Wahusika muwaonee huruma watumishi wa wilaya ya Urambo

KIMBURU

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
210
189
Ni jambo la kusikitisha sana kuona mpaka leo tarehe "33" bado watumishi wa wilaya ya Urambo wanaowakilishwa bungeni na mh. Sitta na Kapuya hawajapata mishahara yao. Tabia hii ya kuchelewesha mishahara inaonekana kuota mizizi kwani hata mwezi uliopita mishahara ilitoka tarehe "34".

Mh. Rais na wote wanaohusika na hili naomba mlitilie maanani ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha watendaji wanaosababisha hali hii; kwani watumishi wa Urambo hasa walimu (sijajua sekta nyingine) wako kwenye hali ngumu na kuishia kukopakopa tu jambo linalowashushia heshima yao machoni pa jamii na hivyo kupunguza hata ufanisi wao wa kazi.

Na pia ni jambo la kusikitisha kuona watumishi wanasherehekea siku yao ya Mei mosi wakiwa hawana hata sent tano mfukoni.
 
Nashindwa kuelewa vizuri mkuu. Ninavyofahamu mishahara yote hutumwa kwenye akaunti za benki za watumishi nchi nzima kutoka hazina. Au bado kuna wanaopokea kutoka halimashauri?

Hata hivyo poleni sana. Pengine mishahara yenu inasaidia kulainisha magamba!
 
Pamoja na kuwa hulipwa na hazina kuna process za msingi zinaanzia halmashauri, wakichelewa hazina haina option zaidi ya kuchelewesha mishahara. Poleni sana wana Urambo, pigeni mnada jengo la Spika mstaafu
 
Back
Top Bottom