changamoto
Member
- Aug 26, 2008
- 11
- 0
Waislamu wana mkakati wa kususia bidhaa mbalimbali za mfanyabiashara maarufu nchini ambaye ananasibisha Uislamu nchini na Ugaidi na kushabikia matumizi ya kondomu na zinaa kupitia kwenye vyombo vyake vya habari.
Kwa mujibu wa redio Kheri, mfanyabiashara huyo ambaye vyombo vyake wala jina lake havikutajwa alikuwa ni gumzo lililochukua mdua mrefu katika kikao cha hivi karibuni cha viongozi hao.
Inavyoelezwa ni kwamba bwana huyo anajali fedha zaidi kuliko maadili na mahusino mema kati ya Watanzania.
Ametuhumiwa pia kuwa na chuki binafsi na wafanyabiashara wenzie ambao ni Waislamu ambao kaika miaka ya hivi karibuni wamenza kupewa heshima ambazo zamani alikuwa akipewa yeye.
Katika kikao hicho pia kumezuka madai ya Serikali kubagua Waislamu pamoja na bunge kutokuheshimu siku ya Ijumaa ambayo ni siku muhimu kwa Waislamu.
Hivi karibuni bunge lilifungwa sikuya Ijumaa tena katika saa za kusali bila ya wabunge Waislamu kukataa jambo hilo.
Viongozi hao wamewataka pia viongozi na watumishi wa serikali na vyama vya kisiasa ambao ni Waislamu kukomesha tabia ya kujidharau na kuidharau dini yao huku wakitoa heshima na kuwa waoga kwa dini nyingine.
Imesemekana hivi sasa viongozi na watumishi wa umma ambao ni Waislamu ndio wanaowanyanyasa Waislamu wenzao kuliko wale wasio Waislamu.
Hata hivyo, baadhi ya wazungumzaji wamedai kuwa matatizo mengi ya Waislamu yanatokana na kutokuwa na viongozi bora na wa safi na wamefananisha dini hiyo na jengo lenye paa bovu.
Kutokana na sababu hii dini hiyo imeshindwa kuwa na mipango na mikakati madhubuti ya maendeleo maana viongozi wake mara kwa mara wanaishia katika mapambano ya ndani kwa ndani na kulinda nafasi zao ambazo zimegeuzwa njia ya kujipatia riziki wala sio fursa ya kuongoza umma wa kiislamu barabara!
Amedai kiongozi mmoja mwenye msimamo huu kwamba hadi hapo Waislamu watakapojipanga vyema na kuwa na umoja siku zote watakuwa watu wa kulalama na matatizo wakati wana uwezo wa kuweka ajenda muhimu katika namna nchi yao inavyoendeshwa labda kuliko hata watu wa dini nyingine.