Waislam: Hoja ni hijabu si kupigwa kwa DC Igunga.

Na chadema wasipoomba radhi tutaamini kweli CDM inawadharau waislamu, na dharau hii itajulikana inatoka wapi!
chadema wamwombe radhi nani? kama ni kumwomba radhi DC,huyo DC yuko huru kupeleka shauri lake mahakamani na ambapo kwa sasa shauri hilo lipo mahakamani tayari,kwa hiyo tusubiri chombo cha kutoa haki kikatiba kitoe maamuzi.
Na kama suala ni kuomba radhi waislam, unataka kutuambia yule mama DC ni kielelezo cha uislam? yaani ukiachilia mbali hiyo inayodaiwa kuitwa hijab aliyovaa-je tabia zake zinazojulikana na zisizojulikana nazo ni kielelezo cha uislam? kama huyo mama DC ni kielelezo cha uislam, kwa hiyo mambo afanyayo na tabia zake itabidi zienziwe na kuigwa na waislam kwa kuwa huyo mama ni kielelezo cha uislam!?-na hivyo tabia zote alizonazo ndio tabia za kiislam! hivi toka lini kitambaa kikawa na dini? dini anayo mtu au dini ipo kwenye kitambaa? na toka lini hijab au kanzu imekuwa ni vazi lenye 'hati miliki' kwa waislam tu!? mbona hizo zniazoitwa hijab au kanzu huvaliwa pia na watu wa imani nyingine tena hata wale ambao waislam hupenda kuwaita 'makafir' mbona hatujasikia waislam wakitoa matamko kuwa mavazi hayo yasivaliwe na 'makafir', je 'makafir' kuvaa hijab si kudhalilisha uislam? 'kanzu' ngapi zinazoingia bar kunywa pombe siku za kawaida, na hasa siku ya sherehe za idd-huwa tunaona,mbona hakuna matamko? au huko si kuudhalilisha uislam? 'hijab' na 'burqa' ngapi zinazoingia kwenye 'magesti uzinzi' na madanguro,hamzioni? hapo uislam haudhalilishwi? uislam ni vazi au ni imani? mwanamke wa kikristoi akivaa hijab anageuka kuwa muislam? uislam ni vazi au imani? nauliza tena! hivi yule mama DC angekuwa anaitwa Rosemary Kimario na angekuwa kavaa hiyo inayoitwa hijab na yakamkuta masahibu kama hayo, napo mngeng'aka? bakwata wangetoa tamko? nauliza tena, uislam ni imani au hijab ndio ina dini ya kiislam? hivi hawa bakwata wamekosa mambo ya msingi ya kukemea, kama vile ufisadi(rushwa),uzinzi,mauaji ya watu wasio na hatia, ukwapuaji wa rasilmali za nchi kama vile madini,wanyama pori n.k haya hawayaoni? wanaona hijab tuuu...ambayo ccm wanaitumia kama ajenda ya kisiasa ili wapate kura za hijab! na wameshawapata wale wale watu ambao wamezoea kuwapelekesha ambao kila ngoma itakayopigwa na ccm wao hucheza tu hata kama itabidi wacheze uchi! msikieni profesa Abdallah Safari ni muislam lakini ameshajua janja ya ccm-kwa kuwa ni msomi, hivi mufti na naibu wake wana elimu kiasi gani ukiachilia mbali elimu ya dini ya kiislam? waislam wekeni wasomi waongoze baraza lenu na sio hao akina 'ndio mzee' wa ccm! ccm wako tayari kutumia mbinu zozote chafu ili mradi wafikie malengo yao, wako radhi kusababisha hata vita ya kidini kwa manufaa yao, ccm si chama cha waislam,ni genge la watu- waislam kwa wakristo na hata wasio na dini na lengo lao ni moja kuendelea kutawala nchi hii kwa manufaa ya genge lao, uislam na ukristo wao ni ghiliba tu, wanayo imani yao ya kiccm nayo msingi mmojawapo ni kujinufaisha wenyewe na kuendelea kuwatawala watanzania kwa namna yoyote ile-kwa mabavu-kwa kutumia vyombo vya dola-jeshi,polisi n.k! waislam mnasema mlikuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa Tanganyika kutoka kwa mkoloni mweupe lakini nachelea kusema kuwa baadhi ya waislam na bakwata wanachelewesha ukombozi wa watanzania kutoka kwa mkoloni mweusi(ccm)!
 
waombe radhi ya nin?..kuomba radhi means kukiri kosa...sasa kosa likowapi ambalo CDM wamefanya?..intention ilikua kumkamata na sio kumvua mtandio which by the way sio hijabu...hijabu ni nguo inayomsitiri mtu kuanzia usoni mpaka kwa miguu
 
Hawa wanaojiita waislam nawashangaa sana..... Mi naona kuna inferiority complex wao siku zote ni watu wa kuonewa sana why? tena kwa vitu vidogo tu hijab kitu gani? Quran nzima haijalitaja neno HIJAB sasa cjui wao wanalitoa wapi? Kwa upuuzi aliokuwa anafanya hata wangemvua nguo nisingeshangaa.
 
Hapo hakuna chakujadili na kuibua mambo yasiyokuepo,DC haijalishi,wakike,wakiume,mkristu,mwiiskamu whatever,jina lake ni Mwalifu.Sheria ichukue mkono wk.
 
Yale ni matukio ya harakati za kisiasa Fatuma hakuwa akienda au kurudu Masjid- Waislam chonde chonde tusiwe wapiga zumari la Wanasiasa.
 
Kwa hili CCM wanafanikiwa kufitinisha. Ila hii itawarudi tu oneday kwani leo linakuuzwa kwa kuwa hijab imewahusu CDM. Siku ikiwahusu CCC wawe tayari kubeba zigo hili. BAKWATA lini mtaacha kutumiwa kama tawi la CCM?
 
mambo mengine ni magumu sana kuyajadili tena unapofanya assumption ya vitu visivyokuwepo.

Kuuliza kama angekuwa sister wangemvua kitambaa chake ni swali linaloonyesha upeo mdogo sana wa kufikiri.

Mhalifu anaposhughulikiwa huwa haulizwi dini yake, masuala ya kuulizana dini ni huko polisi na mahakamani sio kwenye eneo la tukio.

bwana mkubwa hata kama ni muharifu kuna taratiibu za kufuata, zipo mamlaka ambazo zimeteuliwa kushughulikia waalifu, kama walimuona ni mualifu walitakiwa kuzipa taarifa mamlaka husika ndo zichukue sheria na sio kujichukulia sheria mkononi. Kufanya vile hakuna tofauti na wananchi wenye hasira wanaoua vibaka badala ya kuwafikisha katika vyombo vya sheria. Hapa ishu sio hijabu/mtandao ishu ni je wao ni mamlaka halali za kushughulikia suala hilo?
 
naiomba chadema itoe tamko hili.
bakwata iombe radhi kwa kuingilia maswala ya siasa wakati tendwa hawatambui.wavue kanzu waingie rasmi igunga wapige kampeni za wazi waeleze sera zao.
wananchi wakiwaelewa wawape kura.
 
bwana mkubwa hata kama ni muharifu kuna taratiibu za kufuata, zipo mamlaka ambazo zimeteuliwa kushughulikia waalifu, kama walimuona ni mualifu walitakiwa kuzipa taarifa mamlaka husika ndo zichukue sheria na sio kujichukulia sheria mkononi. Kufanya vile hakuna tofauti na wananchi wenye hasira wanaoua vibaka badala ya kuwafikisha katika vyombo vya sheria. Hapa ishu sio hijabu/mtandao ishu ni je wao ni mamlaka halali za kushughulikia suala hilo?
Mkuu, hakuna upofu mbaya kama upofu unaosababishwa na imani.

1) wewe ukimkuta mwizi nyumbani kwako huwa unapiga simu polisi waje kumkamata au unamkamata na kumpeleka polisi??........ina maana hata hii tu ambayo hata sio logic.......ni comonsense, wewe hujui?? au upofu wa imani???

2) Unapokamata mwizi, yeye huwa anakubali akamatwe tu kirahisi? tena akiwa na mali zako alizokuibia mfukoni??.......sasa kama yule Fatuma alikamatwa, akiwa na karatasi za maombi ya wasimamizi wa uchaguzi (kidhibiti) ulikuwa unategemea acheke na kusema waheshimiwa wananchi, twendeni polisi tu, kweli mmenikamata??.............imani isikupofushe!!
 
naiomba chadema itoe tamko hili.
bakwata iombe radhi kwa kuingilia maswala ya siasa wakati tendwa hawatambui.wavue kanzu waingie rasmi igunga wapige kampeni za wazi waeleze sera zao.
wananchi wakiwaelewa wawape kura.

mkuu, hapa umenikumbusha yale ya Arusha!!

inanichekesha sana, ni kwajinsi gani hawa mabwana wanavyoshughulika na mambo yasiyo na maana na madogo madogo.

Wamekuwa wakilalamika kuwa serikali imewaonea sana, imewapendelea wakristo..........ooh! mara shule, mara vyuo, mara mahospitali...........Inamaana wao wanaishia kulalamika tu???!! then wanasahau mambo hayo makubwa, wanaanza kushughulika na HIJAB ya DC wa Igunga.

WATU WA MAMBO MEPESI MEPESI NA YASIYO NA MAANA!!!
 
Waislamu kwanini mnakubali kudhalilishwa na waislamu feki hawa? msikubali uisalmu wenu uachafuliwe na wachache waliowekwa mfukoni na CCM, yaani kweli inawezekana kumkamata mtu usimshike sehemu? kwani mtandio unafungwa kwa kifungo/vifungo? si unaegeshwa tu? kwanza sio hijabu tangu lini akavaa hijabu yule? je Waislamu (naamini sio wote) wanatetea uchochezi na uongo?? Hapana sitaki kuamini hivyo.
 
kama cdm ni kweli kuna ajenda mbaya dhidi ya uislam nawashauri ombeni msamaha,kama hakuna ajenda yoyote mbaya na uislam,kuomba msamaha ni ujinga mzito ambao hautapata muzani wa kupimia. Mkiomba msamaha tu,magamba wamewapiga bao, wataanza oooh tulisema hawa wanampango mbaya na uislam,oooh tulisema hawa ni kanisa,si mnaona wamegundua mmewasitukia ndo wanajifanya bahati mbaya, hakika magamba watakuwa wameshinda kwa tko.

mimi nadahani shauri liko mahakamani na hivyo tuache sheria ichukue mkondo wake. Kuomba msamaha kwa nini sasa? Na nani aombwe msamaha bakwata au huyo mama?
 
jamani ile haikuwa hijabu bali ni mtandio ambao ata wakristo wanavaa

Huenda kwa imani yenu hijabu/mitandio mnaona kama si mavazi ya lazima

Ulazima wa hijabu katika uislamu:
Lakini katika uislamu ni lazima kwa wanawake kuvaa hijabu yameelezewa wazi katika Qur-ani, Kuna sehemu mbili katika Qur-ani ambazo zimeelezewa ulazima wa kuvaa hijabu kwa wanawake.

Moja ni katika Suratul Nuur aya ya 30 na 31, na sehemu nyengine ni katika Suratul-Ahzaab aya ya 59ni lazima kwa wanawake kuvaa hijabu yameelezewa wazi katika Qur-ani.

Endapo ulikuwa hujui uzito wa hijabu katika uislamu natumai umepata kujua lakini kama una nia ya ku challenge then nakutakia kila la kheri.
images
 
Ningefurahi sana kama viongozi wetu wa dini ya Kiislamu wangelaani wale waislamu wanaodhulumu kwa kupandisha bei za vitu katika maduka na vituo vyao vya mafuta, kunywa pombe na kula nyama ya mbuzi katoliki aka kiti moto wakati dini inakataza mambo haya. Hili swala la hijabu wangeliweka kwenye mikakati yao ya elimu kwa umma. Mbona nchini Ufaransa hijabu ilipigwa maruifuku na sikusikia sauti ya kiongozi wa dini ikipaazwa kulaani? Uchaguzi wa Igunga utaibua mengi, kukuza madogo kuwa makubwa na kufunika makubwa kuwa madogo (mfano: mgomo wa kuuza mafuta, ajali ya meli, uhaba wa sukari, mgao wa chakula Igunga, nk). Yetu macho na masikio.
 
Huenda kwa imani yenu hijabu/mitandio mnaona kama si mavazi ya lazima

Ulazima wa hijabu katika uislamu:
Lakini katika uislamu ni lazima kwa wanawake kuvaa hijabu yameelezewa wazi katika Qur-ani, Kuna sehemu mbili katika Qur-ani ambazo zimeelezewa ulazima wa kuvaa hijabu kwa wanawake.

Moja ni katika Suratul Nuur aya ya 30 na 31, na sehemu nyengine ni katika Suratul-Ahzaab aya ya 59ni lazima kwa wanawake kuvaa hijabu yameelezewa wazi katika Qur-ani.

Endapo ulikuwa hujui uzito wa hijabu katika uislamu natumai umepata kujua lakini kama una nia ya ku challenge then nakutakia kila la kheri.
images

Mbona hujafafanua kuhusu mtandio? Hijabu si hufungwa kwa mapini na hivo si rahisi kuvulika?mbona hii ya huyu mama ni kama mtandio bila mapini? Huyu mama mnafiki sana

Hapa kabla ya tukio kavaa mtandio:

07igu.jpg


Baada ya tukio kakumbuka hijabu:

09_11_72rf7k.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom