BABA KEREN
Member
- Jun 5, 2011
- 29
- 12
Wakata Miwa wa Kiwanda cha ILOVO chenye Matawi Mawili (KILOMBERO-1 na KILOMBERO-2) Leo ni siku ya Nne wamegoma wakidai Nyongeza ya Mishahara yao, huku wakiwa na Maandamo yasiyo Rasmi wakiwa na Fimbo mikononi mwao tayari kumuadhibu Yeyote yule atakaye wasaliti katika Maamuzi yao.
Mpaka muda Huu ninapo wajuza taarifa Hii kuna hali ya sintofahamu kati ya WAKATA MIWA na UONGOZI wa Kiwanda.
Nimejaribu kufanya Mahojiano na Baadhi ya Wakata miwa Hao kutaka kujua endapo wataweza kusitisha Mgomo wao Haraka ili warejee katika Mazungumzo Mezani nao wamenieleza yakuwa, wapo tayari kusikia kwanza Mabadiliko ya Fedha na Si Vinginevyo. Mpaka sasa Usiku wa Saa 2:45 tarehe 18 August 2011 Wakata Miwa hao wanaendelea na Maandamano.
Kuna taarifa zasizo Ramsi ya Kesho kufika Waziri Mkuu-Mh:Mizengo Kayanza Peter Pinda.Kesho zaidi nitaendelea Kuripoti Yatakayojiri.