wakaka kujeni huku mnifadhili shemeji yenu...

The Donchop

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
294
376
Hamjambo?
Jamani mimi nina shida. Hapa nimeachwa na bae nina kama wiki mbili hivi. Kisa cha kuachwa ni cha kawaida sana. Uzuri tunaongea kwa simu ingawa mara ya kwanza aliniblock ila sijui nini kilimpata, alinifungua (kunitoa kwenye block list) na kunitumia pesa bila kuniambia. Nilipoikuta pesa, nikajaribu kumpigia nimjulishe, bila kutegemea nikakuta inaita na akapokea na nikaishia kumshukuru tu.
Kaka zangu, nipeni maujanja ya kurudiana na huyu mtu. Sitaki kabisa aondoke katika maisha yangu. Nampenda sana na hata yeye anajua hivyo. Tatizo haonyeshi ushirikiano wa kurudiana nami.
Nipeni maujanja mwanawane.
 
Sasa shemeji kwan ulimuudhi nin kaka yetu maana kila comeback inategemea na kosa ulilotenda, halafu sikukuu zimekaribia lazima uwe mpole.
 
Tafuta Kanisa lenye Nguvu ya Mungu, ukatoe sadaka ya kumshukuru Mungu. Kila jambo litakuwa kama upendavyo na kwa kadri utakavyotaka. "UKITAKA UNAWEZA"
 
Sasa kama hadi anakutumia pesa si bado yuko keako!! We mpelekee mzigo ale maisha yaendelee
 
Kama ameku unblock na amekutumia pesa ni dalili bado ni wako huyo...

We endelea kuwasiliana nae kama kawaida.. Si unajua tena wanaume walivo sanyingine wanapenda kubembelezwa
 
Was finna ask what's in it for us, but decided against it.

Hebu taja hicho kisa cha kuachwa tupime wenyewe. Pengine si cha kawaida kama unavyodhani.
 
Hamjambo?
Jamani mimi nina shida. Hapa nimeachwa na bae nina kama wiki mbili hivi. Kisa cha kuachwa ni cha kawaida sana. Uzuri tunaongea kwa simu ingawa mara ya kwanza aliniblock ila sijui nini kilimpata, alinifungua (kunitoa nami.
Nipeni maujanja mwanawane.
cha kawaida ndo kisa gan hcho?
 
Siku nyingine usijisahau basi......amefikiria mengi so be carefully atarudi tu huyo!! Uwe na Amani ashaona umuhimu Wake
 
Mtumie sms mwambie humuombi tena hela ila yeye atakuwa anagegeda tu. Full stop
 
Mapenzi ya vijana wa siku hizi yana tabu kweli kweli......

Kwa kutumia tu akili ya kawaida ni kuwa huyo kijana mwenzio bado anakupenda na bado amekuweka moyoni.......ndio maana akakumbuka na kukutumia fedha........

Ingawaje hatujui kisa cha wewe kugombana na kijana mwenzio mpaka kufikia kuachana.....lakini mimi nawaasa vijana wote kuwa wanapokuwa katika mahusiano.....msipende kudharau tatizo au kero......

Kwani jambo dogo sana ambalo katika hali ya kawaida unaweza ukalidharau....lakini kwa mwenzio likawa kubwa sana mpaka kupelekea kumnyima.....mpaka ukija kushtuka unakuta mwenzio ameshakukatia tamaaa.....

Cha msingi hapo kwa kuwa ameshakuja kwenye maisha yako tena......jaribu kwa kadri ya uwezo wako kuachana na mambo aliyokuwa akiyalalamikia kuwa hayapendi......

Jiepushe katika mambo yaliyokuwa yanawaletea ugomvi..na mikwaruzano.......

Pia kumbuka mafahari wawili hawakai zizi moja.....na hewala si utumwa......jishushe kwake kwa kuwa yeye ni kiongozi wako na dira yako.....na sikio halizidi kichwa..........

Kitendo cha wewe kujibizana na yeye hata katika mambo madogo kinaweza kikamfanya aone kama unataka kumpanda kichwani au unamtawala....ingawaje wakati mwingine unapaswa kumjibu......

Kuwa mtu mpya kwake mpaka aone kama ndio mmefahamiana upyaa......

Kila la kheri kwenye mahusiano yako.....
 
Kama bado anakutumia hela sioni kama anatatizo na ww sema tu unajishtukia inaonekana ww ndio mkosaji
 
Usipende kupost vitu nusu nusu. Msuluishi mara nyingi huelezwa kila kitu. Endelea kuficha utaishia kudanganywa
 
Kama unapajua anapokaa na una uhakika haishi na mtu, mvizie siku moja kabla hajaenda kazini au usiku kabla hajalala. Vaa koti refu bila chupi ndani wala sidiria. Ukifika kwake, mgongee na akifungua tu mlango, vua koti na ubaki kama ulivyizaliwa kisha umkumbatie na kulia haswa. Lia kike bila aibu ukiwa umemng'ang'ania hata kama atafurukuta usimwachie. Ataelewa umemmisi na sitakueleza yatakayofuata maana wewe ni mtu mzima. Baada ya hapo umweleze namna unavyompenda na kama ulikuwa umejisahau katika maeneo fulanifulani muahidi kubadilika. Mpikie, mfulie nguo, mnunulie zawadi na hata kumsaidia vitu vingine hata kama hajasema. Usibweteke hata kama ana pesa, jishaue na kumpatia pesa, usimchungechunge sana wala kumwonyesha wivu wa kitotokitoto na badala yake onyesha kumjali, usiingilie wala kuhoji sana maswala yake ya kikazi au kibiashara isipokuwa pale atakapokushirikisha, kama anavuta sigara au anakunywa pombe, mnunulie na kumletea bila yeye kuomba mradi iwe brand unayojua anatumia.
Mwombe ngono hata kama utaona aibu na uwe mbunifu sana, mwonyeshe utundu mpaka ule wa akiba. Mwanaume hapendi mwanamke asieweza kujibeba, labda huyo mwanaume awe na tatizo la kupenda kumcontrol mtu ndio atataka uwe na character za mtu asieweza kujitegemea maana ukionyesha kuwa strong, kwake ni jambo linalomtia hofu kuwa hataweza kukumudu ambako kwa tafsiri yake huwa ni kukucontrol na kukufanya kama mtumwa fulani hivi. Msome yeye yuko upande gani na kama ni mtu anaependa ujimudu, buni miradi na kuonyesha kiu na bidii ya kufanya shughuli za kujiongezea kipato chenu.
Kwa haya machache, sidhani kama atatoka mikononi mwako labda iwe ulilala na rafiki yake au mtu yoyote akajua maana hujasema ulichomkosea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom