Wahitimu wa Vyuo Vikuu Tanzania na mtazamo hasi dhidi ya ajira na kujiajiri

Aug 26, 2017
63
66
MTAZAMO HASI WA WAHITIMU WA VYUO VIKUU TANZANIA NA TATIZO LA AJIRA TANZANIA, NI NINI KIFANYIKE NA SULUHISHO LA TATIZO HILO NI LIPI?

NA, MrPhilosopher Kanju-MPK.

KISEMVULE, TANZANIA 10.02.2022
Nchini Tanzania kumekuwa na wimbi kubwa sana la wahitimu wengi wa vyuo vikuu na watimu hao baada ya kumaliza masomo yao huwa na matarajio makubwa sana ya kupata ajira kutoka serikalini. Kwa matarajio makubwa waliyo nayo wahitimu ya kupta ajira baada ya kuhitimu mavyuoni pale tu yatakapokwenda tofauti ndipo tatizo kubwa hutokekea na tatizo hilo si kwamba linawapata wahitimu wote laa ni baadhi tu ya wale wahitimu ambao huwa hawana mawazo mengine nje ya wazo kuu la kuajiliwa serikalini. Hivyo kwa kubweteka na kiwango kikukbwa cha elimu aliyo nayo mhitimu hupelekea kukaa tu mtaani bila kufanya kitu chochote kitakacho mletea maendeleo.

JE NI UPI MTAZAMO HASI WA BAADHI YA WAHITIMU WA VYUO VIKUU TANZANIA?

Kwa msomaji yeyote wa makala hii pale tu atakapoona kichwa cha habari cha makala hii kitu cha kwanza atajiuliza kwamba hii mwandishi wa makala hii anamaanisha nini? Anadhumuni gani? Na je analenga nin? Na maswali kadhaa wa kadhaa msomaji atakua anajiuliza.

Kwanza kabla ya kuandika makala hii nilifanya utafiti mdogo wa kuwahoji wahitimu wa vyuo vikuu kupitia utafiti huo ndipo nilipopata shauku ya kuandika makala hii na kupata angalau kwa kuanzia kuandika makala hii na kupata mtazamo hasi karibia kwa robo tatu ya wahitimu niliowahoji. Kitu kikubwa nilichogundua kwa wahitimu wa chuo kikuu kwanza wanajiona wana hadhi kubwa sana kulinganisha na watu ambao hawana elimu kubwa kujilinganisha na wao wenye elimu ya chuo kikuu. Pili wanajiona kwamba wao hadhi ya ni kufanya kazi katika maofisi na si kufanya kazi ambazo hazina mbele wala nyuma.

Tatu kujiona kwamba wameshafanikiwa na kutokua na shaukula kufanya kazi nyingine ngumu za kujiingizia kipato kwa kutegemea kwamba wao hadhi yao ni kuajiliwa na serikali hivyo kukaa tu nyumbani kwa kutegemea kamba ipo siku lazima waajiiwe na serikali au sekta binafsi. Nne kuwa na mtazamo kwamba wao kutoajiliwa na serikali ni kuonewa na kutotendewa haki na serikali kwa sababu ni wajibu wa serikali kuajiri hivyo wahitimu wenye mtazamo huu kubakia kishinda tu vijiweni na kwenye mitandao ya kijamii kuilaumu serikali kwa kutoajili.

TATIZO LA AJIRA TANZANIA.
Ni kweli kila mtu anatambua ya kwamba Tanzania kuna tatizo kubwa na la ajira kwa kutokana na wimbi kubwa sana la wahitimu vyuo vikuu na vyuo vya kati. Kuna watu watakua wanajiuliza maswali kwamba kwa nini awamu za utawala za vyuma kwa nini zilikua zinaajili na kwa nini hakukua na tatizo la ajira? Yapo mambo mengi sana yaliyopelekea kutoka kwa tatizo hili la ajira kama vila maswala ya kisera, mifumo mipya ya utawala ulio madarakani, ongezeko kubwa la ufaulu wa wanafunzi kupelekea udahili wa wanafunzi kuongezeka katika vyuo vikuu vya Tanzania hivyo kufanya ongezeko la wahitimu wa vyuo vikuu kuongeeka.

Pia uchumi wa nchi kua chini hivyo serikali kushindwa kuweka bajeti kubwa kwa ajili ya ajira na pia uwepo wa miradi mikubwa sana katika nchi ambayo inagharimu pesa nyingi sana hivyo pesa nyingi kuishia katika miradi hivyo. Kutokana na sababu kadhaa wa kadhaa serikali iliyopita ndiyo iliyopelekea wimbi la wahitimu wa vyuo vikuu kuwa wengi sana na kukosa ajira hivyo serikali iliyopo madarakani kushindwa kuajiri kutokana na namba sana ya wahitimu walio kuwepo mtaani.

JE NINI KIFANYIKE NA SULUHISHO LA TATIZO HILO NI LIPI?

Kwanza elimu ni mtaji mkubwa sana kwa sababu elimu humfanya mtu apevuke kiakili pia hupelekea mtu kupata maarifa mapya na pia kuwa na uwezo mzuri sana wa kufikiri na kuunda mawazo chanya. Lengo kubwa la elimu ni kumfanya mwanafunzi aelimike na kufanya mambo yake kwa ustadi wa hali ya juu na lengo kuu la elimu si kuajiriwa bali ni kuitumia elimu hiyo uliyo ipata ikunufaishe katika mambo yako na maendeleo yako kiujumla kama vile mwanafalsafa wa ugiriki ya kale aliyeitwa plato alipopata kusema kwamba “lengo la elimu ni kumfanya mtu awe na uwezo mzuri wa kufikiri na kuchakata maarifa. Na pia lengo lingine la elimu ni kupata jamii bora na viongozi bora”. Hivyo kutokana tu na maneno ya mwanafalsafa plato inatakiwa tuitumie elimu kutunufaisha sisi wenyewe katika maendeleo yetu na si kutegemea kuajiriwa.

Pia kwa sababu tumeshajua kwamba katika nchi yetu kuna tatizo la ajira kwa nini tusibadilishe mitazamo yetu kutoka kufikiria kuajiriwa na kuanza kujiajiri wenyewe? Kwa sababu akilini mwetu wazo la kuajiriwa likiwa bado lipo tunajidumaza wenyewe na kulemaa kwa sababu siku zote muda haukusubiri hivyo ukiendelea tu kukaa nyumbani bila kutafuta kazi yeyote ya kukuingizia pesa umri utazidi kukuacha na kutegemea kuajiriwa ikiwa huna uhakika wa kuajiriwa ni kujisababishia kufa masikini.

Na pia kuilaumu serikali kwa kutoajiri hakuifanyi serikali itoe ajira na itatoa ajira ikiwa tu wamepata pesa za kuajiri hivyo wahitimu wa vyuo vikuu wanatakiwa kubadili mtazamo huu kama wasomi na watumie elimu walizo pata kujiendeleza kimaisha kwa kufanya ujasiriamali au kitu chochote kinachokuingizia faida ni bora ajira ikukute ukiwa umejiajiri kwa sababu ajira itakuongezea motisha ya kuendeleza biashara yako kuliko kukaa tu nyumbani kusubiri ajira.
Kitu kingine wanafunzi wa vyuo vikuu wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwamba hakuna ajira kuna kujiajiri hii itawafanya hata wakihitimu kuanza kujiajiri na kuzitumia elimu walizopata kujiendeleza kimaisha na kuboresha bishara au miradi watakayoanzisha hii itawasaidia kutobweteka baada ya kuhitimu na wataipnguzia serikali kupunguza wimbi kubwa sana linalotaka kuajiriwa na itawasaidia wahitimu kutokuwa mizigo majumbani mwao baada ya kuhitimu.

Kitu kikubwa anachotakiwa kujiuliza mhitimu wa chuo kikuu baada ya kuhitimu ni kwamba je bora nikae tu nyumbani kusubiri ajira kutoka serikalini ambayo sina uhakika nayo au nijiajiri ambapo uweekano wa kufanya biashara na kutumia elimu yako ikunufaishe unao je kati ya viwili hivyo uchague kipi? Ukitumia vizuri uwezo wako wa kufikiri utapata majibu na hutokaa vijiweni kuitukana na kuilaumu serikali.

WAKO KATIKA UJENZI WA TAIFA.

NI MIMI MJOLI WAKO.

MRPHILOSOPHER KANJU-MPK.

PALE UTAKAPO NAKILI MAKALA ZANGU USISAHAU KU ACKNOWLEDGE.

EMAIL: Swaibkanju1@gmail.com

PHONE: 0655189430
 
Mimi ushairi wangu kwa watu mnaoshauri vijana, ni kuwa muweke uzani baina ya kile mnachomlingania kijana kukifanya(kujiajiri) na kitakachompa kijana hamasa ya kusoma.

Unamwambia ajiandae kisaikolojia kuwa ajira hakuna aje kujiajiri,sawa lakini sio wote wanasoma kozi ambazo wanaweza kujiajiri kwazo.

Hivyo akija kujiajiri maana yake anajiajiri nje ya kitu alichosomea.

Sasa kama ni hivyo unadhani kitu gani kitampa kijana hamasa ya kusoma ikiwa anajua anachokisomea hakitokuja kumnufaisha?

Hivyo kijana kuwa na hope kuwa atapata ajira ni lazima awenayo kwa sababu ndio inampa hamasa ya kusoma.

Nadhani nyinyi ni wajuvi hivyo mtajua namna ya kubalamce.
 
Watu hatutaki sijui serikali imletee ugali mtu ijengwe mifumo imara ya kuwezesha vijana wafanye mambo yao watafute riziki ya kila siku.Lakn imekuwa tofauti kwa serikali kukwepa jukumu lake na kuona vijana wapumbavu, na kukaa kwenye majukwaa ya siasa kuanza kuwasema.
 
Mkuu kwanza kabisa hawa vijana wahitimu hawana mtazamo hasi kama ulivyosema. Ukiangalia mambo yote uliyoyataja kama mtazamo hasi sio kweli kuwa ni hasi hata kidogo.

Kwanza angalia mfumo wetu wa elimu, uchambue kwa umakini utagundua mfumo wetu ndio umetoa aina ya elimu iliyowaelimisha vijana wetu kupata huu mtazamo, kivipi useme ni hasi?, haya ni matokeo chanya ya kimfumo, yaani mfumo umefanikiwa.

Sasa tujiulize je mfumi wetu wa elimu ni mbovu au je mfumo umepitwa na wakati?, La hasha mfumo wetu wa elimu sio mbovu wala haujapitwa na wakati bali ni kufanya mageuzi kwenye masomo tu na sio mfumo.

Mwaka 1984 Mwl. Nyerere akiongea na waalimu na wadau wa elimu alieleza vizuri sana sababu za kuwa na huu mfumo wa elimu ambao una likizo nne kwa mwaka na madarasa 7 kwa msingi, manne kwa elimu ya sekondari na mawili kwa elimu ya juu sekondari.

Tatizo kubwa sana ni wana taaluma kutokujua hasa sababu ya huu mfumo na kutokuhimiza kuutekeleza badala yake tunayumba yumba kama taifa.

Tuna likizo ya mwezi wa nne (msimu wa mvua) hii inatoa muda vijana kushiriki kilimo vijijini/nyumbani kwa kupanda mazao

Tuna likizo mwezi wa sita, hii inatoa nafasi kwa vijana kushiriki uvunwaji wa mazao mashambani

Tuna likizo mwezi wa tisa vile vile inatoa nafasi vijana kishiriki kilimo

Na mwisho likizo ya mwezi wa kumi na mbili inayotoa nafasi vijana kupumzika na kujiandaa kwa mwaka unaofuata.

Haya yote aliyaeleza bayana Mwl. Nyerere na kuwataka waalimu, watendaji wa vijiji na maafisa wengine wa serikali walisimamie hili kwa kufanya elimu inayotolewa shule iende sambamba na elimu ya maisha uraiani. Kwa bahati mbaya hili limebaki nadharia tu.

Badala yake vijana wamehitimu bila kukamilisha masomo waliyotakiwa kupitia kwa kipindi chote cha makuzi yao kitaaluma. Hawa vijana sio wakulaumu.

Mwisho kabisa serikali itafute fedha iajiri vijana tuachane na porojo za vijana jiajirini/hakuna nafasi za ajira wakati shuleni, hospitalini, mahakamani na ofisi nyingine nyingi zina uhaba wa wafanyakazi.

Shukrani.
 
Serikali itoe ajira na iache porojo ...huyo raisi mwenyewe amempa ajira mkwe wake..alishindwa nini kumpa mtaji wa mamilioni bwana mohammed ili afanye biashara na ajiajiri?...badala yake amemtoa Tamisemi amempeleka wizara ya michezo ili aendelee kula mema ya inji..
 
Mkuu umeleza na kufafanua vizuri sana kwamba tatizo lipo serikalini kwa hiyo unashauri vijana kwamba wabweteke na wasubiri mtaani hadi pale serikali itakapo yasimamia hayo uliyoyasema? Au unawashaurije hawa vijana wanaosubiri kuajiriwa ikiwa serikali imegoma kuajiri je waisubiri serikali hivyo hivyo hata kwa miaka 10 hadi pale itakapoajiri na vijana wakae tu nyumbani kama mzigo kwa wazazi wao?
 
Mimi ushairi wangu kwa watu mnaoshauri vijana, ni kuwa muweke uzani baina ya kile mnachomlingania kijana kukifanya(kujiajiri) na kitakachompa kijana hamasa ya kusoma.

Unamwambia ajiandae kisaikolojia kuwa ajira hakuna aje kujiajiri,sawa lakini sio wote wanasoma kozi ambazo wanaweza kujiajiri kwazo.

Hivyo akija kujiajiri maana yake anajiajiri nje ya kitu alichosomea.

Sasa kama ni hivyo unadhani kitu gani kitampa kijana hamasa ya kusoma ikiwa anajua anachokisomea hakitokuja kumnufaisha?

Hivyo kijana kuwa na hope kuwa atapata ajira ni lazima awenayo kwa sababu ndio inampa hamasa ya kusoma.

Nadhani nyinyi ni wajuvi hivyo mtajua namna ya kubalamce.
Mkuu upo sahihi sana kinachotokea hapa ni kwamba mwanafunzi akishafika level ya chuo kikuu kwa kada yeyote ile uwezo wake wa kufikiri lazima uongezeke.

Hivyo kwa kipindi ambacho ajira zimekua adimu anatakiwa kutumia maarifa aliyoyapata chuoni iwe katika vitabu mbalimbali hata kama kada yake aliyosomea hawezi kujiajiri lakini mtu huyu kesha elimika hivyo anaweza tumia ufanisi wake wa akili kuendesha guludumu la maisha yake nje na ajira ni bora ajira kama atapata imkute teali ana kitu chenye kumuingizia kipato ili aweze kuendesha maisha yake na asiwe tegemezi kwa wazazi wake.

Kwa sababu ajira teali ni tatizo hivyo huwezi kaa tu nyumbani zaidi ya miaka 5 ukisubiri ajira je hiyo miaka mitano ungejiongeza kufanya kitu ambacho kitakuongezea maisha ungepiga hatua.

Hivyo sio lazima kujiajiri kutokana na kitu ulicho somea.

Mfano mtu umesoma Philosophy utaajiliwa wapi na utajiajiri vipi kutokana na philosophy uliyosoma? Lakini kwa kusoma tu philosophy uwezo wako wa kufikiri utaongezeka na pia utakuwa na uwezo wa kubuni kitu chochote ambacho unaweza kukifanya na kikakuingizia faida iwe ujasiria mali, biashara , kilimo na kadharika hivyo maarifa uliyoyapata chuoni yanakuongezea ufanisi katika utendaji wa mambo yako. Na hata kama ni biashara umeanzisha utakuwa makini sana na mbunifu kwenye bishara yako. Yapo mengi sana mkuu wangu.
 
Suluhu ni kufumua mfumo mzima wa elimu kuanzia msingi mpaka chuo.

Watu wafundishwe kutafuta pesa badala kwa njia za ufugaji, udereva, kilimo, ufundi mbalimbali, biashara , ujasiriamal n.k
Naam mkuu hilo umeongea la maana inatakiwa mwanafunzi akimaliza asiwe tegemezi ajitegemee yeye mwenyewe ndio maana mwalimu anachukua nchi alianzisha Education for self reliance.
 
Serikali itoe ajira na iache porojo ...huyo raisi mwenyewe amempa ajira mkwe wake..alishindwa nini kumpa mtaji wa mamilioni bwana mohammed ili afanye biashara na ajiajiri?...badala yake amemtoa Tamisemi amempeleka wizara ya michezo ili aendelee kula mema ya inji..
Kwa hiyo mkuu Serikali kufanya hivyo je vijana wabweteke? Na je unawashaurije vijana? Maana ndio serikali imeamua hivyo na hakuna suluhisho kutoka serikalini.
 
Back
Top Bottom