Wakati ni sasa, Katiba mpya ni muhimu. Je, kwa harakati hizi tutapata Katiba sahihi?

Katung'a

Member
Jul 2, 2015
38
19
Kumekuwepo na ushinikizwaji wa kupatikana kwa Katiba mpya ambao umekuwa ukiendelea kufanywa na kundi kubwa la wanaharakati wakiongozwa na chama la wana CHADEMA huku chama cha mapinduzi (viongozi na Baadhi ya wanachama) wakionyesha kutokua tayari kwa kipindi kushiriki katika mchakato mzima wa kupata katiba mpya.

Wakati haya yakiendelea viongozi wa dini, wasomi wakiibuka na mitazamo tofauti huku wakiwaacha wananchi wengi ambao ndio hasa wahitaji wa katiba mpya wakiwa hawajui wasimame katika upande upi.

Swali langu, Kwa harakati hizi zinavyoendelea, Je tunaweza kuendelea na mchakato wa kupata katiba mpya yenye kukidhi matakwa ya watanzania?? Je waliopoka mchakato wa awali wa upatikanaji wa katiba wanaweza kukwepwa vipi katika mchakato huu wa sasa?

Je, watanzania wanahusishwa vipi katika kupata katiba bora ambayo ndio hitaji lao kwasasa? Vipi KUHUSIANA na kauli ya Rais ya kuhitaji muda Kwenye suala la katiba? Kauli ile (kwa mamlaka yake) inaweza kutenguliwa na nani?

Tuwaze kwa maslahi mapana ya watanzania na sio kwa maslahi ya kundi fulani.

Karibu tujadili
 
Hauwezi kusisitiza ujenzi na uboreshaji wa nyumba ya jirani yako, na wakati banda lako linavuja. Jenga kwanza kwako ili uwe mfano mzuri kwa jirani yako. Kwa sasa Mbowe arudishe katiba ile aliyoikuta chamani ambayo ilikuwa inamruhusu mwenyekiti wa chadema kukaa madarakan kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Kinyume na hapo hakuna mtu mwenye akili atakubali kufuata mkumbo wa hili genge la wachumia tumbo ambao wamefanya siasa ni kichochoro cha kupitishia ajenda za kuliangamiza taifa. Kama kanogewa na uenyekiti wa chama tu, je kwa upande wa uraisi itakuaje?
 
Back
Top Bottom