Wakati wa mimi kusema umefika

Propaganda za kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 kuna mengi yatajitokeza. Mi nakushauri kijana kama unatafuta umaarufu kwa kupitia marehemu ujue unajitafutia matatizo, fanya kazi za halali ujipatie kipato cha halali na Mungu atakulinda na kukubariki vinginevyo Mungu atakuacha uangamie. Jeshi la Polisi lilishafanya kazi yake na kumaliza na wewe kutoa ushahidi wako, kama ulidanganya na kuficha ukweli inamaana wewe ulihusika moja kwa moja na kifo cha marehemu Wangwe kwa hiyo adhabu uliyopewa ya uzembe haikustahili bali ulitakiwa ushitakiwe kwa kuua kwa kukusudia na adhabu yake iwe ni kunyongwa mpaka ufe.
 
Nimeamini kuwa watanzania wengi tuko nyuma kwenye "fasihi" mnataka nini tena Deus Mallya aseme? mbona mwenye akili tayari anajua ebu angalia nukta zifuatazo:
-Kwamba hatojibu wa vile anapokea matusi, kejeli na kutishiwa kuvamiwa,
-Kwamba ameambiwa akae kimya,
-Kwamba hata wakimtisha na hata akifa ukweli utabaki kuwa ukweli na utaishi hata kwa vizazi vijavyo,
-Kwamba wanaomtisha na kumwambia akae kimya ni wafuasi wa chadema,
-Kwamba tujiulize kwa nini wanamtisha na wanamwambia akae kimya?
-Kwamba wanamwambia akae kimya ili asiseme nini?
-Kwamba kwa nini chadema wana hofu asiseme?
Tukijiuliza na tukichambua nukta hizi tutapata jibu, na kwa mwenye akili jibu liko wazi na kuwa Deus Mallya kwa maana nyingine tayari ameshasema.

Kwenye fasihi hapo ndiyo kunanini wewe ..........fu
Mbona sioni hicho alichosema kifasihi.
Kama anaweza afunguke tu,
 
Hivi jamani,,ndugu yangu Ben Saanane yuko wapi..,mbona simuoni akitokwa mapovu kwenye thread kama hizi...yaani Mzee wake anakaribia kupelekwa lupango na yeye amekaa kimya kama hayamuhusu..njoo uwaambie umma wa JF kuwa hatuhusiki na atakachosema Mallya ni uzushi.

Duh "Benazir" !

Sasa mimi naingiaje hapa? Povu ulilotoa hapa linatosha.Niongeze lingine la nini?
 
Propaganda za kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 kuna mengi yatajitokeza. Mi nakushauri kijana kama unatafuta umaarufu kwa kupitia marehemu ujue unajitafutia matatizo, fanya kazi za halali ujipatie kipato cha halali na Mungu atakulinda na kukubariki vinginevyo Mungu atakuacha uangamie. Jeshi la Polisi lilishafanya kazi yake na kumaliza na wewe kutoa ushahidi wako, kama ulidanganya na kuficha ukweli inamaana wewe ulihusika moja kwa moja na kifo cha marehemu Wangwe kwa hiyo adhabu uliyopewa ya uzembe haikustahili bali ulitakiwa ushitakiwe kwa kuua kwa kukusudia na adhabu yake iwe ni kunyongwa mpaka ufe.

Naona mapovu tuuuu. Shangilia atanyongwa soon sasa.
Acha kelele
 
Ukiwa Muongo kuwa na kumbukumbu.. Ukiona mbwa anabweka sana jua kuna mwenye mbwa anamsukuma
 
Dogo hao CCM watakutumia kwa propaganda zao na kuku-damp km vile dekio chafu, wapo wengi waliofsnywa misukule km ww kwa njaa za siku moja. Kwanini uje useme huo ukweli Leo siku zote ulikuwa wapi? Kumbuka Watanzania wa Leo sio wale wa zidumu fikra za mwenyekiti, ni vigumu sn kuwadanganya kwa propaganda za kipuuzi. Wote tunajua kwa unatumika na CCM, angalia kuwa watoto na wajukuu zako watakuja kujiuliza kuwa mzazi wetu kwanini alikuwa hivi! Be ware

Hahahahahaaah
Kwani umejua anachotaka kusema?
Acheni kujistukia
 
Huyu Malya nadhani karukwa akili maana kila siku anasema, 'nitasema, nitasema', kama huna la kusema kaa kimya. Wewe inaonesha huna la kusema. Yaelekea bado unaandaa sinema yako, sasa kila ukipima upepo kama watazamaji wataipokea unakuwa huna uhakika.

Tuliza kichwa na akili, kama zimo. Kutumika hakuweza kumwinua mtu zaidi ya siku moja kummaliza. Jifunze toka historia, ni nani aliyetumika halafu siku moja akawa maarufu au kuaminika. Watazame akina Kabourou, Tambwe, Juliana, Mpembwa, Masumbuko, n.k.
 
Mbona mnakimbilia chaka jamaniiiii. Kusema ni kutumika? vitu viwili tofautiii
 
Usimuogope atauwa mwili tu ila roho na ukweli utabaki
 
Attachments

  • 1409563181229.jpg
    1409563181229.jpg
    64.3 KB · Views: 162
Usichezee Jina la Mungu. Mungu haunganiki na mnafiki na wauaji. Kuendelea kutumia jina lake katika uovu ni kutafuta laana zaidi maana ulikwishalaanika wewe na vizazi vyako mpaka kizazi cha 4.

Salaam!

Kwa muda Mrefu nimekuwa nikipata msukumo unaonitaka kuzungumzia maneno yaliyosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari hivi karibuni kutoka kwa ndugu ma makundi mbali mbali.

Kimsingi sintajibu wanayotaka kwa sababu nimeendelea kupokea jumbe za Matusi na kejeli hata kuvamiwa na wanaodai ni wafuasi wa CHADEMA wakitaka niendelee kuwa Kimya!. Wapo walioamua kujitaja majina yao ili nijue ni kiasi gani wako 'Serious' kwenye kile wasemacho!.

Japo nilishatoa taarifa Polisi, kwa sasa nimechoka kuishi maisha ya kuwindwa ndani ya Nchi yangu. Nimechoka. Nitakachofanya ni KUONGEA na si KUJIBU kilichosemwa na yeyote kuhusu Mimi na 'Ajali ya Pandambili'

Naamini kwa Mungu siku zote
Naamini nikifa ni kwa Mpango wake

Nikifa ukweli Utaishi hadi vizazi vijavyo.

Deus Mallya
Dar es Salaam.
 
We nae Mallya ni mnafiki tena haufai ktk jamii, inakuaje unaficha uovu mpaka leo ndo unataka kutuaminisha upuuzi gani
Hapa au mmeshndwa kuelewana kwahyo ukaona utibue
Kabla ya kutibua jihukumu kwanza kwa ujinga wako
 
Siasa ni nzuri sana hasa zikiwa upande wako...Inaonekana dogo sasa anataku kutengeneza headline kama za Mahimbo wakati ule wa uchaguzi...

Kila la heri na siasa zenu!! Tunachotaka sisi ni kuona ni kwa kiasi gani gesi na madini zimeweza kuwaletea maendeleo Watanzania.., ni jinsi serikali imeweza kuwazuia wakwepa kodi na kuweza kuongeza makusanyo ya mapato...etc

Nani alimuua huyu
 
Attachments

  • 1409563310537.jpg
    1409563310537.jpg
    7.8 KB · Views: 354
Usichezee Jina la Mungu. Mungu haunganiki na mnafiki na wauaji. Kuendelea kutumia jina lake katika uovu ni kutafuta laana zaidi maana ulikwishalaanika wewe na vizazi vyako mpaka kizazi cha 4.

Mmepewa mamlaka hata ya kutoa laana kwa wenzenu? noma sana
 
ha ha haa!

Kasi hii ya siasa za vijana sidhani kama zitaisaidia zitaikwamua nchi yetu toka kwenye umasikini uliopindukia. Sipati picha ingekuwaje endapo Mwl Nyerere na vijana wenzake enzi zile wangeshupalia siasa za namna hii.

Back
Top Bottom