Mwalimu wa tuisheni
JF-Expert Member
- Oct 19, 2019
- 5,476
- 8,600
Wakazi wa mkoa wa Lindi wameridhia kumpa muwekezaji hekari 1000 kwaajili ya uwekezaji.
---
Mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 12 baina ya Mwekezaji pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Kichonda katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi umetatuliwa na Naibu Waziri wa Ardhi Geofrey Pinda baada ya Wananchi wa kijiji hicho kuridhia kumpatia hekari 1000 Mwekezaji huyo.
Taarifa zinaeleza kuwa Wananchi hao wameridhia kutoa ardhi hiyo kwa lengo la kuchocheza maendeleo ya kijiji hicho. Msosa Said ambaye ndiye Mwekezaji ndani ya kijiji hicho anaeleza kuwa baada ya kukubaliwa kuwekeza katika eneo hilo Wanakijiji watanufaika kwa kupata elimu ya kilimo biashara, Watapata ajira na kufanya biashara.
Waziri Pinda anaeleza kuwa Wizara imeshakaa na Mwekezaji huyo na kwa kuanzia watampa hati ya awali (hati ya kimila).
Source: ITV habari
My take: Je, na wao wamemuuzia muwekezaji, au wamenunuliwa..?
Tujadili kwa hoja sio matusi