Wajumbe waasi wa kamati ya utendaji taifa CWT wakimbilia Wizara ya Kazi

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
Kama tulivyowaarifu jana tarehe 15 Juni 2023, kimeitishishwa kikao cha baraza la taifa cha dharura jijini Dodoma tarehe 18 Juni 2023 kati ya mengi ambayo yangejadiliwa ni pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji wa taifa kuvunja katiba na kuvuruga uongozi na chama kwa ujumla. Naibu Katibu Mkuu Joseph Misalaba ameandika barua ya kuzuia kikao hicho jambo ambalo hana mamlaka nalo na kinyume cha katiba huku ikithibitisha pia kuwa anamdharau msajili wa vyama vya wafanyakazi kwa kuamua kwa makusudi kiuka maagizo yake na mamlaka yake aliyonayo kisheria.

Katika hatua ya hivi karibuni yani jana, viongozi wa genge hilo wamekwenda wizara ya kazi kuuona uongozi wa juu wa wizara kuwanusuru kwa kumuagiza/kumuelekeza msajili azuie kikao hicho cha baraza la dharura kwa madai eti hakikufuata katiba. Hatuamini kama msajili anaweza kulifanya jambo hilo kwa kuwa yeye ndiye anayesimamia katiba za vyama vya wafanyakazi. Tunashauri wajumbe wa baraza wapuuze harakati hizi na waende wakahudhurie kikao halali kwa ajili ya mustakabali wa chama chao jijini Dodoma.

Hivi tunajiuliza, wajumbe hawa 18 wakisaidiwa na viongozi waandamizi wa kisiasa wanawezaje kuyumbisha chama kikubwa kama hiki chenye wanachama zaidi ya 280,000. Hatuamini kama viongozi waandamizi wa wizara ya kazi wanaweza kuchangia kuhakikisha kikao hiki halali hakifanyiki kwani kuzuia kikao hicho itakua ni namna ya kubariki harakati za wahuni hawa ambao tayari wana hofu kwamba kikao hicho kitawaadhibu kwa vitendo vyao vya uvunjaji wa katiba na kuuyumbisha uongozi halali.

Ni vyema ifahamike kwamba walimu wapo makini kutazamia hatima ya jambo hili. Kundi hili likiachiwa kuendelea na linachofanya kunaweza kukazuka makundi mengine ya namna hii sio tu ndani ya chama cha walimu bali pia kwenye vyama vingine vya wafanyakazi.
 
Back
Top Bottom