Mwanafalsafa
Platinum Member
- Jun 24, 2007
- 662
- 851
Nimepitia matokeo ya NECTA kidato cha pili na kugundua jambo lifuatalo.
Shule za Kata zina ufaulu hafifu sana (mwingi ni wa daraja F) katika masomo yote isipokuwa somo la Kiswahili. Somo la Kiswahili ndo limezibeba shule za kata zisitumbukie shimoni kabisa.
Mifano michache ni hii hapa (ikiwemo shule ya Mburahati ambayo imevuma hapa JF kwa jinsi ilivyopata sifuri nyingi):
Hii maana yake nini?
Hii maana yake ni kwamba Kiswahili kinaeleweka vizuri zaidi. Wanaosoma shule za kata mara nyingi ni watoto wa maskini ambao elimu ya msingi waliipata kwenye shule za serikali ambazo huwa zinatumia Kiswahili. Kwa hiyo wanapoingia kidato cha kwanza wanakutana na Kiingereza kinawasumbua.
Ila utafiti zaidi unahitajika ili kujua ufaulu wao ulikuwaje kwenye shule za msingi walikotoka ambako walikuwa wanatumia Kiswahili.
Wazazi maskini hawana hata bajeti za kuwalipia watoto hawa wakasome masomo ya ziada ya Kiingereza (yaani "twisheni" au "English course"). Kwenye hizi shule ndo kuna watoto wa wale akina mama wanaolea peke yao, ambao wanatembeza mabeseni ya matunda na mihogo mibichi barabarani kutafuta pesa.
Kwa wale wanaosemaga kwamba maarifa mengi yako kwa Kiingereza, jibu ni kwamba Kiingereza kinatafsirika. Lakini tusijidharau na lugha yetu ya Kiswahili hata siku moja. Hakuna jamii iliyoweza kupiga hatua kwa kujidharau.
Hata hao Waingereza wenyewe walikuwa koloni la Ufaransa na walikuwa wanatumia Kifaransa kama lugha rasmi ya serikali na sheria.
Lakini mambo makubwa walianza kuyafanya walipoachana na Kifaransa (ambacho walikitumia kwa miaka 700) na kukumbatia Kiingereza kama lugha ya serikali na ya sheria.