwe kukamilisha uchunguzi wetu, ofisi hii inakutaka ufike ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Kanda Maalum Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2023 saa 09:00 asubuhi bila kukosa kwa ajili ya mahojiano.




Pia soma:
Rugemeleza Nshala: Tutafungua Kesi kupinga Mkataba wa DP World na Tanzania
Dkt. Rugemeleza Nshala: Nimetishiwa maisha baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World
Kwenye kuitikia huo wito Dr. Rugemeleza aongozane na Adv Kibatala, ni imani yangu mahojiano hayatazidi dakika tano.
 
Back
Top Bottom