Wakati gani Mabasi yakaguliwe

IshaLubuva

JF-Expert Member
Dec 4, 2008
250
11
Ijumaa iliyopita nilikutana na kero ya Polisi wa Usalama Barabarani wakati nikisafiri kutoka Dodoma Kwenda Kondoa Irangi na Basi la Machame Investment. Abiria tulitakiwa kufika kituoni saa 11.30 alfajiri ili basi lianze safari saa 12.00 asubuhi. Abiria tukawa tumetimiza wajibu wetu na ilipofika saa 12.00 asubuhi basi likaanza safari. Tukiwa tumeondoka kwenye stendi ndogo ya CCM Makao Makuu tukapigwa mkono na Polisi wa Usalama Barabarani. Na baada ya maongezi kati ya Polisi na wafanyakazi wa basi, dereva akaambiwa alipeleke basi kituo cha polisi kwani lilikuwa halijakaguliwa. Tumefika kituoni na kukaa hadi saa 1 na ushehe hakuna ukaguzi uliofanyika. Mimi nikawa nimeteremka kwenye basi na kuwasha kamera yangu kujifanya kama nachukua matukio fulani hivi, ndipo Askari mmoja akajitokeza na kusema namnukuu "sisi tunafanya kazi kwa uwazi kabisa, angalia milango yetu iko wazi kabisa; tunamsubiri Askari wa Vehicle inspection ili aje kuikagua basi yenu". Mimi nikamwuliza;

1) Kwani hili basi ratiba yake si inajulikana kuwa linatakiwa kuondoka saa 12.00 asubuhi iweje lisikaguliwe kabla ya muda huo?

2) Hamuoni kuwa mnaharibu ratiba za wasafiri ambao wanatarajia kuwahi mabasi ya kuunganisha?

3) Na iwapo mtagundua kuwa basi hilo halifai kwa safari nani atawajibika kurejesha gharama za teksi walizolipia abiria ili kuwahi muda wa safari?

4) Kwa nini gari lisifanyiwe ukaguzi jioni ya siku moja kabla ya safari ili kuokoa muda wa wasafiri lakini pia kuzuia haja ya kufidia muda waliopoteza wakikaguliwa?

Alichonijibu ni hivi;

"Hoja zako zote ni za msingi lakini sisi (Polisi wa Usalama Barabarani) tunatekeleza tu amri za wakubwa wetu, wasubiri wakija uwaeleze ushauri wako". bahati mbaya/nzuri basi letu lilikaguliwa na kuruhusiwa kuendelea na safari na mimi sikupata fursa ya kufika ofisi ya kibosile wao ili kuwasilisha maoni yangu. Kwa hiyo nayaweka hapa JF ili tujadiliane ni wakati gani muafaka kulikagua basi. Natoa hoja
 
Hoja yako nzuri sana hivyo ndo hasa inavyotakiwa, hivi si kuna chama kinachoongoza biashara ya mabasi? wao wanatakiwa kuwasilisha hoja kama hizo, juzi juzi nilikia kuwa IGP amewatimua askari waliofanya uzembe wa kutozuia gari lisiendelea na safari kwani baada ya ajali ilibainika kuwa matairi yalikuwa mabovu. hapa cha msingi ni gari kukaguliwa mwanzo wa safari, askari wa njiani ni kuhakikisha kama limekaguliwa , kwani hapo mwanzo wa safari baada ya kukaguliwa inabidi wapewe inspection certificate.

Mapendekezo ni kwamba mwisho wa kila safari gari lifanyiwe ukaguzi ili kesho yake iwe ni safari tu kuondoa usumbufu kwa abiria.
 
Back
Top Bottom