Wakazi wa jiji walilia umeme, wakata tamaa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
WAKAZI WA jiji la Dar es Salaam wameonyesha kukata tamaa kuhusiana na umeme wa uhakika na kufanya walilie nishati hiyo kutokana na uchumi na hali ya kifedha kuzidi kua ngumu siku hadi siku kutokana na kukosa huduma hiyo muhimu Wakazi wengi ambao ni wafanyabiashara wanaotegemea nishati huyo wamejikuta wakiporomosha mitaji yao huku wengine wakionekana kufunga ofisi kutokana na kukosa nishati hiyo kwa muda mrefu huku hali hiyo ikifanya baadhi yao kuchanganyikiwa kimaisha

NIFAHAMISHE imeshuhudia jana mwanamke mmoja anayefanya biashara ya vinywaji ikiwemo uuzaji maziwa wa jumla amejikuta akililia hali ya kukosa umeme kwa kua amekua akimwaga lita kadhaa kila siku kutokana na bidhaa hiyo kuharibika

Mbali na kuwaza umeme pia amekuwa akililia umaliziaji wa deni la fedha linalomkabili katika taasisi moja inayokopesha wanawake kwa lengo la kujiendeleza hali inayofanya achanganyikiwe kwa kuwa hakuwa na rejesho la kurejesha ili kumaliza mkopo aliopewa katika taasisi hiyo

Mbali na mwanamke huyo pia ilishuhudia wafanyabiashara wa vinywaji baridi, stationary na wengine wengi wakilalamikia kukosa huduma hiyo ya nishati hali inayofanya kujkosa usingizi kutokana na kuporomoka kiuchumi wka kwua ofisi hizo huwasaidia kuingiza kipato chao cha kila siku ikiwemo na kujipatia fedha ya kujikumu na familia zao

Hali ya umeme jijini Dar es Salaam haipatikani kwa uhakika na wakazi wengi wakionekana kukata taamaa juu ya huduma hiyo kwa kuwa Shirika la Umeme Tanesco kutangaza makali ya mgaona kukiri hali kuwa tete kwa kuwa uzalishaji wa nishati kupungua

Baadhi ya maenenop umeme hupatikana kwa dakika kadhaa na si masaa kama awali huku wenigne wakikosa kabisa nishati hiyo kwa karibu siku mbili mfululizo hali inayofanya kukosa uhakika wa umeme kwa Watanzania

Chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
 
Ni upuuzi kukaa nyumbani na kulilia umeme(kunung'unika)!AMKENI JITOKEZENI BARABARANI muoneshe hasira zenu.
 
Ni upuuzi kukaa nyumbani na kulilia umeme(kunung'unika)!AMKENI JITOKEZENI BARABARANI muoneshe hasira zenu.
<br />
<br />
Pengine hasira zitaonyeshwa ifikapo2015 nayo sio mbaya ingawa tutakuwa tumesha umia sana.
 
ni kweli kabisa, kila pembe wameshika tamaa , wapo ambao wamejinunulia viledio vidogo wakisikiza bunge , wengine wakisikiriza mizikila maneno makali ya ROMA, huku wakisubiri kuuziwa nyumba na majembe action , wanaojiiita vijana wa kazi. Wengine wapo wanasubiriwa na wachina huku wakizunguka huku na huku wakiulizwa neno moja tu, bado mzigo, ndio wachina hawahawa waliojitolea kuwakopesha vitu wananchi nguo, viatu, simu na mabegi sasa wanaona godawn zimejaa hakuna wanunuzi, hukipanda basi utasikia , "kondoa na mia mbili leo hakikueleweka si unajua tena umeme" Konda anajibu sawa lakini usizoee, utakosaje kutozoea , Tanesco wasitufananishe na Bata ambao wakikosa nchi kavu wanazama majini kutafuta.
 
Back
Top Bottom