SoC03 Wahudumu wa afya, msinyanyase wagonjwa na wajawazito. Wanaosababisha vifo vya makusudi washitakiwe kwa mujibu wa sheria

Stories of Change - 2023 Competition

Fannjosh

Member
May 28, 2016
35
46
UTANGULIZI
Tunamshukuru Mungu kwa neema alotupatia kua hai hadi sasa. Ni jambo lisilopingika kwamba, kumekuwa na changamoto kubwa hasa kwa wahudumu wa Afya kutokujali wagonjwa na mara kadhaa kutojali akina mama wajawazito. Changamoto hii hupelekea baadhi ya wajawazito ama wagonjwa kupoteza maisha kwa uzembe wa wauguzi ama wahudumu wengine wa Afya.

Katika zahanati moja, aliwahi kufariki mama aliyeenda kujifungua. Mama huyo alikosa msaada wa muuguzi kwa sababu muuguzi alikuwa aki-chat huku mama aliyetayari kujifungua akiwa anahangaika mwenyewe kitandani bila msaada hadi kupoteza maisha yake pamoja na mtoto.

MADHARA YA WAHUDUMU WA AFYA KUTOJALI WAGONJWA NA WAJAWAZITO
  • Mgonjwa kupoteza uhai
Hili ni tatizo kubwa. Kutojali wagonjwa na akina mama wajawazito kumesababisha wengi wao kupoteza maisha. Inasikitisha sana kuona ndugu yako amepoteza maisha kwasababu ya uzembe wa mhudumu fulani wa afya.
  • Kusababisha magonjwa mengine
Kutomjali mgonjwa anapokuwa kwenye kituo cha huduma za Afya kunaweza kusababisha maambukizi ama kuzalishwa kwa magonjwa mengine. Mfano mama mjamzito anaweza kupata fistula baada ya kujifungua ikiwa hakupata msaada wa wauguzi kwa wakati.
  • Kupoteza uaminifu
Baadhi ya watu wakiugua hawaendi kwenye kituo cha afya ikiwa wanaamini kwamba, kituo hicho hakina huduma nzuri na hivyo kituo kinapoteza uaminifu wa raia hata kama wahudumu watakuwa wamebadilika. Hii ni mbaya zaidi kwani baadhi ya watu huweza kujihudumia wenyewe bila ushahuri wa daktari kwa kuamini kwamba wakienda kwenye kituo husika wanaweza kupoteza maisha.
  • Kudharau viongozi wa serikali serikali
Wauguzi na wahudumu wa afya wasio waaminifu huwa sababu ya watu kudharau serikali na kuona kama serikali haijali watu wake. Kama raia watapoteza uaminifu wao kwa serikali yao basi inakuwa vigumu kuirudisha imani hiyo.

NINI KIFANYIKE ILI KUONGEZA UWAJIBIKAJI WA WAHUDUMU WA AFYA
  1. Wahudumu wa Afya wapewe stahiki zao kwa wakati.
  2. Sheria ichukuliwe kwa wote wanaosababisha vifo vya wagonjwa au wajawazito kwa makusudi. Wanaofanya hivyo wanapaswa kupewa adhabu kama wauwaji wengine. Hii itaweka fundisho kwa wengine ili kila mtu ajue uhai ni bora kuliko fedha na madaraka. Ikiwa wakosaji watawajibishwa kwa mujibu wa sheria na sio kuwaamisha vituo vya kazi kwani hata huko waendako watarudia tabia hizo hizo.
  3. Semina za mara kwa mara kwa wahudumu wa Afya zifanyike. Serikali chini ya wizara husika itenge bajeti ya kutoa semina za maadili na wajibu wa wahudumu wa afya mara kwa mara ili kuamsha hali ya uwajibikaji pindi wanapokuwa katika huduma.
  4. Viongozi wa juu wa serikali wakemee na kulaani vitendo vya kutojali wangonjwa na wajawazito. Kwa kufanya hivyo, kila mhudumu atatambua kwamba anapaswa kutoa huduma kama taaluma yake inavyomwelekeza na kama maadili ya kazi yanavyotaka.

HITIMISHO
Kila mhudumu wa Afya atambue kwamba kazi yake amepewa dhamana ya kusaidia afya za watu na sio kuziangamiza. Wanaohudumia akina mama wajawazito watambue kwamba na wao walizaliwa. Wanaohudumia wagonjwa watambue kwamba na wao kesho wanaweza kuwa wagonjwa, Kama uongozi wa juu wa kituo husika utasimamia maadili ya taaluma ya afya ipasavyo, na kila mhudumu akatambua wito wake ipasavyo, basi vifo vya makusudi vya wagonjwa na akina mama wajawazito vitapungua sana.
 
Back
Top Bottom