Wakati wa mimi kusema umefika

Mkuu mwaga mboga yote na hata maji yakunawa ikiwezekana!

Nakumbuka walisema wewe ni msaliti na majuzi ulikuwa kwenye maongezi!

Mkuu sema bila kuogopa!

Sasa Mbowe na Mnyika tumbo joto!

R.I.P Chacha wangwe!
 
Usiogope, sema lakini semea mahali stahiki, na ni kwa hao nlokuambia. Kama ulifungwa kwa kuonewa, nenda kwa walio tofauti na serekali. Tafuta msaada, Haki za Binadamu. Usitishie watu na weye kuwa unajua kuchonga. Amka asubuhi, chonga sana ila chongea penyewe wala usipotee njia mchongo wako ukapotea tena.

Acha vitisho unataka hasiseme? Hata Lwakatare alikamatwa kupitia ushahidi ulio tolewa kwenye mitandao!

Usimfundishe chakufanya!
 
Diallo amekupa sh ngapi ? Hela ya watu itakutokea puani ! Unafungwa miaka 3 halafu baada ya wiki 2 unapata msamaha wa rais , bahati ilioje !

Mkuu hapo juu nimemshauri kuwa hiyo taarifa yake ni bora aende akaitolee kule Tarime ambako ndio Marehemu Wangwe alikokuwa anakuwakilisha. Kisha akirudi hai kutoka huko aje atumegee na sisi hapa JF


Sent from my iPad using JamiiForums
 
- HA! HA1 HA! HA! HA! mbona mnaaanza kutoka mapovu kabla mwananchi hjasema lililotokea mnajua kumbe kilichotokea ha! ha!

Le Mutuz

Ni kweli tunajua kilichotokea kuwa gari ilipata ajali ikasababisha kifo cha Wangwe.Polisi na madaktari na mwisho mahakama waliweza kuthibitisha hivyo kuwa kifo cha Wangwe kilisababishwa na ajali.
 
Kama unatumika kwa vile kipindi cha uchaguzi ndani ya chama kimefika basi umepotea njia. Kumbuka humu JF watu walikutetea sana na hoja nyingi za kizushi kuwa ile haikuwa ajali bali ni mpango wa mauaji ulioandaliwa na Chadema.

Mbona kama Chadema mnahofia ukweli na kuanza kujihami na kutaja taja watu.Ebu mwacheni Deus atoe dukuduku lake,haraka ya nini labda anakuja kutangaza nia ya kugombea ubunge 2015?
 
Duu hawa chadema wakiguswa wameanza kugwaya hata mallya hajasema chochote. ile kusema nitaeleza ukweli kelele matusi dharau yameanza hivi mkipewa muongoze nchii si mtazuia wananchi wasiseme kero zao.kwa ukweli huu 2015 msahau kushinda
 
Move yako na Dialo ndio imeanza ama tusubiri ingine?

Kuna thread ulishajibu kuhusu kifo cha Kamanda Chacha Wangwe.

Ndg. Kimbuka ndugu wa Chacha ni binadamu kama unamtumia marehemu ili kujijenga ama kupata pesa inawauma sana.

Why usitafute kick zingine?

Ok weka hiyo move CHADEMA ni mpango wa Mungu.

Hatafuti kick nyie mlianza kumuita msaliti na mkamsingizia ana wasaliti sasa yeye leo ana mwaga mboga!

Amekuwa akiwatete sana viongozi wenu na mkakosa shukrani sasa amechoka!

Deusi Mwaga Mboga!
 
CCM wamefikia kubaya, yaani wanaanza hadi kutumia Siasa za Marehemu kujinusuru!!

UGAIDI - ukashindikana
UDINI - Ukashindikana
UKABILA - Ukashindikana
KUASISI USALITI NDANI YA CDM - Umeshindikana

Sasa tumehamia kwenye Siasa za kutumia Marehemu kujinusuru - CCM mnajidhalilisha sana.
 
Baada ya msajili wa vyama kuja na ile single yake ya kuwa katiba imechakachuliwa na Mbowe na Slaa hawana sifa ya kuongoza tena kukosa soko na kutupiwa kapuni, sasa wanakuja na propaganda za kuchafuana kwa kutumia vijana wasio jielewa huku taratibu za uchaguzi zinasonga mbele.

Shukrani sana kwa Idara ya oganizisheni na uenezi ya CCM kwa kuisaidia Chadema kueneza Chama ( bila wao kujua) na ningewashauri wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema waandae tuzo maalumu kwa Nape na Idara yake kwa kazi nzuri wanayoifanyia Chadema. Tutawakumbuka sana kwa kujitoa kwao kwa kazi hiyo yenye faida kwa Chadema.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Wewe si si ndio ulikuwa kwa Antony Dialo Mwanza kusajiliwa ukaongee na vyombo vya habari kwa kulipwa ili ukauze uzushi??!!
 
Deus Mallya si ndiyo wewe uliyepigisha mbono Chacha Wangwe? Au ww ni mwingine? Pia naskia Diallo kakukatia mtonyo kwa Mpesa kama Ludovick ili utengeneze bongo movie nyingine,
 
Nimesoma nimekuelewa Ndugu Mallya
lakini ni lini utasema? pia kinachonitia mashaka ya unachotaka kusema ni kujitokeza kundi linalopinga wewe kusema. Hili kundi ni la nani? Liko chini ya nani? Wanataka unyamaze kwa faida za nani?
 
Daaaah!
Siyo kila mtu hapa ni mwana siasa!

"Double jeopardy"inakataza kesi iliyokwisha kuamuriwa Mahakamani kurudishwa kwenye Mahakama ingine yyt ile!Alikuwa na nafasi kusema hayo anayotaka kusema siku hizo yupo Mahakamani sio sasa!

Huyu ni msanii tu hana jipya!!

Mbona unatokwa na povu sana??? Kwanini hamtaki aseme? mnaficha nini?
 
Back
Top Bottom