Wahusika Kampuni ya Uber Tanzania naomba msome hapa

Zemanda

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
5,707
11,961
Naandika huu uzi nikiwa na hisia zenye mchanganyiko wa hasira, jazba na huzuni.

Hivi kwann kampuni kama Uber ambaye ndie muanzilishi wa huduma ya usafiri kwa njia ya mtandao kwa gharama nafuu anahujumiwa na watendaji wake ndani ya kampuni kiasi hiki.

Huwezi fananisha au linganisha Uber na kampuni nyinginezo kama bolt, ping, indrive, eneo la uwekezaji katika mtandao namna jamaa wamejipanga kuanzia software hadi integrated system yao na zinginezo kama Google map, etc.

Kwann sasa kampuni kama Uber inakuwa ngumu kwa sisi wateja kupata madereva wa bodaboda kwa wakati maeneo ya katikati ya mji kama kariakoo eneo ambalo kuna mkusanyiko mkubwa sana wa watu ambao wanaingia na kutoka?

Unaita bodaboda wakati wa kurequest unaziona nyingi katika Map ila sasa gusa ile neno "REQUEST" uone balaa la kusubiria hapo. Utaona dereva wa bodaboda yupo mtaa wa nyuma kabisa ila anaelekea opposite direction kutoka direction uliyopo kumaanisha madereva wa bodaboda aidha wapo busy sana au na wamezidiwa abiria huku wakipokea request mpya.

So nataka kujua shida ni nini mbona Bolt ni tofauti. Ukirequest bodaboda wanakugombania shida ni app yao haieleweki. Unaweza shangaa bodaboda anakupigia simu yupo sinza na wewe umerequest ukiwa posta anakuuliza aje wapi sababu map inamuonyesha upo mwenge mataa.

Shida ni nini sana? Why app bora kama Uber yenye ubora on top of all apps iwe na supply ndogo sana ya bodaboda?

Uongozi wa Uber hebu kaeni chini na watu wenu wa masoko, nahisi kuna kazi hawafanyi sawa sawa. Soko ni kubwa sana hili na linawahitaji plus tunategemea huduma isambae hapa hadi mikoani huko iwe rahisi kupata huduma kwa njia ya mtandao.

Hebu waulizeni kwann wateja wanakaa muda mwingi kusubiria bodaboda na wanachelewa hadi wanaamua kucancell na kuchukua bodaboda kwa mdomo/mluzi.

Uber management,nadhani ni bora mfanye kuketi chini na watu wa masoko na mauzo ili kuweza kubaini kama kampuni mnafeli wapi kutengeneza jeshi la boda boda watakaotoa huduma vema bila usumbufu kwa wateja. Kimsingi team ya masoko na mauzo wamelala na wapo comfortable au watakuwa wapo na morale ya chini kushindwa kufanya kazi nzuri.
 
Uber kariakoo wana challenge root fupifupi. Ruti ikisoma buku mbili kariakoo hawaji. Ushaling'amua Hilo?
 
Nimeifanya iyo kazi kwa kipindi cha mwaka mzima na sasa nimeamua kuachana nayo.

Zipo sababu zinazopelekea masoko za hizi huduma ku feli moja wapo ikiwa ni pamoja na offers za mara kwa mara kwa wateja hili ninalizungumza in general sio uber pekee bali app zote za usafirishaji.

Unakuta bodaboda anahitaji kula,pikipiki inahitaji service, pikipiki iyo iyo inahitaji kulipiwa hesabu bado askari akikukamata anahitaji pesa au fine lkn kubwa kuliko viwango vya nauli ni vidogo haviendani na uhalisia lkn katka hali ya kushangaza hapo hapo kwenye nauli unakuta wametoa offer ambayo inakuumiza wewe dereva
 
Mimi nilijua wana incentives kwaajiri yenu madereva maana mnawafanyia kazi 24/7.
 
Back
Top Bottom