consigliori
JF-Expert Member
- Mar 29, 2010
- 392
- 89
Mimi sina sababu ya ku-challenge uwakili wako au uelewa wako. Km wewe na wateja wako mmeamua kujibu tuhuma na kuwasilisha maamuzi kwa kamati kuu sasa kuna sababu gani ya ku-pre empty decision ya kamati kuu na kuleta kesi yenu kwa vyombo vya habari? Je waandishi wa habari ndo sehemu ya vikao vya chadema! Hapo wakili umechemsha labda km unafanya mikutano na waandishi wa habari kujitafutia jina/kuji-market! Wewe ukiwa wakili wao kwa nini usitoe hoja zako humo za kukiukwa kwa vifungu na kuomba swala hilo lipitiwe upya ama na kamati kuu au kikao cha juu yake, ili utaratibu mzuri ufanywe haki itendeke? Ni swala la kawaida hata mahakamani kuomba mahakama kupitia tena hukumu yake kwa vile kuna vifungu au ushahidi haukuzingatiwa. Halafu kwa nini msisubiri majibu au matokeo au maamuzi ya kamati kuu kwanza km wataendelea kuwavua vyeo au kuwafukuza chamani, baada ya hapo sasa mkate rufaa? Utaonyeshaje nia ya kukata rufaa hata shauri halijasikilizwa? Huko ni ku-pre empty decisions na kujaribu kuitisha kamati kuu! Km mlitaka kukata rufaa kupinga maamuzi ya kikao kilichopita cha kamati kuu mngekuwa mmefanya hivyo siku nyingi na siyo kusubiri hadi siku 14 zinakwisha? Kwa utaratibu wewe kama wakili wao ulipaswa ukitaarifu chama cha chadema nia yenu ya kukata rufaa kwanza na siyo kuanzia kuvitaarifu vyombo vya habari. Nahisi nia yenu si kujenga chama bali ni kubomoa kwa kisingizio cha maamuzi ya kamati kuu. Na kuhusiana na uhusika wa zitto katika vurugu mimi nilidhani zitto angejitokeza kuanzia day one pale viongozi wa kigoma walipotoa tamko la kumzuia Dr slaa kwenda kigoma ingeleta more sense au hata walipofanya maandamano kwenda polisi? Yeye binafsi au wewe ulitakiwa utoe statement immediately ya kukemea lakini mliziba masikio na kufumba macho hadi mwone mambo yanakwendaje! Mmekuja kugundua Dr Slaa hakutishwa na matamko hayo na watu walijitokeza katika mikutano yake hadi anamaliza ziara yake. Hapo na nyie ndo mnatoa very thin explanations ya kukanusha lakini circumstantial evidence zina m-implicate zitto katika vurugu au waraka wa siri, hawezi akafanyiwa mapango wa uongozi bila yeye kujua NEVER NEVER! Vurugu haziwezi kuandaliwa jimboni kwake pasipo yeye kujua NEVER NEVER! Nawasilisha, mimi ni wakili wa kuzaliwa au wa wito na si wa kusomea lakini.
hii yote paragraph moja! duh